KAGERA: Watu kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Wilayani Karagwe, ikihusisha Lori la mizigo na magari mawili ya Abiria
Akizungumza na Kasibante FM, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Kalanga Lisser amesema “Siwezi kuthibitisha idadi ya waliopoteza maisha lakini miili inapelekwa kuhifadhiwa, majeruhi wanapatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya na wengine wanaweza kupelekwa Hospitali ya Mkoa.”
Amesema Lori lilikuwa limebeba maparachichi limegonga kwa nyuma Gari la Abiria Toyota Hiace lililokuwa likitokea Karagwe kwenda Bukoba, ambapo Hiace hiyo nayo ikagonga Costa iliyokuwa ikitoka Bukoba kwenda Karagwe
Soma https://jamii.app/AjaliKaragwe
#JFMatukio #JamiiForums

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Akizungumza katika Kongamano la Afrika la Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Meya wa Entebbe, Fabrice Rulinda anasema “Watu wamekuwa na uhuru wa kutoa taarifa za wengine bila ridhaa zao, mfano unaweza kupigiwa simu kuwa mtu fulani alikopa na kama hatalipa tutakufuata wewe.”
Ameongeza kuwa hiyo ni kero na inaonesha jinsi kulivyo na upungufu wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ambapo pia amesema hali hiyo imekuwa ikisababisha Watu wengi kupokea matangazo mbalimbali, ambayo hawakuwahi kuridhia kuyapokea au kutoa namba zao kwa wanaotuma matangazo hayo
Amesema katika Kongamano la Afrika kuhusiana na Ulinzi wa Taarifa Binafsi jijini Kampala linaloendeshwa na ADRH (Africa Digital Rights Hub) ikishirikiana na JamiiForums pamoja na Wadau wengine, likihusisha Mafunzo, Mijadala na kubadilishana uzoefu katika Ulinzi wa taarifa Binafsi na Faragha za Watu
Fuatilia https://jamii.app/DPAS2024
#JamiiForums #PrivacyAfrica #DataProtection #DPAS2024 #DigitalWorld

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia Watoza Ushuru wa Magari ya Mizigo kwenye Eneo la Mpanda, akidai kuna Mazingira ya 'upigaji'
Soma https://jamii.app/WiziUshuruMpanda
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji

DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto ya vibanda na makontena yaliyopo maeneo ya Urafiki kufanywa 'Madanguro', huku pia watu wakiyatumia kujisaidia hivyo
Soma https://jamii.app/MakontenaKutumikaHovyo
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability

KOREA KUSINI: Wabunge 190 kati ya 300 wamepiga Kura ya kuzuia utekelezwaji wa Amri ya Rais Yoon Suk Yeol ya kutangaza Utawala wa Kijeshi, baada ya kuwatuhumu Wabunge wa upinzani kupingana na Serikali yake, pamoja na kushirikiana na Korea Kaskazini
Muda mfupi baada ya Amri hiyo kutolewa, Vikosi vya Kijeshi viliripotiwa kuzingira Bunge kwaajili ya kutekeleza Amri ya Rais lakini Wabunge wamefanikiwa kupiga Kura na kuifuta, ambapo Spika wa Bunge, Woo Won Shik amesema Amri ya Kiijeshi ilikuwa "Batili" na kwamba Wabunge watalinda demokrasia na watu
Kwa mujibu wa baadhi ya Sheria za Utawala wa Kijeshi ni pamoja Vyombo vya habari na machapisho yote kuwa chini ya udhibiti wa Kijeshi, Migomo na mikusanyiko inayochochea machafuko ya kijamii inapigwa marufuku, huku Watumishi wa Afya wakiwemo Madaktari waliopo kwenye Mgomo kwa zaidi ya miezi 11 wakitakiwa kurejea kazini ndani ya saa 48
Soma https://jamii.app/SouthKoreaMartialLaw
#JamiiForums #Governance #Democracy

NAMIBIA: Chama Tawala cha South West Africa People’s Organisation (SWAPO) kimefanikiwa kubaki Madarakani baada ya Mgombea wake Netumbo Nandi-Ndaitwah (72), kushinda nafasi ya Urais kwa 57.31% na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Nchi hiyo
Atakuwa Rais wa 5 wa Namibia na Mwanamke mwingine anayeingia katika orodha ya Marais Wanawake Barani Afrika, inayowajumuisha Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia (2006 - 2018), Joyce Banda wa Malawi (2012 - 2014), Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuanzia 2021 hadi sasa, nk
Alikuwa Makamu wa Rais wa Chama cha SWAPO chini ya Rais Hage Geingob, aliyefariki Februari 2024 na Makamu wa Rais anayemaliza muda wake, Nangolo Mbumba, aliyeendelea na jukumu la mpito baada ya kifo cha Geingob
Soma https://jamii.app/SWAPOAgain
#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights

MAREKANI: Mwigizaji Kerry Washington (47) ameingia katika orodha ya Mastaa wa Filamu waliopata heshima ya kupewa Tuzo ya Nyota ya Hollywood Walk of Fame, kwa kutambua kazi kazi zake alizoigiza kwa takriban Miaka 30
Washington alijizolea umaarufu zaidi akiwa ni mmoja kati ya Waigizaji wa tamthilia za Scandal, Confirmation, Little Fires Everywhere na n.k
Mdau, ulivutiwa na uigizaji wa Kerry kwenye Movie au Series gani?
Soma https://jamii.app/KerryHollywoodFameStar
#JamiiForums #HollywoodWalkofFame #JFEntertainment

Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu Ubora wa Vifaa vya Ujenzi vinavyoingizwa Sokoni kwa sasa na pia, baadhi ya Maafisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) wachunguzwe, akidai wengi wao wanaoingia ‘field’ kufanya ukaguzi wanajua kinachoendelea
Mdau anasema kwa kuwa kazi zake zinahusisha Vifaa vya Ujenzi, amegundua vingi havina ubora kama ilivyokuwa hapo awali
Soma https://jamii.app/UbovuVifaaUjenzi
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Mdau anasema kwa kuwa kazi zake zinahusisha Vifaa vya Ujenzi, amegundua vingi havina ubora kama ilivyokuwa hapo awali
Soma https://jamii.app/UbovuVifaaUjenzi
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
USAFIRISHAJI: Treni ya Abiria ya Kisasa (SGR) iliyokuwa ikitokea Dar kuelekea Dodoma imeripotiwa kukwama katika Stesheni ya Kilosa Mkoani Morogoro kwa kilichoelezwa kuwa ni hitilafu ya Umeme na hivyo kusababisha safari hiyo kushindwa kuendelea
JamiiForums imewasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Fredy Mwanjala kuhusu taarifa hiyo, amesema “Siwezi kuzungumzia hilo kwa sasa hadi nitakapopata taarifa ya mafundi.”
Ikumbukwe, Julai 30, 2024, TRC iliomba radhi kutokana na hitilafu ya Kukatika kwa Umeme iliyosababisha Treni ya #SGR kutoka Dar - Dodoma kusimama kwa zaidi ya Saa 2 kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete, taarifa ya awali ilionesha ilisababishwa na Ngedere au Bundi wanapogusa Nyaya za Umeme zilizotandazwa juu ya Reli
Soma https://jamii.app/SGRKilosa
#JamiiForums #Governance #JFHuduma #ServiceDelivery