JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Utaratibu wa kulipia huduma za '#TwitterBlue' ulioanza rasmi Aprili 20, 2023 umewaathiri Mastaa wa Muziki Tanzania wakiwemo #DiamondPlatnumz, Alikiba na #Harmonize ambao wameondolewa Tiki za Uthibitisho (Verified Badge/Check) kwa kutolipia Tsh. 18,764

Watu maarufu wengine walioondolewa 'Tiki ya Blue' ni pamoja na wanamuziki #Beyonce, DJ Khaled, #BurnaBoy, Davido #Wizkid pamoja na Rais wa zamani wa Marekani, #DonaldTrump. Hata hivyo #ElonMusk ametangaza kumlipia Mcheza Kikapu #LeBronJames

Vipi Mdau, utalipa Pesa ili kubaki na 'Blue Tick'?

#JamiiForums #Entertainment #DigitalRights #JFDigitali
πŸ‘6
MDAU: NI DHARAU WASANII KUGOMA KUHUDHURIA TUZO ZA MUZIKI NCHINI

Anasema Wasanii wa #Tanzania wanajiona 'Mastaa' na kudharau Watanzania wenzao kwa 'kuzikaushia' Tuzo hizo muhimu na kuishia kutuma Wawakilishi

Anasema Aprili 29, 2023 zimetolewa tuzo kibao bila wahusika kuwepo, mfano; #Zuchu, #AllyKiba, #Barnaba, #Nandy, #Harmonize na #DiamondPlatnums kama vile hawakuwa na taarifa. Ajabu ni kuwa hadi ma 'DJ' nao hawakutokea

Ameshauri Wasanii kuacha dharau na kujiona wakubwa

Soma https://jamii.app/TMAKususiwa

#TMA2022 #TanzaniaMusicAwards
πŸ‘6
Ujumbe huu wa Msanii wa #BongoFleva, Rajab Abdul Kahali "#Harmonize" unapatikana kwenye Wimbo wa Never Give Up aliouweka YouTube, Mei 24, 2019 akisisitiza kutolipa kisasi, kuwa makini na marafiki na kutokata tamaa kwenye harakati za #Maisha

Video iliongozwa na 'director' Kenny na kurekodiwa katika Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam ambapo imetazamwa zaidi ya mara Milioni 17.7

#JFNukuu #GoodMorning #Entertainment #Quotes #AmkaNaJF #JamiiForums
πŸ‘9❀2
Wimbo β€œMatatizo” wa #Harmonize, ulioachiwa Mwaka 2016, unazungumzia changamoto za Maisha wanazokutana nazo Vijana wengi katika utafutaji na upambanaji

Zaidi https://jamii.app/MatatizoWimbo

#JamiiForums #JFNukuu #Goodmorning #Quotes #AmkaNaJF #Entertainment
❀2πŸ‘1
BURUDANI: Msanii wa #Bongofleva Rajab Abdul β€˜#Harmonize’ atakiwa kuilipa Benki ya #CRDB fidia ya Millioni 10, gharama za kesi na Deni la Mkopo la Tsh. Milioni 103 baada ya kushindwa kulipa kikamilifu Mkopo wa Tsh. Milioni 300 tokea Mwaka 2019

Aidha, CRDB na Harmonize walikubaliana angefungua akaunti ya Kibiashara katika benki hiyo kisha kuweka Tsh. Milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za Kibiashara, lakini alikiuka makubaliano hayo

Benki ya CRDB ilifikia uamuzi wa kwenda Mahakamani baada ya usumbufu wa ulipaji deni kutoka kwa msanii huyo, ambapo Mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Msanii huyo lakini hakufika Mahakamani

Soma https://jamii.app/HarmonizeKuwalipaCrdb

#JamiiForums #Accountability
πŸ‘8❀1πŸ‘1