JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza anakunywa Soda Nne aina ya Cola kwa siku, Mtaalam wa #Afya ameeleza unywaji wa soda na vitu vingine vya Sukari kwa wingi inasababisha hatari ya kupata magonjwa kama Kisukari, anashauri ni vyema kuepuka vitu hivyo kwa wingi ikiwemo juisi, energy drinks n.k.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mlonganzila, Dkt. Anthony Gyunda anaeleza “Matumizi mengi ya Sukari yanasababisha uraibu, hiyo pia ipo katika vinywaji vya chupa na makopo sababu vinatunzwa kwa kuweka ‘preservatives’ ambazo zingine zinaleta uraibu kama Dawa za Kulevya tu.”

Kuhusu kuachana na uraibu huo, Dkt. Gyunda anasema “Kuondokana na Uraibu wa Sukari ni sawa tu na Uraibu mwingine kama wa Dawa za Kulevya, ushauri nasaha, maamuzi ya muathirika mwenyewe na matumizi ya dawa za kukakata uraibu.”

Soma https://jamii.app/UnywajiSoda

#JamiiForums #PublicHealth #JFMdau2025 #JamiiAfrica
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Aprili 10, 2017, Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitaka Bunge lijadili matukio ya utekaji wa Watu ambapo alidai yeye pia ametumiwa ujumbe wa vitisho, hoja yake pia iliungwa mkono na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi "Sugu"

Akijibu hoja hiyo, Dkt. Tulia alisema“Masuala yaliyoulizwa na Bashe na Mbilinyi yapo chini ya utaratibu wa Sheria, Bunge hili litashughulika na mambo yenye maslahi kwa umma ambayo Sheria haina uwezo wa kuyatolea majibu, hivyo sitalihesabu jambo hilo kuwa ni jambo la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 (4) bali utaratibu wa Kisheria utafanya kazi."

Soma https://jamii.app/BasheUtekaji2017

#JamiiForums #JFKumbukizi #JamiiAfrica #HumanRights #Transparency #Siasa
👍1
Mdau unapendekeza kitu gani kiwepo kwenye Nyumba za kupanga ambacho ni cha muhimu kwaajili ya Wapangaji?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NyumbaKupangaVyamuhimu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories
UGANDA: Rais #YoweriMuseveni na Mkewe Janet Museveni ambaye ni Waziri wa Elimu na Michezo, wameomba msamaha hadharani, wakikiri kuwepo kwa mapungufu katika Utawala wao, #Rushwa na kuwatelekeza Wananchi, hasa wa eneo la Buganda, wakati joto la kisiasa likizidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Januari 2026

Katika tukio lililoandaliwa na binti yao, Mchungaji Patience Rwabwogo, Wawili hao walisimama bega kwa bega na kusoma sala ya pamoja ya toba waliyoiandaa, walikiri uzembe na kasoro zilizopo Serikalini katika Miaka 39 ya Uongozi wao

Hata hivyo Kijana wao, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye amekuwa gumzo hasa kwa kutoa vitisho kwa wapinzani wa Serikali ya Baba yake, hakuhudhuria tukio hilo

Soma https://jamii.app/MuseveniRadhi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance #UgandaPolitics #UgandaElections
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akidai kumekuwa na 'trend' ya Viongozi kuonesha dharau kwa Wananchi hasa kipindi hiki tunapokaribia Uchaguzi, tabia anayodai ni ishara ya Viongozi hao kujiamini kupita kiasi kwamba watarudi Madarakani bila kujali ridhaa ya Wananchi, na kwamba nafasi zao hazitegemei kura

Mdau amekumbusha kuwa Mahusiano ya Viongozi na Wananchi wao yanapaswa kuakisi Uwajibikaji, Uadilifu na Heshima ya pande zote mbili. Kujenga Mazingira ya Kuheshimiana ni Msingi wa Demokrasia Imara na Maendeleo ya Taifa

Soma https://jamii.app/ViongoziKuraWananchi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #Democracy #Kuelekea2025
DODOMA: Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu imetengua uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua Uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa

Mahakama imesema Mkutano Mkuu wa NCCR Mageuzi wa Septemba 24, 2022 haukumpatia Haki ya msingi (Natural Justice) Mbatia ya kusikilizwa, hivyo ulikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Chama cha NCCR-Mageuzi na Sheria za Vyama vya Siasa

Aidha, Mahakama imetengua maamuzi yote yaliyofanywa na Mkutano huo ya kumuondolea Mbatia Uanachama na Uenyekiti huku ikikitaka Chama hicho kulipa gharama zote za kesi

Zaidi https://jamii.app/MbatiaAshinda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Democracy #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imebaini Mabati yenye thamani ya Tsh. Milioni 220 yaliyonunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Katavi na Sekondari Rungwa kuwa yapo chini ya kiwango

Kaimu Mkuu wa #TAKUKURU Mkoa, Daud Lyamongo akitoa taarifa ya Ufuatiliaji wa Utelelezaji wa Miradi ya Maendelo ya Robo Mwaka, leo Mei 28, 2025 amesema Taasisi hiyo ilikagua Miradi miwili ya Elimu yenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.3 na kubaini kasoro

Lyamongo ameongeza kuwa walibaini Mzabuni alilipwa Tsh. 220,023,980 na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kabla ya Mabati kufika eneo la ujenzi kinyume na utaratibu

Soma https://jamii.app/TAKUKURUKatavi

#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica
DAR: Goli pekee la Steven Mukwala katika dakika ya 42 limeipa Simba ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa KMC Complex

Ushindi huo unaifanya #Simba kufikisha alama 72 ikiwa nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya #Yanga yenye pointi 73, timu zote zikiwa zimecheza Michezo 27

Singida imebaki katika nafasi ya nne ikiwa na alama 53 katika Michezo 28

Soma https://jamii.app/SimbaSingidaMei28

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema maoni yaliyotolewa na baadhi ya Wabunge wakati wa mjadala wa Bajeti za Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Maendeleo ya Jamii hayawakilishi msimamo rasmi wa Bunge hilo

Kauli hiyo inagusa baadhi ya kauli zilizotolewa kuhusu Wanaharakati kutoka Kenya na Uganda ambao waliingia Nchini kufuatilia kesi dhidi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ambapo baadhi ya Wabunge waliooneshwa kukerwa ujio wa Wanaharakati hao

Soma https://jamii.app/MaelezoYaSpika

#JamiiForums #Siasa #Diplomacy #Kuelekea2025 #Democracy #JamiiAfrica
👍2
KENYA: Rais #WilliamRuto ameomba radhi kwa Nchi jirani za Uganda na Tanzania, endapo kuna migogoro au sintofahamu ambazo hazijatatuliwa na zinaweza kudhoofisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Nchi hizo

Akizungumza katika Hafla ya Kitaifa ya Maombi, Rais Ruto amesisitiza kuwa #Kenya ipo katika safari ya 'kufufuka' na kujijenga upya na kuhimiza Wakenya kubadili mtazamo na kuwa na roho ya upatanisho na mshikamano, akieleza Serikali yake inalenga kuunganisha Taifa na kulijenga kwa pamoja

Amesema "Nawaomba tuache lawama na badala yake tujenge Madaraja ya maridhiano na umoja yatakayoiinua Nchi yetu kuwa bora zaidi,”

Soma https://jamii.app/RutoAombaRadhi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #UtawalaBora #Diplomacy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Jeshi la Polisi limesema linafanya uchunguzi kuhusu kifo cha Sheikh Jabir Haidar Jabir Mkazi wa Fuoni ambaye Mwili wake uliokotwa eneo la Kizimbani Bumbwisudi Mkoa wa Mjini Magharibi ukiwa hauna jeraha wala hakukuwa na dalili za vurugu

Mwili huo uliokotwa Usiku wa kuamkia Mei 28, 2025 ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Mchomvu, amesema umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya uchunguzi zaidi

Amesema Marehemu alikuwa anaishi na Kijana aliyekuwa akimsaidia na Mei 27, 2025 Saa 12 Jioni Sheikh alitembelewa na Vijana kadhaa ambapo aliondoka nao Saa 2:30 Usiku na baadaye akapatikana akiwa amefariki

Soma https://jamii.app/SheikhJabirHaidar

#JamiiForums #HumanRights #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MAREKANI: Msanii wa Kenya, Bien-Aime Baraza "Bien" akihojiwa katika Kipindi cha Breakfast Club Power amezungumzia mambo yanayoendelea katika Nchi yake akitaja uwepo wa matukio ya Utekaji, Upinzani kuminywa na nafasi ya Vijana katika kuiwajibisha Serikali

Amesema kumekuwa na Uhuru wa Kujieleza lakini hakuna Uhuru baada ya Kujieleza na kwamba ana Imani kubwa kwa Vijana wa sasa kuliko Viongozi lakini pamoja na hayo bado anajivunia kuishi Kenya kwa kuwa ni Nchi nzuri na ina mambo mengi mazuri

Soma https://jamii.app/BienInterview

#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica #Democracy #Entertainment #FreedomOfSpeech
1