JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki anaomba ushauri kuhusu changamoto ya mahusiano anayopitia, ameeleza kuwa awali aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi ya dhati, baadaye alisalitiwa hadi mpenzi wake akapata ujauzito wa mwanaume mwingine.

Anasema kwa sasa ana mwenza mpya na uhusiano wao upo vizuri, lakini bado anapata ugumu kuamini masuala ya ndoa, kwani kila akikumbuka yaliyompata huko nyuma moyo wake unakuwa mgumu.

Kushiriki mjadala soma https://jamii.app/KupendaTena

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMahusiano
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo Agosti 24, 2025 kwa njia ya Mtandao, Mwanasiasa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema, “Mungu akituvusha, nashauri Sheria irekebishwe ili Viongozi (Rais) wawajibishwe kwa kushtakiwa kwa makosa waliyoyafanya wakiwa madarakani.”

Soma https://jamii.app/PolepoleTumeuzwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa
4👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza kwa njia ya Mtandao, Agosti 24, 2025, Mwanasiasa na Kada wa CCM, Humphrey Polepole amesema Mfanyabiashara Rostam Aziz ameuziwa Asilimia 70 ya Mgodi wa Makaa ambao ni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati kwa kiwango cha Tsh. Bilioni 5 na kwamba ameshalipa Tsh. Bilioni 2.5.

Zaidi soma https://jamii.app/PolepoleMakaa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa
3👎2
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiAfrica #JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
👏2
ARUSHA: Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la Mtu mmoja aitwaye Bakari Halifa Daud (18) Mkazi wa Sombetini kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na Abdulaziz Abubakari (Dogo Janja).

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 Saa 5:30 Usiku maeneo ya Sombetini na kwamba Jeshi linawashikilia Watu wawili kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.

SACP Masejo ameongeza kuwa wakati Abdulaziz Abubakari (30), Mkazi wa Levolosi akiwa anashuka kwenye gari alidai kutaka kuvamiwa na Bakari akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi hali iliyosababisha kutumia silaha aliyokuwa nayo.

Zaidi https://jamii.app/DogoJanjaKumpigaRisasi

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #Uwajibikaji
Mdau ikiwa mwenza uliyeachana nae ameshinda kiasi kikubwa cha fedha unaweza kuamua kurudiana nae au utakaza uendelee na Maisha yako?

Shiriki mjadala huu https://jamii.app/TalakaNaEx

#JamiiForums #JamiiAfrica #JukwaaLaMahusiano #Maisha #JFChitChats
🔥1
Kupitia Jukwaa la Entertainment ndani ya JamiiForums.com Waadau wanajadili kuhusu nyimbo za Kitanzania ambazo zilifanya vizuri ngazi ya Kimataifa kiasi cha kuweza kuutangaza muziki wa Bongo Fleva kwa kiwango kikubwa.

Unadhani ngoma gani kati ya hizi au kama nyingine ilitoboa zaidi Kimataifa?

Shiriki mjadala huu https://jamii.app/HitKimataifa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFBurudani #JFEntertainment #JFBongoFleva
Mwanasaikolojia Nadia Ahmed amesema kuwa kauli za Chuki Mtandaoni huleta madhara mbalimbali ya Kisaikolojia kwa Mtu anayekumbana nazo Mtandaoni na husababisha kuathiri matendo na maamuzi ya muhusika.

Tembelea Jukwaa la JamiiForums.com

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju akifungua Mkutano wa Tisa wa Kamati ya Utatu kwenye Ukumbi wa PSSSF TOWER - Mawasiliano, leo Agosti 25, 2025 amesema angependelea utaratibu wa Kikokotoo kwa Watumishi wa Serikali Kuu kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Jaji Masaju alisema “Haiwezekani mimi nastaafu kisha ndiyo mnaanza kusema sijui nilete hiki, nilete hiki. Taarifa hizi mlikuwa nazo kuanzia mwanzo, kabla ya kustaafu niliwapa taarifa miezi sita kabla. Sisi tungependa Kikokotoo kirudi kwa Watumishi wa Serikali Kuu kama ilivyokuwa.”

Zaidi Soma https://jamii.app/JajiMkuuKikotoo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Kikotoo
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Siasa anasema katika kipindi hiki cha Uchaguzi na uteuzi wa Wagombea, Wananchi wameonekana kuwakataa wale Wagombea walioteuliwa na chama husika.

Shiriki Mjadala https://jamii.app/MtuBinafsi

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
KILIMANJARO: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Serikali Kuu na Mamlaka za juu za Usalama kuingilia kati na kuchukua hatua juu ya matukio yanayoendelea kati ya Wakulima dhidi ya Wafugaji katika Kijiji cha Mbatakero, Wilaya ya Hai, akidai kuna uvamizi unaoathiri Watu, Mazao, mali na kutishia uhai wa Watu.

Mdau anadai mgogoro huo umesababisha kuwe na matumizi ya ndivyo sivyo ya silaha za jadi na kwamba walalamikaji wanapowasilisha hoja zao kwa Mamlaka mbalimbali hazifanyiwi kazi kwa usahihi.

Anadai baadhi ya Wananchi wameanza kuhamasishana kujilinda wao, mali zao na afya zao na kwamba wamefikisha malalamiko yao katika Vyombo vya Habari vya Mkoani hapo navyo vimekuwa na uzito wa kuwasikiliza hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama hakutakuwa na muongozo wa Serikali.

Zaidi soma https://jamii.app/KijijiChaMbatakero

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #JFMdau2025
2
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change (SoC) 2021 katika andiko lake alieleza namna ambavyo ucheleweshwaji wa maamuzi ya kesi Mahakamani unavyoweza kuathiri #Demokrasia na kuminya Haki za Binadamu hasa katika harakati za kutetea mabadiliko muhimu ya nchi.

Hivyo, amependekeza kuongezwa kwa majaji, kuboresha Miundombinu ya Mahakama, Wahusika wa Sheria kuwajibika inavyotakiwa katika ngazi zote.

Soma zaidi https://jamii.app/KesiKuchelewa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #HumanRights #StoriesOfChange
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa zamani wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akizungumza kwa njia ya Mtandao, leo Agosti 25, 2025, amesema Viongozi ambao hawanyenyekei na kusikiliza malalamiko ya Wananchi basi uongozi wa Viongozi hao haujatoka kwa Wananchi bali umetoka sehemu nyingine hata Wananchi wakilia na kuomboleza.

Ameyasema hayo leo Agosti 25, 2025 akiwa anazungumza Mtandaoni.

Zaidi https://jamii.app/HotubaYaGwajima

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #FreedomOfExpression
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza kwa njia ya Mtandao, aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, leo Agosti 25, 2025 amesema kwamba kama hoja alizoziibua aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa #CCM, Humphrey Polepole zinaukweli, basi anampongeza kwa ujasiri wake wa kujitokeza na kuzungumza hadharani.

Askofu Gwajima amesema: “Niseme tu ukweli wangu, kama haya mambo aliyoyasema Polepole ni ya kweli basi ninampongeza sana kwa ujasiri huo kwa sababu ili haki iweze kutawala katika nchi ni lazima ianzie kwenye chama chetu.”

Zaidi Soma https://jamii.app/HotubaYaGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akizungumza kwa njia ya Mtandao, leo Agosti 25, 2025 amesema mwisho wenye afya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaweza kupatikana tu pale ambapo haki itatawala, na kuongeza kuwa ni vyema chama hicho kikawakumbatia zaidi Watu wanaoweza kusema ukweli.

Soma Zaidi: https://jamii.app/HotubaYaGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki akiongelea kuhusu Mikataba na Leseni za Madini bungeni Juni 13, 2017 kwenye kikao cha Bajeti ya Serikali 2017/2018.

Soma Zaidi https://jamii.app/LissuMadini

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKumbukizi
2
Siku yenye mafanikio hujengwa kwa mpangilio mzuri na nidhamu binafsi, huku ukizingatia uwiano kati ya kazi na afya.

Je, Mdau, una mbinu au mikakati maalum ya kuendesha siku yako kwa ufanisi?

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Agosti 26, 2025, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema kumekuwapo na msisitizo mkubwa wa kulinda amani nchini huku haki ikisahaulika.

Amesema ni muhimu kutambua kuwa amani ya kweli haiwezi kuwepo bila haki na kwamba msisitizo wao kama Tanganyika Law Society (#TLS) ni kuuangalia Uchaguzi katika msingi wa haki, amani na utulivu.

Soma Zaidi https://jamii.app/TamkoTLS

#JamiiForums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema, "Hatukatai kwamba kulikuwa na mabadiliko, yamefanyika ya Kisheria kwenye Sheria za Uchaguzi lakini tuwe wakweli, unapobadilisha unataka kutibu nini? Hiyo ndiyo hoja, siyo mabadiliko tu."

Ameongeza kwa kusema, "Tunapoangalia zoezi la Uchaguzi lazima liwe lenye kuwajibika, usawa, uwazi, kutoa heshima na thamani ya Kura."

Soma https://jamii.app/MwabukusiTamko

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (#TLS), Boniface Mwabukusi amesema “Sasa hivi Watu wanatekwa, wanapotea. Lazima Taifa tukae pamoja tujadiliane shida iko wapi, na tunapowaomba Viongozi wetu watusikilize wasione kama Watu tunaowaghasi kwenye utulivu, bali watambue tuna nia njema.”

Amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Agosti 26, 2025.

Soma https://jamii.app/TumezoeaKutekwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025