JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NI KOSA KISHERIA MTUMISHI WA UMMA KUTOA SIRI ZA WATEJA

Kujadili taarifa za Wateja kwenye maeneo ya Umma kama Sokoni na kwenye Migahawa ni kuvunja #Haki ya faragha ya Mtu

Mtumishi anatakiwa kuendelea kutunza Siri za Mteja hata ikiwa amestaafu au kuacha kazi

#JamiiTalks #Privacy
FINLAND: Baada ya video kuvuja ikimuonesha akicheza muziki katika sherehe binafsi, Waziri Mkuu, Sanna Marin (36) amefanya vipimo vya kuthibitisha kuwa hakuwa ametumia Dawa za Kulevya

> Hii ni baada ya kudaiwa kuwa alikuwa ametumia dawa hizo

Soma https://jamii.app/FinlandPolitics

#Privacy #Accountability
😁7👍3🎉1
Mdau wa JamiiForums.com anasema ni jukumu la kila mmoja kulinda na kuheshimu faragha ya mwingine kwa kukemea tabia ya Kuwarekodi Watu wakiwa sehemu za Starehe au kwenye Sherehe na kuweka Mtandaoni bila ridhaa yao

Anasema mtindo huu ni hatari kwasababu wakati mwingine Video hizo huweza 'kutrend' na kuwafikia Watu wa Karibu, kudhihakiwa Mtandaoni na kuambiwa maneno mabaya yanayoweza kuathiri Afya ya Akili ya Mhusika pamoja na Uhusiano wa Kijamii

Umewahi kukutana na Video inayokuhusu Wewe, Ndugu au Rafiki yako 'ikitrend' Mtandaoni?

Mjadala https://jamii.app/InvasionOfPrivacy

#JamiiForums #Privacy #DigitalRights #Accountability
JFHUDUMA: Kero ya Vijana wa Kiume kudaiwa kuwachungulia Wanawake wanaojifungua katika Zahanati ya #Isevya, Mkoani Tabora, imeibuliwa baada ya baadhi ya Wanawake ambao wamewahi kujifungulia hapo kuiomba Serikali kujenga uzio mrefu kuzunguka Zahanati hiyo ili kukomesha kero hiyo

Tovuti ya #Mwananchi imeripoti kuwa Vijana hao huchungulia kupitia uwazi uliopo kutokana na eneo la Zahanati kutokuwa na uzio hivyo kuwa na ugumu katika udhibiti wa mwingiliano wa watu wa nje

Tovuti hiyo pia imeripoti kuwa Muuguzi wa Zahanati hiyo alisema changamoto hiyo ipo na wameifikisha kwenye Mamlaka husika kwaajili ya kushughulikiwa baada ya malalamiko kuwa mengi

Soma https://jamii.app/ZahanatiIsevya

#JamiiForums #Privacy #Afya #ServiceDelivery #Accountability #Governance #Uwajibikaji
1