JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAGONJWA YA AFYA YA AKILI YANATIBIKA NA KUEPUKIKA, TUVUNJE UKIMYA

Mdau anasema Jamii inapaswa kuwaonyesha Upendo wenye Matatizo ya Afya ya Akili na kutowatenga. Pia, kuwepo utaratibu wa kuwasaidia katika mahitaji yao ya msingi ikiwemo kuwapeleka kupata huduma

Soma - https://jamii.app/AfyaAkiliSOC

#StoriesOfChange #JFAfya
SARATANI: Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya (WHO) Mwaka 2020 zinaeleza ongezeko la Visa vipya vya Saratani linakadiriwa kufikia Milioni 19.3, huku Vifo vikiwa Milioni 10

Ulimwenguni kote, inakadiriwa Visa vipya Milioni 28.4 vya Saratani vinaweza kutokea hadi kufikia Mwaka 2040, huku ongezeko kubwa likiwa katika Ukanda wa Nchi zinazoendelea

#JamiiForums #Cancer #JFData
TANZANIA KUFANYA MAKUBALIANO YA KUTENGENEZA NDEGE NDOGO

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kipo ktk hatua za mwisho za majadiliano na Kampuni ya #Skyleader inayotengeneza Ndege ndogo ili ifanye Uwekezaji wa Ndege hizo Nchini Tanzania

Soma - https://jamii.app/Ultralight
#COVID19: Shirika la Afya (WHO) limesema Maambukizi vya Corona yamepungua kwa 19% Wiki iliyopita. Visa vipya Milioni 16 na Vifo 75,000 viliripotiwa kuanzia Februari 7 - 13, 2022

Virusi aina ya Alpha, Beta na #Delta vinaendelea kupungua

Soma - https://jamii.app/WHOCovid

#UVIKO3
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema baadhi ya Watanzania walijifanya Wagonjwa wa COVID-19 na kwenda kutibiwa #India lakini walikuwa wakibeba #DawaZaKulevya

Watumishi wa Afya wametakiwa kuwa makini wanapotoa vibali

Soma - https://jamii.app/CoronaDawaZaKulevya

#JFMatukio
KIGOMA: WANAFUNZI WADAIWA KUJISAIDIA VICHAKANI BAADA YA VYOO VYA SHULE KUTITIA

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kasaba wako hatarini kupata Magonjwa ya mlipuko kutokana na kutokuwa na Huduma ya Vyoo tangu Mwaka 2020 baada ya vilivyokuwepo kutitia

Soma - https://jamii.app/WnfzVyooTitia

#JFUwajibikaji #HakiMtoto
#SOMALIA: Wanamgambo wa Al-Shabaab wameshambulia Vituo viwili vya Polisi Mjini #Mogadishu na kusababisha vifo vya Watu 5 na majeruhi 16

Shambulio hilo limetokea Februari 16. Serikali imesema shambulio limeshadhibitiwa na Vikosi vya Usalama

Soma - https://jamii.app/AlshababSomalia
#JFLeo
BRUSSELS, UBELGIJI: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya Lissu kukutana na kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali

Lissu amwomba Rais afanye analoweza kwa Mamlaka yake ili Kesi dhidi ya Mbowe iondolewe

Soma zaidi > https://jamii.app/LissuRaisSamia

#Governance
BURKINA FASO: Jeshi Nchini humo limeahidi kushirikiana na ECOWAS katika kurejesha Mchakato wa Uchaguzi wa Kidemokrasia

Hata hivyo, haijawekwa wazi ni muda gani Luteni Kanali Paul-Henri Damiba aliyeapishwa kuwa Rais wa Taifa hilo atakaa Madarakani

Soma - https://jamii.app/UtawalaJeshiBF

#JFDiplomasia
#MICHEZO: TFF imemfungia kwa miaka 5 pamoja na faini Tsh. milioni 6, Shaffih Dauda kujihusisha na masuala ya Soka ndani na nje ya Nchi

Dauda alilalamikiwa kwa kuandika TFF kuwa sio kama Nyumba ya Kupanga inayoongoza kiimla na mwenye Nyumba

Soma - https://jamii.app/ShafiiTFF

#JFSports
UJERUMANI NA AUSTRIA KULEGEZA KANUNI ZA #COVID19

Ujerumani italegeza Kanuni kufuatia Wimbi la Maambukizi kutokana na Kirusi cha #Omicron kuonekana limepita kilele chake

Serikali ya Austria italegeza asilimia kubwa ya Kanuni kuanzia Machi 5

Soma https://jamii.app/KanuniUVIKO

#UVIKO3 #Governance
NCHI TATU ZA AFRIKA KUPEWA VIFAA VYA KUZALISHA CHANJO

Kampuni ya BioNTech na #Pfizer zitaleta Vifaa vya kutengeneza Chanjo #Rwanda, Senegal na Afrika Kusini Julai 2022

Vitawezesha utengenezaji wa Chanjo ya #CoronaVirus, #Malaria na Kifua Kikuu

Soma - https://jamii.app/VifaaChanjo

#JFAfya
RAIS MWINYI: #ZANZIBAR HAINA WAGONJWA WA UVIKO-19

Serikali imesema hivi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja, lakini haiwezi kuweka wazi kama Ugonjwa umeisha moja kwa moja

Imeelezwa, hakuna kisa kipya kwa Wakazi wala Wageni tangu Januari 2022

Soma - https://jamii.app/COVIDZnz

#UVIKO3 #JFAfya
DKT. NDUGULILE: SERIKALI ILIPE DENI LA NSSF ILI KUONDOA TOZO DARAJA LA KIGAMBONI

Mbunge Dkt. Faustine Ndugulile amesema Wakazi wa Kigamboni hawana njia mbadala ya kutumia kama ilivyo kwa wa Msasani, Masaki na wengine wanaotumia Daraja la Tanzanite

Soma - https://jamii.app/DarajaNyerere

#Governance
UFARANSA KUONDOA VIKOSI VYAKE MALI

Rais Emmanuel Macron asema Vikosi vya Nchi hiyo vitaondoka Mali baada ya takriban miaka 10 ya kushirikiana na Wanajeshi wa Taifa hilo

Uamuzi huo umekuja wakati kuna uhasama kutoka kwa Utawala wa Kijeshi

Soma - https://jamii.app/FrenchTroopsMali

#JFDiplomasia
MOROGORO: AJALI ZA BODABODA ZATAJWA KUONGEZA WAGONJWA WA KIFAFA

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu na Ubongo kwa Watoto, Dkt. Edward Kija amesema Watu 30 kati ya 100 ktk wilaya ya Mahenge wana Kifafa

Ajali za Bodaboda huchangia Ugonjwa huo kwa kuwa Watu hugonga Vichwa na kuathiri Ubongo, hasa wanapokuwa hawajavaa Kofia ngumu (Helmet)

Soma - https://jamii.app/KifafaMahenge

#EpilepsyAwareness #JFAfya
BUNGENI: Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imeshauri Serikali kujenga maghala makubwa yenye kuhifadhi Mafuta zaidi ya Lita za ujazo Milioni 1.25

Imesema hatua hiyo itawezesha kuagiza mafuta zaidi wakati Bei imeshuka katika Soko la Dunia

Soma - https://jamii.app/KamatiBeiMafuta

#Governance
MOSHI: WAFANYABIASHARA WATAKA UCHUNGUZI WA MOTO SOKONI, WADAI NI NJAMA

Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko la Mbuyuni waomba Serikali kuunda Tume kuchunguza chanzo cha Moto uliotokea Februari 15, 2022 na kuteketeza Maduka 3 eneo la Stendi ya Mboya

Soma - https://jamii.app/TumeMotoSoko

#JFUwajibikaji
NJOMBE: WANAOTUHUMIWA KUMUUA KATIBU WA KANISA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Waliofikishwa Mahakamani ni Daniel Mwilango (Katekista) na Nickson Nyamideko

Nickson Myamba aliyekuwa Katibu wa Baraza la Walei Kigango cha Makambako aliuawa kwa kukatwa mapanga

Soma - https://jamii.app/MauajiKatibu

#JFMatukio
Rais wa #Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametengua Uteuzi wa Salum Yussuf Ali ambaye alikuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) ili kupisha uchunguzi wa Ubadhirifu wa Tsh. Bilioni 9

Salum Yussuf alishika wadhifa huo tangu Machi 2021

Soma - https://jamii.app/KamishnaZRB

#JFUwajibikaji #Governance