JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (#TLS), Profesa Edward Hoseah, amesema “Miaka michache iliyopita Jeshi la Polisi na baadhi ya Vyombo vya Dola vilikuwa na wimbi la kuwakamata Mawakili ovyo pasipo kufuata Sheria”

Ameeleza “Kwa ushirikiano na Serikali wimbi hilo limeanza kutulia, natoa wito kwa Vyombo vya Dola kuendelea kuwaheshimu Mawakili kwa kuwa ni Maafisa wa Mahakama"

Soma https://jamii.app/MkutanoMawakili

#Democracy #Governance
👍1
Mchakato wa kupiga kura katika Uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) umesimama baada ya Karatasi za Kura kumalizika, hivyo baadhi ya Wapiga kura wamekwama kupiga Kura

Mmoja wa Wagombea Urais, Wakili Boniface Mwabukusi amesema “Karatasi zimeisha tumekubaliana ziongezwe angalau Mia mbili Mia mbili na wote waliofika kupiga Kura watapiga, wameenda kuchapisha, wakifika tutazihakiki.”

Amesema awali uchaguzi huo ulikuwa umalizike Saa Sita Mchana lakini waliokwenda kuchapisha Karatasi wakirejea wataongeza dakika 60 za kuendelea kupiga kura

Awali, #TLS kupitia ukurasa wao wa X (Twitter) uliandika “Zoezi la Mawakili kushiriki kwenye Uchaguzi wa Viongozi wa TLS limekamilika, Asanteni kwa kushiriki.” Dakika 40 baadaye ujumbe huo ukafutwa

Soma https://jamii.app/UchaguziTLS24

#JamiiForums #Democracy
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SHERIA: Akizungumza na Waandishi wa Habari, aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Sweetbert #Nkuba, amesema hatambui Matokeo yaliyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi kwa madai ya kufanyika kwa Uchakachuaji Mkubwa

Uchaguzi huo uliofanyika jana Agosti 2, 2024, Wakili Boniface #Mwabukusi alitangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa #TLS kwa kupata Kura 1,274 huku Wakili Sweetbert Nkuba akifuatia kwa Kura 807

Soma https://jamii.app/MatokeoTLS

#JamiiForums #JFDemokrasia #Governance #CivilRights #SocialJustice
👎21
Kauli hiyo ilizungumzwa Agosti 3, 2024 na Wakili Boniface Mwabukusi ikiwa ni Hotuba yake ya kwanza tangu achaguliwe na kuapishwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Mwabukusi ameshinda Urais wa #TLS siku chache tangu alipoondolewa kwenye orodha ya Wagombea, baadaye aliamua kufungua Kesi ya kupinga uamuzi huo

Julai 26, 2024, Mahakama ilimrejesha kuendelea na mchakato huo ikiwa imesalia Wiki moja kabla ya uchaguzi.

#JamiiForums #GoodMorning #AmkaNaJF #JFQuotes #SocialJustice #NukuuZaJF #Governance #Democracy
👍6
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), #BonifaceMwabukusi akihojiwa katika Kipindi cha Medani za Siasa cha Star TV, alisema Taasisi hiyo inatarajia kupata ushirikiano wa Serikali na hakuna ugomvi binafsi baina ya TLS na #Serikali

Alisema #TLS ni Taasisi yenye Mamlaka huru ambayo inahitaji ushirikiano wa Serikali, #Bunge, #Mahakama na Wananchi.

#AmkaNaJF #NukuuZaJF #JFUwajibikaji #GoodMorning #JFQuotes #Governance #JamiiForums
👍14
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (#TLS), Boniface Mwabukusi amesema Bunge lina wajibu wa kuruhusu suala la utekaji kujadiliwa ndani ya Bunge bila kujali kuna mambo ya kiufundi ambayo yanakwamisha hilo.

Mwabukusi amezungumza hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Redio cha Crown FM

Soma https://jamii.app/MwabukusiCrownFM

#JamiiForums #JFHakiRaia #Governance #JFMatukio
👍2
Akizungumzia taarifa ya Mahakama kuhusu zuio la viongozi wa #CHADEMA kuzungumza na Vyombo vya Habari masuala ya chama, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (#TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amesema, “Linaweza kuwa moja ya zuio la kipekee kabisa, la upande mmoja, kuwahi kutolewa katika historia ya nchi zinazofuata mfumo wa Common Law.”

Mwabukusi ameongeza kuwa “Zuio (injunction) hutolewa kwa lengo la kulinda hali iliyopo (status quo) ili kuzuia madhara zaidi mpaka haki itakaposikilizwa kikamilifu.”

Amehoji, “Je, yawezekana tuko katika janga la Mkwamo wa Kisheria na uminywaji wa Demokrasia na Haki za Kikatiba kupitia Mahakama? Unawezaje kutoa amri ya kusimamisha shughuli zote za chama cha Siasa wakati wa Uchaguzi bila kusimamisha shughuli zinazohusiana na Uchaguzi?''

Soma https://jamii.app/MabukusiKauli

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #CivilRights #Democracy #Uchaguzi2025 #Siasa
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Agosti 26, 2025, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema kumekuwapo na msisitizo mkubwa wa kulinda amani nchini huku haki ikisahaulika.

Amesema ni muhimu kutambua kuwa amani ya kweli haiwezi kuwepo bila haki na kwamba msisitizo wao kama Tanganyika Law Society (#TLS) ni kuuangalia Uchaguzi katika msingi wa haki, amani na utulivu.

Soma Zaidi https://jamii.app/TamkoTLS

#JamiiForums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (#TLS), Boniface Mwabukusi amesema “Sasa hivi Watu wanatekwa, wanapotea. Lazima Taifa tukae pamoja tujadiliane shida iko wapi, na tunapowaomba Viongozi wetu watusikilize wasione kama Watu tunaowaghasi kwenye utulivu, bali watambue tuna nia njema.”

Amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Agosti 26, 2025.

Soma https://jamii.app/TumezoeaKutekwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (#TLS), Boniface Mwabukusi akizungumza leo Agosti 26, 2025, kuhusu kesi zinazomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu amesema, "Tunaishauri Serikali iondoe kesi yake Mahakamani. #DPP anajua cha kufanya ili Lissu aondoke, kwani kama Taifa tukitaka kupona lazima tuache unafiki."

Ameongeza, "Lissu hakuongea gizani, bali aliongea hadharani na wote tunajua kuna kauli kali zaidi zilitoka kuliko za Lissu, lakini zile ni kauli za Kisiasa."

Zaidi https://jamii.app/LissuAtoke

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025