Kijana unafahamu matumizi ya kodi nchini?
Fedha za umma si za viongozi ni za wananchi. Kama raia anayewajibika unayohaki ya kufuatilia miradi ya maendeleo, kuhoji kuhusu bajeti zake na kuhakikisha zinatumika kwa usahihi.
#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa

Mshiriki wa Shindano la Stories of Change Mwaka 2024, alishauri Serikali ibadilishe Mfumo wa Mitihani Vyuo Vikuu kutoka wa Maandishi na kuwa wa Vitendo kuendana na Mabadiliko yanayotokea sasa Duniani
Anasema hii inaweza kusaidia kupunguza changamoto ya Ajira, kwani Watu wengi wanapoajiriwa ndipo wanaanza kupewa Mafunzo ya Kazi fulani, ambayo angepewa akiwa anasoma.
Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/MitihaniVitendoChuo
#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica #SOC2024 #Elimu

MAREKANI: Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) imeidhinisha dawa mpya iitwayo (Yeztugo) Lenacapavir ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya #UKIMWI, ambayo imeelezwa kupunguza hatari ya maambukizi kwa Asilimia 99.9
Dawa hiyo inatolewa kwa sindano mara mbili kwa Mwaka na inadaiwa inaweza kuuzwa kwa hadi Tsh. Milioni 66
Aidha, uidhinishwaji wa dawa hiyo umetokea wakati ambapo Serikali ya Trump imepunguza kwa kiasi kikubwa fedha zinazotolewa kwaajili ya huduma za matibabu na kinga dhidi ya #VVU, ndani na nje ya Marekani, jambo linalozua wasiwasi kuhusu upatikanaji wa dawa hiyo kwa Watu wa kipato cha chini
Soma https://jamii.app/DawaKuzuiaVVU
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFAfya

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Naibu Waziri Mkuu wa Pili na Jenerali Mstaafu Moses Ali amechukua fomu za uteuzi ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Adjumani West kupitia Chama cha National Resistance Movement (NRM), kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2026
Moses Ali amewahi kushikilia nyadhifa mbalimbali za juu Serikalini kwa Miaka mingi, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni (2011–2016), kisha kupewa wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza (2016–2021)
Wanaowania nafasi hizo wanatakiwa kuchukua fomu, kukusanya sahihi kutoka kwa Wanachama wa chama waliopo kwenye majimbo yao, na kurejesha fomu hizo zilizojazwa
Soma https://jamii.app/MkongweKuwaniaUbunge
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance

❤2
Ukivitambua na kuvishinda Vizuizi vya ndani, unafungua mlango wa Mafanikio ya kweli.
Komesha Uvivu kwa kuchukua hatua, tuliza Hasira kwa Busara. Ndani yako kuna nguvu ya kubadilika.
#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha

❤1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Naibu Spika na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Zungu akiwaaga Wabunge na Watumishi wa Bunge Juni 20, 2025, amewahimiza kuwa na Ushupavu na kuwajali Wananchi hasa wale wa Kipato cha chini na Yatima kwani wanahitaji kusaidiwa
Soma https://jamii.app/ZunguAdabuHeshima
#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Bungeni

DAR: Taarifa ya Kanisa Katoliki imesema Maaskofu wameagiza maboresho ya Maadhimisho yanayohusu Daraja Takatifu, Nadhiri za Kitawa, Ndoa, Jubilei na Maziko ya Kikristo kutokana na kuwepo kwa tabia ya kuingiza matangazo mengi na hotuba nyingi kwenye Maadhimisho mbalimbali ya Kiliturujia
Taarifa imesema kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Kikao cha 109, kilichofanyika Kurasini tarehe 16-19 Juni 2025, Maaskofu wameagiza mwishoni mwa Adhimisho (baada ya sala ya komuniyo), itatolewa mara moja Baraka ya mwisho
Hakutakuwa na hotuba za kupongezana, isipokuwa tu Mwadhimishaji (Paroko/Padri/Askofu/Rais wa TEC) atatambua kwa ufupi uwepo wa Wageni wa Kidini, Kiserikali, Kijamii na Waalikwa wote bila kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia. Mwadhimishi Mkuu anawajibika kuwaalika wageni kutoa zawadi zao na bila ya wao kutoa Salamu za pongezi.
Soma https://jamii.app/TECBanWanasiasa
#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji

❤4👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalumu, Thea Ntara, amesisitiza Serikali kuwalipa Watumishi wa Vyuo Vikuu wakiwemo Wahadhiri madeni yao, akieleza wengi wao wanafanya kazi katika Mazingira magumu na hawajitokezi kugoma au kuonesha utovu wa Nidhamu
Ikumbukwe Januari 2025, Mdai wa JamiiForums.com aliandika hoja akisema "Chuo Kikuu Huria Tanzania lipeni Waajiriwa wenu pesa zao za kujikimu, mtawaua njaa na kuwafedhehesha Mtaani"
Mdau huyo alitoa Mfano kuwa Watumishi wanaohamishwa Vituo vya Kazi hukaa hadi zaidi ya Mwaka bila kupewa Fedha zao za kujikimu
Soma https://jamii.app/MbungeMadeniWahadhiri
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Bungeni #JFMdau2025

👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Uchambuzi wa Bajeti kutoka Chama cha ACT - Wazalendo umesema kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Serikali imepanga kutumia Trilioni 56.49, ambapo Mgawanyo wa matumizi ni trilioni 38.99 kwa ajili ya Mishahara, Posho, Magari na Misafara ya Viongozi, Mabango ya Kumsifu Rais, Chai na Deni la Serikali (69.04%)
Wakati Miradi ya Barabara, Mikopo ya Wanafunzi, ujenzi wa vituo vya Afya, Shule, Dawa, Maji, Pembejeo za Kilimo, imetengewa Trilioni 17.49 (30.96%), ikimaanisha katika kila Tsh. 1,000, Tsh. 700 inaenda kwenye Mishahara, Chai, Deni na Posho huku Tsh. 300 tu ndio inaenda kuhudumia Wananchi
ACT imesema Mgawanyo wa Bajeti uliopelekwa kwenye matumizi ya Maendeleo ya Wananchi ni kiwango kidogo zaidi na itategemea zaidi Fedha za nje au Mikopo.
Soma zaidi Uchambuzi huu https://jamii.app/UchambuziBajetiACTWazalendo
#JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025

❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema licha ya Vyama ya Siasa kuwa na kaulimbiu zake lakini itakapofika Siku ya kupiga kura, Akili za kuambiwa changanya na zako
Ameyasema hayo leo Juni 21, 2025 katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Sheria JNICC
Soma https://jamii.app/KikweteAkiliKura
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #UchaguziMkuu2025 #KuelekeaUchaguzi2025

DAR: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema moja ya changamoto inayosumbua Sekta ya Habari ni suala la Upotoshaji wa Taarifa unaofanyika kwa makusudi ama kwa kutofahamu
Amesema hali hiyo imetokana na maendeleo ya Teknolojia ambayo yanatengeneza fursa kwa usambaaji wa Taarifa Potoshi, ambapo ameeleza hoja za kukabiliana na changamoto hizo ni sehemu ya Mada zitakazojadiliwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14 - 17, 2025)
Aidha, ameongeza kuwa Mkutano huo utajadili mijadala ya kitalaamu kuhusu changamoto zinazoathiri Tasnia ya Habari na namna Mabaraza ya Habari kote Duniani yanavyokabiliana na changamoto hizo
Soma https://jamii.app/MabarazaYaHabari
#JamiiForums #JamiiAfrica #FactChecking #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck

DAR: Akizungumzia umuhimu wa kuwa na Watu wanaohusika Uhakiki wa Taarifa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema “Uwepo wa Wadau kama #JamiiAfrica unahitajika kutumika kusaidia kutoa elimu ya Uhakiki wa Taarifa kama ambavyo wamekuwa wakifanya (kupitia #JamiiCheck).”
Ameongeza “Tunahitaji Wadau aina hiyo waongezeke kusaidia kukabiliana na Taarifa Potoshi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, kwani kupotosha Sera, Ilani au Taarifa za Watu wakati huu tunapoelekea katika kampeni kunaweza kuwa na madhara makubwa.”
Amesema hayo wakati akizungumzia ujio wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14-17, 2025) unaoandaliwa na MCT kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), Umoja wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (EAPC) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Soma https://jamii.app/MCTFactChecking