JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2024/25 zinaendelea kushika kasi, #Yanga imeendelea kubaki katika nafasi ya kwanza kwa kufikisha Pointi 76 baada ya kuiunga Tanzania Prisons Magoli 5-0, #Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 75 baada ya kuichapa KenGold Magoli 5-0 pia

Yanga imeshinda ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya wakati Simba nayo ilikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora

Timu hizo mbili zimesaliwa na michezo miwili kukamilisha Ligi, ukiwemo unaozikutanisha zenyewe mnamo Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, ambapo ni mchezo unaotarajiwa na wengi kuwa utaamua bingwa wa Ligi

Soma https://jamii.app/MbioZaUbingwa

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu kuelekea kwa Mbunge, Luhaga Mpina kwamba yalimfurahisha na kumpa furaha

Jana Juni 17, 2025, Rais Samia akiwa ziarani Mkoani Simiyu alisema Mbunge wa Kisesa (Mpina) 'amerukaruka' kwenye kutaja Mambo yaliyofanyika Jimboni kwake, huku akieleza amelidharau Jimbo lake kwa kusema "Kisesa iko kama Mwanamke aliyesuka Nywele"

Soma https://jamii.app/MbungeNgonyani

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025
2
Kijana, Kujua haki zako ni ngao ya kukulinda. Ukiwa na uelewa wa haki zako, unapata ujasiri wa kuzitetea si tu kwa ajili yako, bali pia kwa ajili ya wengine katika jamii.

Ni wajibu wetu sote kujielimisha kuhusu haki na majukumu yetu kama raia

Tuelewe sheria, sera na mifumo ya kisheria inayotuathiri na tushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi ili kuhakikisha jamii yenye haki, usawa na uwajibikaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia amesema “Halmashauri zote zijitahidi katika makusanyo ya Mapato, kwa upande wa TRA wanajitahidi sana lakini kwa Halmashauri mnakula nyingi mnaleta kidogo. Niwaombe sana mjizatiti katika makusanyo ili maendeleo yaendelee kama tulivyoyapeleka katika Miaka hii mitano”

Amesema hayo leo Juni 18, 2025 wakati akizungumza na Wananchi wa Bariadi

Soma https://jamii.app/HalmshauriMakusanyoKidogo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya matukio ya Watu kupotea au kutekwa, kwa kusema taarifa zote zinazopokelewa huwa zinafanyiwa uchunguzi wa kukusanya ushahidi kutoka vyanzo mbalimbali, ili kupata ukweli wa taarifa ya nini kilichotokea ili kupata ushahidi wa kuthibitisha

Polisi imeeleza Kifungu cha 117 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Marejeo ya Mwaka 2022 na Kifungu cha 161 cha Sheria ya Ndoa Sura ya 29 marejeo ya Mwaka 2019, dhana ya Mtu kuchukuliwa kuwa amekufa inapaswa kuthibitishwa na Mahakama baada ya Miaka mitano kupita, kulingana na vielelezo na ushahidi utakaowasilishwa

Soma https://jamii.app/PolisiKuhusuUtekaji

#JamiiForums #HumanRights #Accountability #Governance
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limesema Sheikh Zuberi Said Nkokoo (53) Mwalimu wa dini na Kiongozi wa Taasisi ya Islam Foundation ya Singida ambaye iliripotiwa ametekwa, imebainika hakutekwa na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya taratibu za Kisheria kukamilika

Taarifa ya Polisi imeeleza Sheikh Nkokoo alidai kutekwa na Watu aliowataja kuwa ni Askari wa Jeshi la Polisi, Juni 2, 2025 akiwa na Tsh. Milioni 42, lakini Uchunguzi umebaini alitengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa na Watu mbalimbali (majina yao yamehifadhiwa) jumla ya Tsh. Milioni 521.5

Soma https://jamii.app/PolisiKuhusuUtekaji

#JamiiForums #HumanRights #Accountability #Governance
2🤣1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limeeleza Uchunguzi wa tukio la Novemba 11, 2024 lililomhusu Deogratius Tarimo, Mkazi wa Kibaha - Pwani ambaye alionekana kwenye picha mjongeo akipambana na Watu waliotaka kumteka ila wakashindwa, umeonesha Watuhumiwa sio Askari Polisi

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, amesema uchunguzi ulibaini waliohusika sio Askari Polisi na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa Mapenzi ambapo Watuhumiwa 6 walikamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Soma https://jamii.app/PolisiKuhusuUtekaji

#JamiiForums #HumanRights #Accountability #Governance
1
Ndoto nyingi hufa kwa sababu wengi hukata tamaa kabla hawajaanza.

Wanaogopa kushindwa, wanasahau kuwa hata mafanikio yanaanza na makosa.

Usiache ndoto zako zife kwa woga au kushindwa mara moja. Jifunze, simama tena, songa mbele.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Machi 04, 2019 Hayati John Pombe Magufuli alizungumzia matukio ya Utekaji Nchini na kusema "Watanzania wanajua kuchambua mambo, na lilipotokea tukio la kutekwa kwa Mo Dewji zilikuja habari nyingi kwamba waliohusika na Utekaji ni Wazungu wa aina fulani lakini suala hilo lilipomalizika, liliacha maswali mengi zaidi."

Aliongeza kwa kusema wahusika walijaribu kulichoma Moto Gari lakini baadae aliyetekwa akaonekana anakunywa Chai na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (wakati huo), Lazaro Mambosasa.

Soma https://jamii.app/MagufuliMatukioUtekaji

#JamiiForums #JFKumbukizi #JamiiAfrica #HumanRights #Transparency #Siasa
2
Umeajiri Vijana katika Biashara yako? Ni Waaminifu?

Unamshauri Mdau atumie mbinu gani ili kushughulikia changamoto za Uaminifu kutoka kwa Vijana wake wa Dukani?

Mjadala zaidi? huu https://jamii.app/KijanaDukaniWizi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Biashara #Uchumi #JFChitChats #JFStories
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Abdallah Possi, ametoa utetezi katika Baraza la Haki za Binadamu ofisi ya Geneva, Uswisi, kuhusu madai ya kutesa na kudhalilisha Wanaharakati Juni 18, 2025

Amesema "Pamoja na kuwa shutuma zao dhidi ya Serikali zina mashaka makubwa, tunayachukulia kwa uzito mkubwa madai ya kuteswa, Unyanyasaji wa Kingono na vitendo vya ukiukaji wa Maadili. Ndio maana Serikali kwa sasa inachunguza, na ikithibitika, wahusika watachukuliwa hatua"

Aidha, ameeleza kuwa "Serikali imejizatiti kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa Amani, Uwazi, na kwa kuzingatia viwango vya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa vya Haki za Binadamu, Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wa Kujieleza, Haki ya kupata Taarifa, na Ushiriki wa Vyombo vya Habari. Tunaamini katika Usawa mbele ya sheria kwa Watu wote, wakiwemo watetezi wa Haki za Binadamu"

Soma https://jamii.app/TanzaniaKujiteteaUN

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia #HumanRights #KuelekeaUchaguzi2025
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema muda wa Miaka mitano hauwezi kumaliza matatizo yote ndani ya Nchi na wale wanaodhani hilo linawezekana ni Watu wa ajabu

Amesema hayo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM katika kikao cha ndani, jana Juni 18, 2025, Geita Mjini

Soma https://jamii.app/WasiraGeita

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Juni 18, 2025, Mwanachama wa Chama cha #ACTWazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewasisitiza Wanachama wa Chama hicho kuwa washiriki katika Uchaguzi wa 2025 na muhimu wanatakiwa kulinda Kura wanazopiga

Soma https://jamii.app/PondaJuni18

#JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
#KENYA: Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imemuita Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIG), #EliudLagat kutoa maelezo kuhusiana na kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang, aliyefariki akiwa Mikononi mwa Polisi akidaiwa kupigwa kwa amri ya DIG na OCS

Lagat, ambaye alitangaza kujiondoa kwa muda Ofisini ili kuruhusu uchunguzi kufanyika, ndiye Mlalamikaji aliyedai kuchafuliwa kupitia chapisho la #Ojwang kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter), na anatarajiwa kufika katika Ofisi za IPOA, leo Alhamisi Juni 19, 2025

Mwenyekiti wa IPOA, Issack Hassan amethibitisha kuwa Mamlaka hiyo “imeona msingi" wa kumuita Afisa huyo wa ngazi ya juu.

Soma https://jamii.app/IPOACallsDIGLagat

#JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Accountability #HumanRights
2