JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo ya karibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mashauri yanayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu, yanaendelea Mahakamani hapo

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa #CHADEMA wameshawasili Mahakamani kufuatilia kinachoendelea

Soma https://jamii.app/KesiLissuKurindimaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu ambaye anakabiliwa na Kesi mbili kwenye Mahakama ya Kisutu amesema kwa siku 68 ambazo amekuwa Gerezani, amenyimwa haki ya kuzungumza kwa faragha na Mawakili wake ambao wamekuwa wakienda kuonana naye

Ameongeza kuwa licha ya hivyo yeye pamoja na Mawakili wake hawapati nafasi ya kubadilishana nyaraka kwaajili ya kushughulikia kesi zinazomkabili

Lissu akiwa kizimbani amesema amekuwa akizungumza na Mawakili kwenye simu akiwa eneo ambalo halimpi nafasi ya kufanya mazungumzo ya faragha, ambapo amesema kuwa, kupitia mawasiliano ya simu au eneo chumba anachotumia kuwasiliana na Mawakili wake kuna uwezekano wa kupokwa kwa Haki ya Faragha

Amesema mazingira ya aina hiyo ni kinyume na Sheria

Soma https://jamii.app/LissuNaMawakili

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Taifa, #TunduLissu ameomba Mahakamani ajitetee mwenyewe katika mashauri yanayoendelea dhidi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Juni 16, 2025 wakati kesi yake ikianza kusikilizwa

Lissu ambaye alikuwa anawakilishwa na Mawakili zaidi ya 30, anakabiliwa na kesi ya uhaini pamoja na kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo Mtandaoni

Soma https://jamii.app/LissuKujibuHoja

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga ameieleza Mahakama kuwa jalada la uchunguzi la kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu tayari limepelekwa kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kwaajili ya kupitiwa kabla ya kuamriwa kupelekwa Mahakama Kuu

Upande wa Utetezi uliomba Mahakama kuitaka Jamhuri kukamilisha uchunguzi katika shauri hilo, ambapo Mahakama ilitoa maelekezo kwa upande wa Jamhuri kuharakisha uchunguzi

Hata hivyo, shauri hilo limekuwa likitajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bila kusikilizwa, kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kulisikiza

Baada ya Jamhuri kueleza hatua hiyo na mshtakiwa kukubaliana nayo, Mahakama imeahirisha shauri hilo mpaka Julai 1, 2025

Soma https://jamii.app/KesiLissuKurindimaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights
DAR: Mdau anadai tangu kuanza kwa Mwaka 2025, hajaona gari la taka katika Mtaa anaoishi (Mbezi Beach), ambapo Wananchi hulazimika kuwakodi Vijana wenye mikokoteni ili kuzoa taka na kuondoka nazo, bila kujua zinaenda kutupwa wapi

Mdau anadai Mamlaka inayosimamia mazingira (NEMC) imekuwa kimya katika suala hilo, akihoji au inasubiri mlipuko wa Magonjwa utokee ndio watoe tamko na kuchukua hatua, halafu ukiisha 'wapige kimya' tena?

Soma https://jamii.app/UzoajiTaka

#Accountability #JamiiForums
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka tarehe 16 Juni, ikiwa ni kumbukumbu ya Maandamano ya Wanafunzi huko Soweto, Afrika Kusini Mwaka 1976, ambapo walidai Haki yao ya kupata Elimu bora

Ulimwenguni kote, Watoto wanaendelea kukabiliwa na vitisho vinavyoingiliana, kutoka Umasikini na njaa hadi upatikanaji mdogo wa Elimu bora na Huduma za Afya. Kwa mujibu wa Shirika la #UNICEF (2023), zaidi ya Watoto Bilioni moja Duniani kote wanakabiliwa na angalau aina moja ya kunyimwa mahitaji muhimu

Hili ni suala la dharura hasa Barani Afrika, ambalo lina idadi ya Watoto inayokua kwa kasi zaidi Duniani, kukiwa na zaidi ya Watoto Milioni 540, karibu 50% ya idadi ya Watu Barani kote. Ifikapo Mwaka 2055, Afrika itakuwa na idadi kubwa zaidi ya Watoto Duniani

Soma https://jamii.app/DAC2025

#AfricanChildDay #InvestInChildren #DAC2025 #DayOfTheAfricanChild #JamiiForums #JamiiAfrica
1
KENYA: Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (DIG), Eliud Kipkoech Lagat, ametangaza kujiondoa kwa muda kazini wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang’, ambaye alikamatwa kufuatia malalamiko ya kashfa yanayodaiwa kuwasilishwa na Afisa huyo

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Lagat amesema “Leo nimeamua kujiondoa kwa muda kutoka katika Wadhifa wa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya hadi uchunguzi utakapokamilika. Majukumu ya Ofisi yataendelea kutekelezwa na Naibu wangu hadi uchunguzi utakapokamilika.”

Ojwang’ alikamatwa muda mfupi baada ya kuchapisha madai ya Ufisadi yaliyomhusisha Lagat, hasa kuhusu upangaji wa kimkakati wa Maafisa ndani ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na vitengo vya trafiki, nafasi zinazodaiwa kuwa na uhusiano na udhibiti wa mapato na taarifa za Kijasusi

Soma https://jamii.app/DIGResignsKE

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akiongea Mahakamani leo Juni 16, 2025, Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu amesema kuwa licha ya kuwa hajahukumiwa, anakaa upande wa Watu waliohukumiwa kifo katika Gereza la Ukonga

Zaidi https://jamii.app/LissuKuhusuGerezani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia Suluhu ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya mapato kwa njia rafiki, lakini sio kubembelezana anayekataa asilipe. Amesema kila anayepaswa kulipa kodi, alipe

Amesema hayo baada ya kufungua Jengo la Ofisi ya TRA Mkoani humo, leo Juni 16, 2025

Soma https://jamii.app/MikopoYaNje

#JamiiForums #Governance #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia akifungua Jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Simiyu, leo Juni 16, 2025 amesema "Ulaya na Marekani sasa hivi hawafanyi vizuri Kiuchumi kama tunavyofanya Sisi huku, hata ndani ya kanda yetu hii ya Afrika Mashariki, Tanzania tunafanya vizuri”

Soma https://jamii.app/SamiaUlayaMarekani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
1👎1
#MALEZI: Vipi kwa upande wako, Mzazi/Mlezi wako aliwahi kukuhusia jambo gani ambalo bado unalizingatia mpaka sasa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MausiaMzazi

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFStories #JFChitChats #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia Suluhu Hassan akifungua Jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Mapato TRA, leo Juni 16, 2025, amezungumzia umuhimu wa Wananchi kulipa Kodi ili Nchi ianze kutegemea mikopo na misaada kutoka nje

Soma https://jamii.app/MikopoYaNje

#JamiiForums #Governance #Accountability
1
MARA: Kesi ya madai iliyokuwa inawakabili Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ambaye ni Mdaiwa namba 1, Karoli Jacob (Mdaiwa namba 2) na Mara TV (Mdaiwa namba 3), imetolewa hukumu leo Juni, 16, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma

Wadaiwa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya madai shauri namba 23, ya Mwaka 2023 iliyofunguliwa na Eliakim Chacha Maswi, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma ( PPRA) , ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria

Eliakim Maswi alifungua kesi kutaka wadaiwa kumlipa Tsh. Bilioni 12 kama fidia ya madhara ya jumla pamoja na Tsh. Bilioni 1 kama fidia ya adhabu, kwa madai ya kumkashfu na kutoa tuhuma za uongo dhidi yake kuhusu Wizi wa Fedha, ambapo Mahakama imeamua Waitara na wenzake wamlipe Maswi Tsh. Bilioni 6, pia waite Vyombo vya habari na kumsafisha dhidi ya tuhuma walizotoa dhidi yake na walipia alipie gharama za kesi

Soma https://jamii.app/WaitaraBili6Udhalilishaji

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
2
UGANDA: Rais, #YoweriMuseveni, amesaini Sheria mpya inayoruhusu Mahakama za Kijeshi kuwahukumu raia, hatua ambayo Viongozi wa upinzani wamesema inakiuka uamuzi wa Mahakama ya Juu

Wanaharakati wa Haki za Binadamu kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Serikali imekuwa ikitumia Mahakama za Kijeshi kuwatesa Wapinzani wa Kisiasa wa Museveni, ambaye amekuwa Madarakani kwa takribani Miaka 40. Wasimamizi wake wamekanusha madai hayo, wakisema kuwa ni raia wanaotumia silaha kwa vurugu za kisiasa tu ndio wanaofikishwa katika mahakama hizo.

Katika uamuzi wake mapema Mwaka huu, Mahakama ya Juu ya #Uganda ilipiga marufuku utaratibu huo, ikisema kuwa ni kinyume cha #Katiba. Serikali ya Museveni iliwasilisha Muswada mpya wa Sheria uliolenga kurejesha utaratibu huo, na Bunge liliupitisha Mwezi uliopita

Soma https://jamii.app/MuseveniMilitaryCourt

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Democracy
Je, Wajua Asilimia 34.4 ya Watu wote Tanzania Bara ni Vijana?

Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 (SWM 2022), Tanzania Bara ina Watu 59,851,347, kati ya hao, Vijana ni 20,612,566 sawa na 34.4%

Ni ukweli usiopingika kwamba Vijana ni kundi kubwa na ndilo lenye nguvu za kufanya kazi, ndio watu wenye ubunifu, wenye uthubutu na ujasiri na ndio waliobeba maono ya Taifa, hivyo Mapinduzi makubwa kwenye uchumi, jamii na teknolojia yatafikiwa endapo kila Kijana atashiriki na kujitoa kikamilifu kuleta mawazo mapya, ubunifu na mikakati mipya ya kuchangia maendeleo kwenye jamii yake

Soma https://jamii.app/UwajibikajiWaVijana

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFVijana #RestlessDevelopment #UshirikiWaVijana
Hakuna mafanikio ya haraka. Unahitaji kuwaza, kupanga na kuendelea kujaribu bila kuchoka. Hii ndo njia ya kuona ndoto yako ikigeuka kuwa kweli

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
👍1