JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Leo Mei 30, 2025 ni Siku ya pili ya Mkutano wa Afrika wa Utawala wa Mtandao, ambapo JamiiAfrica itashiriki kwenye Mjadala utakaoangazia namna ya Kuitumia Akili Mnemba (AI) kwa Maendeleo na Ustawi wa Afrika

Mjadala huu unatarajiwa kuwa na mwelekeo wa utekelezaji, ukizingatia changamoto na fursa za kipekee kwa Afrika katika Mazingira ya Kimataifa ya AI

Wadau wataangazia namna ambavyo Nchi za Afrika zinaweza kuunda Mifumo ya AI kwa kuzingatia muktadha wa ndani, ili kuhakikisha hazibaki kuwa watumiaji wa AI pekee, bali zinakuwa wabunifu.

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
😈1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob amesema Vijana wa Chama hicho wanajivunia Utumishi wa aliyekuwa Mwenyekiti Taifa, Freeman #Mbowe, na kumtaka kutokaa pembeni kwani bado wanamhitaji

Amesema hayo akihutubia Wilayani Hai, Kilimanjaro Mei 29, 2025.

Soma https://jamii.app/MboweAsikaePembeni

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
1
JamiiAfrica inafurahia kuwa sehemu ya Mkutano wa 14 wa Utawala wa Intaneti Afrika (AfIGF), unaofanyika kuanzia Mei 29 - 31, 2025 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam!

Tembelea Banda letu la Maonesho ujumuike nasi, ujifunze zaidi kuhusu kazi tunazofanya, na uchangie Mawazo ya kibunifu juu ya mustakabali wa Kidigitali unaowawezesha Vijana Barani Afrika.

Kama Wewe ni Mdau wa Teknolojia, una hamu ya kujifunza au unatafuta njia za kushiriki na kuleta mabadiliko tungependa sana kukutana nawe!

Zaidi https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #UsalamaWaMtandao #HakiZaKidijitali #UchaguziTZ #UpotoshajiTaarifa #UtawalaWaMtandao #UaminifuNaUwajibikaji #Tanzania2025
KENYA: Ripoti ya Utafiti wa “Trends and Insights for Africa (TIFA)” umeonesha ongezeko la ugumu wa Maisha, hali ambayo Wakenya wengi wanapitia tangu Rais William Ruto aingie madarakani Mwaka 2023

Ripoti hiyo imeonesha 75% ya waliohojiwa wamesema hali yao ya Kiuchumi ni mbaya zaidi sasa kuliko ilivyokuwa Miaka mitatu iliyopita , kabla ya Uchaguzi wa mwisho, wakati 10% pekee wamesema hali imeboreshwa, huku ikionesha maeneo yaliyoathirika zaidi ni Ukanda wa Mashariki na Nyanza (82%), yakifuatiwa na Nairobi na Mlima Kenya (79%)

Aidha, sababu kuu zilizotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo ni Ufisadi, Uongozi duni, Ukabila, Migawanyiko ya Kikabila pamoja na gharama kubwa ya Maisha

Soma https://jamii.app/KenyaMaishaMagumu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability
Mkuu wa Sekretarieti ya IGF, Chengetai Masango amesema Mikutano kama hii inatusaidia kukuza ubunifu, kulinda Haki za Binadamu Mtandaoni na kutumia Teknolojia kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2030

Ameeleza kuwa, Nguvu ya mawazo ipo katika ushirikishwaji wa Wadau mbalimbali, ambapo Wawakilishi kutoka Serikalini, Vijana, Wabunge, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu ya Juu na Sekta ya Mtandao wamekusanyika kwenye Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao Afrika, kuonesha juhudi muhimu zinazohitajika kujenga mustakabali endelevu unaoakisi Matarajio ya Afrika yote

Ameongeza "Tunaweza kuhakikisha Mtandao wa Intaneti unabaki kuwa Rasilimali ya Kimataifa inayosimamiwa kwa manufaa ya Umma na kwamba Afrika inachangia katika kuunda mustakabali wetu wa Kidigitali wa pamoja"

https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ametembelea banda la JamiiAfrica lililopo ukumbi wa JNICC, katika Mkutano wa 14 wa Utawala wa Intaneti Afrika (AfIGF), unaofanyika kuanzia Mei 29 - 31, 2025

Waziri amepata nafasi ya kuelezwa mambo mengi ikiwemo kuhusu Taasisi ya JamiiAfrica pamoja na Majukwaa mbalimbali yanayopatikana ndani ya JamiiForums.com

Mdau pia una nafasi ya kutembelea Banda letu ujifunze zaidi kuhusu kazi za JamiiAfrica na kuchangia Mawazo ya kibunifu, juu ya mustakabali wa Kidigitali unaowawezesha Vijana Barani Afrika

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
2
Moses Kunkuyu, Waziri Habari na Digitali wa Malawi amesema Kama Bara la Afrika, hebu tuanze mazungumzo kwa ajili ya Afrika nzima, mazungumzo ya kuhakikisha kwamba Bara letu lote linaunganishwa Kimtandao.

Ameeleza kuwa "Kwa sababu, tukikumbuka yaliyopita: wakati janga la COVID-19 lilipotokea, Watoto wa Nchi zilizoendelea waliendelea na masomo yao kupitia mtandao. Lakini Watoto wa Afrika? Walibaki nyumbani, bila shule, bila intaneti. Tusiruhusu hilo litokee tena"

Ameongeza kuwa "Ikiwa tukio jingine kama hilo litakuja, Kila Mtoto wa Kiafrika lazima aendelee na masomo yake. Kila raia wa Afrika apate Huduma za Afya kwa njia ya mtandao. Ni hapo ndipo tutaweza kusema kwa dhati kuwa: Ajenda ya mabadiliko ya Kidijitali Barani Afrika ni ajenda ya kila Nchi ya Afrika.

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi katika kuwezesha huduma za Mtandao wa simu nchini ambapo ameeleza kwamba kwa sasa Wananchi wanaotumia Mtandao wa 5G ni Asilimia 23.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (IGF) Mei 30, 2025 amesema "Tumeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji, jambo lililowezesha huduma za mtandao wa simu kufikia 92% (3G), 91% (4G), 23% (5G) ya Wananchi."

Ameongeza "Lengo letu ni kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Kidijitali na kuboresha maisha ya Wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.”

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
Akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao Afrika, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amesema pochi ya Kidijitali, ni kama ile Pochi ya kawaida tu ambapo Mtu huhifadhi pesa zake, kadi za Benki, na Vitambulisho. Ni programu salama iliyounganishwa na inayomruhusu Mtu kuhifadhi, kutuma, kupokea, na kusimamia Fedha zake katika Mfumo wa Kidijitali.

Ameeleza hii inawasaidia sana Wajasiriamali kwa kurahisisha njia ya kufanya Biashara, na pia kurahisisha upatikanaji wa Mitaji.

Amesema "Kama unavyojua, ukienda Benki za kawaida kuomba mkopo, unalazimika kujaza fomu, kuandaa ripoti – na mara nyingine ripoti hizo zinaweza kuwa za kughushi. Lakini sasa, kupitia pochi ya Kidijitali iliyounganishwa, ni rahisi kupata Huduma za Kifedha kwa njia ya Mtandao, na kwa haraka.

Fuatilia https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu ameagiza mchakato wa kuchuja Wagombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (#CCM) ufanyike kwa haki ili kuzuia chama hicho kisiwe ‘Gwajiminized’

Amesema hayo Mei 30, 2025 wakati wa Mkutano Maalum wa CCM, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete

Soma https://jamii.app/RaisSamiaGwajima

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Lamin Jabbi, Waziri wa Mawasiliano na Uchumi wa Kidigitali Nchini Gambia, amesema ni muhimu sana kutambua Teknolojia zinazobadilisha Mifumo (disruptive technologies) ambazo tayari zipo na zinakuja Afrika

Ameeleza kuwa "ni muhimu kuwa na msimamo wa pamoja kama Nchi za Afrika katika kukabiliana na changamoto hizi. Hatupaswi kukabiliana na changamoto hizo kama nchi moja-moja, bali kwa mtazamo wa pamoja wa Afrika."

Amesisitiza kuwa "Tunahitaji kuelewa kwamba kuendeleza Miundombinu ya Kidijitali si jambo la mara moja au la mwisho, ni mchakato unaoendelea, kwani Teknolojia hubadilika mara kwa mara. Ni muhimu sana kutambua mabadiliko hayo na tuyakabili kwa mtazamo wa Kiafrika. Hili haliwezi kufanywa na Nchi moja au mbili – lazima tufanye kama Bara moja lenye msimamo mmoja.

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Prof. Kitila Mkumbo, akiwasilisha Ilani hiyo ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 amesema sehemu kubwa ya maudhui yametokana na maoni ya Wanachama wa CCM, Wananchi na wadau mbalimbali

Amesema Chama kitaelekeza Serikali kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora ikiwemo kuuhisha na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya

Soma https://jamii.app/KatibaMpyaCCM

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025
1
Mdau wa masuala ya Usalama Kidigitali, Ihueze Nwobilor amesema “Usalama wa Kidijitali ni muhimu sana na tunapaswa kuhakikisha kuwa hata wale wasiojua kusoma na kuandika wanaweza kutumia kwa urahisi.”

Ameongeza kuwa ni muhimu kutengeneza Mifumo na Vifaa ambavyo hata Watu wa Kijijini wasiojua Kusoma na Kuandika ila wana Vifaa vya Kieletroniki wanaweza kutumia humu wakizingatia Usalama wa Kimtandao wa taarifa zao

Ameeleza “Nchini kwangu tunatoa Elimu kuhusu Usalama Mtandaoni lakini ukimwambia Mtu wa Kijijini kuhusu “Two factor authentication” hawezi kukuelewa”

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
3
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia za Digitali Afrika Kusini, Mondli Gungubele akielezea Mafanikio ya Nchi hiyo katika Mifumo ya Kidigitali amesema, Mabadiliko ya Kidijitali ya Afrika Kusini yanaendelea kwa kasi na yana Mafanikio

Ameeleza Mafanikio ya Kidijitali ya Afrika Kusini yanajumuisha: Upatikanaji wa Kitaifa wa Usafiri wa Kidijitali, unaosaidia Mamlaka kufuatilia taarifa za Trafiki (foleni ya barabarani) kwa wakati halisi, pia kuna Mfumo wa malipo wa kisasa, unaowezesha Miamala kufanyika papo kwa papo (instant to instant transactions)

Ameongeza kuwa Mashirika kama Interpol na wadau wengine yanatumia Huduma za Kidijitali kufuatilia na kudhibiti taarifa za Kijasusi za kuvuka mipaka

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Leo ni Siku ya Mwisho ya Mkutano wa Jukwaa la Utawala wa Intaneti Afrika (AfIGF) 2025, unaofanyika katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam

Kwa siku 3, wadau mbalimbali kutoka barani Afrika wamekutana kujadili mustakabali wa usimamizi wa intaneti kuanzia haki za kidijitali, usalama mtandaoni, sera, hadi ushirikishwaji wa vijana na makundi maalum.

JamiiAfrica inajivunia kuwa sehemu ya mijadala yenye tija, kubadilishana uzoefu, na kujifunza namna bora ya kuhakikisha intaneti salama, jumuishi na endelevu kwa wote

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
👍1