JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Peter Kibatala, mmoja wa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika shtaka linalomkabili la 'kuchapisha taarifa za uwongo Mtandaoni', amesema walikuwa wamejipanga kumtetea mteja wao kwa kumuuliza maswali shahidi ambaye alianza kutoa Ushahidi wake jana Juni 16, 2025

Kibatala amesema shahidi huyo aliyejitambulisha kwa jina la PF. 22863 Inspekta John, wanamfahamu vizuri na siku atakaporejea Mahakamani wataonesha kitu tofauti

Shahidi huyo akitoa ushahidi Mahakamani, amesema alikutana na picha mjongeo (video) kupitia Akaunti ya YouTube ya Jambo TV, ambayo ilichapishwa Aprili 3, 2025 na kudai alibaini maudhui yenye jinai kupitia matamshi yaliyotolewa na Lissu

Soma https://jamii.app/KibatalaNaShahidi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights
1
Wimbo wa 'My Heart Will Go On' ni kati ya kazi zilizomuongezea umaarufu #CelineDion, ambayo alirekodi akiwa na umri wa Miaka 29, ukiwa maalum kwaajili ya ‘soundtrack’ ya Filamu ya #Titanic iliyotoka Mwaka 1997

Celine aliwahi kuhojiwa na kusema alipofuatwa kwaajili ya kurekodi wimbo huo hakuona kama inamfaa. Alisema“Sikuona kama inanifaa, nilichoka sana siku hiyo. Nilifikiria nimeshafanya ‘soundtrack’ kadhaa, sikutaka kuonekana kazi yangu ni hiyo tu, mume wangu (René Angélil) akanishawishi niimbe demo (wimbo wa awali kabla ya wimbo wenyewe).”

Alieleza kuwa baada ya demo aliondoka studio, hawakurudi tena kwaajili ya kuimba wimbo wenyewe, na hiyo ndiyo ikatengenezwa na kutumika kuwa wimbo rasmi wa Filamu

Soma https://jamii.app/MyHeartWillGoOn

#JFEntertainment #JamiiForums #JamiiAfrica
1
Israel na Iran wamekuwa wakishambuliana kwa Makombora kwa Siku ya tano mfululizo, baada ya #Israel kufanya mashambulizi ya anga Juni 13, 2025 dhidi ya maeneo ya #Iran, ikiwemo Shirika la Utangazaji la Taifa huko Tehran na vituo vya kurutubisha Urani

Iran ilijibu kwa kurusha Makombora na Ndege zisizo na Rubani (Drones) kuelekea Miji ya Israel, na kusababisha vifo vya raia zaidi ya 220 Nchini Iran na takriban 24 Nchini Israel

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth amesisitiza kuwa Marekani iko katika msimamo wa kujilinda, ikiwa tayari kusaidia kufanikisha makubaliano ya amani na kulinda majeshi yake katika eneo hilo lakini si kwa ajili ya kushambulia.

Soma https://jamii.app/IsraelIranMissileTrade

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy #HumanRights #IsraelIranConflict #Diplomacy
KENYA: Inaelezwa Askari James Mukhwana ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Mwanaharakati Albert Ojwang’, amesema (OCS), Samson Talaam alitoa amri ya “kumuadhibu” Ojwang, amri ambayo Mukhwana anadai ilitoka kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat

Maelezo hayo, ambayo Citizen TV imeyapata yanadai Mukhwana amesimulia jinsi alivyoitwa Ofisini kwa OCS usiku huo akiwa kazini, na kuelezwa “Kuna agizo kutoka kwa DIG Lagat. Unamfahamu? Kuna Maafisa kutoka Makao Makuu ya DCI wanamleta mtuhumiwa hapa saa mbili Usiku. Waambie wale wafungwa wamuonyeshe adabu kidogo.”

Ojwang alifungiwa ndani Saa tatu na dakika 20 Usiku, muda mfupi baada ya hapo mateso yakaanza kwenye selo ya mwisho karibu na Vyoo. Mukhwana anasema wafungwa wanne, Collins Ireri, Gil Ammiton, Brian Mwaniki na Erick Ndambuki waliagizwa kumshambulia.

Soma zaidi Ushahidi huu https://jamii.app/KonsteboMukhwanaTalks

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #HumanRights #HakiZaBinadamu #Transparency
2🤔1
DAR: Jeshi la Polisi linadaiwa kuzuia kufanyika kwa Mkutano wa #CHADEMA na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025 katika Ukumbi wa Seashells Millennium Hotel, kwa maelezo kwamba Chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Kisiasa

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia amesema wakati wakijiandaa kwa Mkutano huo, walifika Watu waliojitambulisha kuwa ni Maafisa wa Polisi na kuzuia usifanyike

Alipoulizwa kuhusu zuio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema “Wanalalamika nini? Basi tunafuatilia wasichokijua na ambacho wanakilalamikia.”

Soma https://jamii.app/CDMBanPolisiDar

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #UchaguziMkuu2025
1
DODOMA: Kampuni za madini za Geita Gold Mine (GGM), Shanta na Buckreef Gold zimeingia mikataba na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya utekelezaji wa Sheria ya Madini, inayozitaka kampuni binafsi za uchimbaji madini kuiuzia BoT dhahabu inayozalishwa na kampuni hizo kwa kiwango kisichopungua Asilimia 20

Mikataba hiyo imesainiwa na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba mbele ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Juni 16, 2025

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema mikataba hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini, kinachowataka wachimbaji wa Madini kutenga 20% ya uzalishaji wao kwaajili ya kuiuza katika masoko ya ndani ikiwemo kuiuzia BoT, ambayo imepewa haki ya kwanza Kisheria ya ununuzi wa Dhahabu.

Ameongeza ‘‘Hadi leo BoT imenunua Tani 5 za dhahabu sawa na Dola za Marekani Milioni 554 na kupitiliza malengo yake ya kununua Dhahabu ya Dola za Marekani Milioni 350."

Soma https://jamii.app/BOTKuuziwaDhahabu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uchumi
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa onyo kwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina pamoja na Wanasiasa wengine wa Mkoa wa Simiyu, kuacha kutumia zao la Pamba kama mtaji wa Kisiasa

Bashe amesema Mpina aliwahi kumdanganya Hayati Rais Magufuli kuhusu Bei ya Zao la Pamba Duniani na kusababisha Wakulima kupata hasara, kwa kuuza Pamba kwa Tsh. 500

Soma https://jamii.app/BasheMpinaKuuaKitalu

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Siasa #Transparency
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amemwambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Jimbo lake bado linamdai na kwamba maeneo mengine yanayodai hayamdai, fedha zao zihamishiwe Kisesa

Ameyasema hayo leo Juni 17, 2025 wakati wa mkutano wa hadhara Wilayani Meatu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Samia Mkoani humo.

Soma https://jamii.app/SamiKisesaTunakudai

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais Samia Suluhu akiwa ziarani Mkoani Simiyu, amesema Mbunge wa Kisesa (Luhaga Mpina) 'amerukaruka' kwenye kutaja Mambo yaliyofanyika Jimboni kwake, huku akieleza amelidharau Jimbo lake kwa kusema "Kisesa iko kama Mwanamke aliyesuka Nywele"

Soma https://jamii.app/SamiaMpinaKisesa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #UchaguziMkuu2025 #KuelekeaUchaguzi2025
DAR: Kesi ya Marejeo iliyopo Mahakama Kuu Dar es Salaam iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri ambayo ilipangwa kutajwa leo Juni 17, 2025 imeahirishwa hadi Juni 27, 2025.

Shauri hilo lilipangwa kusikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jaji Mkwizu, lakini Mahakama imeagiza kuwa litakapotajwa tena Juni 27, Lissu anatakiwa kufikishwa Mahakamani

Katika shauri hilo Lissu anaoimba Mahakama kufanya marejeo ya mwenendo wa Kesi ya tuhuma za 'kutoa taarifa za uongo Mtandaoni', ambayo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Muhini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Soma https://jamii.app/KesiMarejeoLissu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia Suluhu amesema Vijana wanne wamepoteza maisha kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuelekea katika mkutano uliofanyika leo, Juni 17, 2025, ambapo kabla ya mkutano huo Rais alitembelea majeruhi wa ajali hiyo, waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya Meatu

Awali, Jeshi la Polisi Mkoa lilitoa taarifa kuwa Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Mwamishari, Kata ya Mwamishari, Meatu ikihusisha gari aina ya Scania lililobeba Wananchi waliokuwa wanatoka kwenye Zoezi la Chanjo ya Mifugo na Utambuzi, jana Juni 16, 2025 Usiku

Soma https://jamii.app/AjaliSimiyuJuni16

#JFMatukio #JamiiForums #Misinformation #Disinformation
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Emilian J. Duzu (21) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Gerald P. Said (22), Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo hicho, tukio ambalo limetokea Alfajiri ya Juni 14, 2025

Polisi imeeleza tukio lilitokea katika maeneo ya Klabu ya Muziki ya Mbeya Pazuri, ikidaiwa Emilian alimjeruhi Gerald kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni, akakimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya lakini alifariki Saa 7:00 Mchana

Soma https://jamii.app/AmuuaMwanafunziClub

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
2
Vijana tusibaki kuwa watazamaji wa kinachoendelea kwenye jamii yetu, tujifunze haki na wajibu wetu, tujue sheria na sera zinazotugusa na tushiriki kikamilifu kwenye maamuzi yanayojenga mustakabali wetu

Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka, kwa kufanya maamuzi sahihi

Tuchukue hatua kwa kufuatilia taarifa kwa makini, kuhoji kwa hoja, na kutoa maoni yanayojenga. Tuwajibike sasa kwa mabadiliko na maendeleo tunayoyataka katika Jamii zetu

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
KENYA: Polisi wa kutuliza ghasia wamempiga Risasi Kijana mmoja aliyekuwa kwenye #Maandamano ya kudai haki kwenye kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang, ambaye Uchunguzi na Mahojiano ya Polisi vilimebaini alifariki kwa kupigwa na Wafungwa kwa amri ya Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIG)

Video inayosambaa Mtandaoni inawaonesha Askari wawili wa kutuliza ghasia wakimfuata Kijana muuza Barakoa, kumpiga na kitako cha Bunduki, kisha kuongea nae kidogo kabla ya Polisi mmoja wao kumnyooshea bunduki na kumfyatulia Risasi, kisha kuondoka

Imeelezwa, Polisi aliyehusika katika tukio hilo tayari anashikiliwa, baada ya Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Taifa (NPS) kuagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/KifoRaiaProtestOjwang

#Democracy #HumanRights #JamiiAfrica #JamiiForums #PoliceBrutarity
1
DIPLOMASIA: Siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani, #DonaldTrump kuwaonya raia wa #Iran waliopo Mji wa Tehran kuhama, kwa kile alichoeleza kutakuwa na mashambulizi yanayoweza kufanyika katika eneo hilo, amedai Marekani ina udhibiti wa anga la Iran

Kupitia Mtandao wa Truth Social, Trump ameandika “Marekani sasa inadhibiti kikamilifu anga la Iran. Iran ilikuwa na vifaa vizuri vya kufuatilia anga na ulinzi wa kutosha na vingi lakini haviwezi kulinganishwa na ‘vitu’ vilivyotengenezwa na Wamarekani. Hakuna anayefanya vizuri zaidi ya Marekani.“

Ameongeza “Tunajua kwa uhakika kabisa alipojificha huyo anayeitwa ‘Kiongozi Mkuu’ (akimaanisha Ayatollah Ali Khamenei). Ni mlengwa rahisi, lakini yuko salama pale alipo hatutamwondoa (kumuua!), angalau si kwa sasa. Hatutakubali makombora yaelekezwe kwa raia au kwa Wanajeshi wa Marekani. Subira yetu inaanza kuisha. Asanteni kwa kulipa hili uzito!”

Soma https://jamii.app/MarekaniKumilikiAngaIran

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
2