JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka zinazohusika na Kituo cha Stendi cha Mbagala Rangi Tatu kutenga fedha kwa ajili ya kufanya uboreshaji hata kama ni ya muda mfupi kwa kuwa hali ilivyo sasa inasababisha kesho kwa Watumiaji

Soma https://jamii.app/StendiYaMbagalaRangiTatu

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Afrika inaendelea kupiga hatua katika teknolojia na matumizi ya mtandao, lakini ili tufike mbali zaidi tunahitaji sera bora, usimamizi wa haki na sauti za wadau wote hasa Vijana, Wanawake, Sekta Binafsi na asasi za kiraia

Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF2025) litafanyika kuanzia Mei 29 hadi 31 na linalenga kuwaleta pamoja wataalamu wa teknolojia, watunga sera, watoa huduma na watumiaji wa mtandao kwa majadiliano ya kina kuhusu mustakabali wa Kidijitali wa Afrika

Ni jukwaa la kujifunza kutoka kwa wengine, kujenga mitandao ya ushirikiano na kuchangia mawazo yatakayosaidia kujenga Afrika jumuishi zaidi mtandaoni

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica
Mwanachama wa #CCM aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ametuma ujumbe kwa Rais Samia Suluhu kupitia Ukurasa wake wa Instagram akisema “Uzalendo ni kuweka siri ila uzalendo zaidi ni kutofanya hayo yanayovujishwa ili kutakiwa kubakishwa sirini.”

Ameandika “Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima na taadhima na upendo mkuu kwako, kuvujisha siri ni utovu mkubwa wa maadili, na ni kosa kubwa ila kufanya yanayovujishwa ni ukosefu mkubwa zaidi wa maadili na kosa kubwa zaidi.”

Ameongeza “Kama wanaokosea ni Viongozi na ni Watu, ni Wanadamu wenye mapungufu, vivyo hivyo wanaovujisha nao ni Watumishi na ni Watu, ni binadamu wenye mapungufu na wakati mwingine ukute anafanya ili mkubwa aone apate kuchukua hatua, akijiweka yeye mwenyewe matatizoni.”

Soma https://jamii.app/BasillaMwanukuzi

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍21
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu wa Hamasa Wilaya ya Kinondoni, Hemedi Hassan Salim amesema "Tunaomba Chama cha Mapinduzi kufanya maamuzi juu ya Gwajima. Hatufurahishwi na kumuona bado anakuwa M-NEC na mbunge wetu baada ya kumtukanisha Rais Samia na wananchi wake. Fanyeni maamuzi na kutuletea watu wanaofahamu miiko ya Chama chetu"

Ameyasema hayo leo Mei 27, 2025 mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/GwajimaAtolewe

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
Mchezo wa #Handball ni mojawapo ya Mchezo mkubwa Nchini Denmark ambao ulivumbuliwa Nchini humo Mwaka 1898 na ni moja ya Michezo inayopendwa sana

Mpira wa 'handball' ni mkubwa, una ukubwa sawa na Tikiti Maji dogo, tofauti na Mpira mdogo unaojulikana Nchi nyingine. Mchezo huu ni wa kasi na ushindani mkubwa, ambapo Mabao 30 au zaidi yanaweza kufungwa katika Mechi ya Saa moja.

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #JFSports
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza Bungeni, leo Mei 27, 2025, Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa ameelekeza Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Camilus Wambura pamoja na Mamlaka nyingine kuwachukulia hatua Watu kwa “kuwashughulikia” wanaotumia Mtandao kumdhalilisha Rais

Soma https://jamii.app/TamkoLaBashungwa

#JamiiForums #Governance #DigitalRights
DEMOKRASIA: Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ametangaza kusitisha kutoa ruzuku kwa CHADEMA hadi pale watakapotekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili kutokana na CHADEMA kutokuwa na Viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za Umma

Taarifa ya Msajili imeeleza endapo CHADEMA wataendelea kukaidi kutekeleza maamuzi na maelekezo waliyopatiwa, basi Mamlaka husika zitatakiwa kuchukua hatua za kisheria na kijinai. Taarifa pia imekumbusha kwa mujibu wa Sheria, Msajili anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa CHADEMA endapo itaendelea kuwatambua wanaojiita Viongozi wa Chama hicho

Imeelezwa kuwa kufuatia taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Dkt. Nshala Rugemeleza amesema “Tutapambana naye kisheria dhidi ya hatua zake alizozichukua, maana amekiuka sheria ni ajenda ya siri ya kutaka CHADEMA ife,"

Zaidi https://jamii.app/NoRuzukuCHADEMA

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #Demokrasia #Utawala #Uwajibikaji
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akizungumza na wakazi wa Mwabuma, Jimboni Kisesa, Mkoani Simiyu amesema hatuwezi kuzitatua changamoto za taifa hili kwa kuongea lele mama, kwa kutokuambizana ukweli hata pale mambo yanapoharibika

Zaidi https://jamii.app/LuhagaUwajibikaji

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Democracy #Governance #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Msanii wa Bongo Fleva, Tumaini Godfrey maarufu kama Dudubaya akitoa maoni yake kuhusu utaratibu wa kuchaguwa Wabunge amesema unaonesha kuwa na upungufu kutokana na baadhi yao kutotambua thamani ya Ubunge wao

Soma https://jamii.app/DudubayaWabunge

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #KuelekeaUchaguzi2025
👍1
PWANI: Mdau anadai Watu waliovaa Kiraia wamefika katika Kituo cha Daladala cha Maili Moja na kukamata Pikipiki za Biashara (Bodaboda) majira ya Saa Tatu hadi Nne Usiku wa Mei 27, 2025 kisha kuzipakia katika ‘Karandinga’ na kuondoka nazo bila kutoa maelezo yoyote kwa Madereva wa vyombo hivyo

Anadai tukio hilo lilisababisha baadhi ya Bodaboda kukimbia ovyo hali ambayo haikuwa salama kwao na Wapitanjia, na waliochukuliwa vyombo vyao walipohoji wamejibiwa wafike Kituo cha Polisi Mji Mdogo watapata maelezo

Mdau anatoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura kuwasaidia Bodaboda hao akidai vitendo kama hivyo vimekuwa vikiwarudisha nyuma kimaendeleo na kuwaumiza Kisaikolojia na Kiuchumi

Soma https://jamii.app/PolisiMailiMoja

#JFMatukio #JFMdau2025 #CivilRights #JamiiForums #JamiiAfrica
👍2
AFYA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza anakunywa Soda Nne aina ya Cola kwa siku, Mtaalam wa #Afya ameeleza unywaji wa soda na vitu vingine vya Sukari kwa wingi inasababisha hatari ya kupata magonjwa kama Kisukari, anashauri ni vyema kuepuka vitu hivyo kwa wingi ikiwemo juisi, energy drinks n.k.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mlonganzila, Dkt. Anthony Gyunda anaeleza “Matumizi mengi ya Sukari yanasababisha uraibu, hiyo pia ipo katika vinywaji vya chupa na makopo sababu vinatunzwa kwa kuweka ‘preservatives’ ambazo zingine zinaleta uraibu kama Dawa za Kulevya tu.”

Kuhusu kuachana na uraibu huo, Dkt. Gyunda anasema “Kuondokana na Uraibu wa Sukari ni sawa tu na Uraibu mwingine kama wa Dawa za Kulevya, ushauri nasaha, maamuzi ya muathirika mwenyewe na matumizi ya dawa za kukakata uraibu.”

Soma https://jamii.app/UnywajiSoda

#JamiiForums #PublicHealth #JFMdau2025 #JamiiAfrica
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Aprili 10, 2017, Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitaka Bunge lijadili matukio ya utekaji wa Watu ambapo alidai yeye pia ametumiwa ujumbe wa vitisho, hoja yake pia iliungwa mkono na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi "Sugu"

Akijibu hoja hiyo, Dkt. Tulia alisema“Masuala yaliyoulizwa na Bashe na Mbilinyi yapo chini ya utaratibu wa Sheria, Bunge hili litashughulika na mambo yenye maslahi kwa umma ambayo Sheria haina uwezo wa kuyatolea majibu, hivyo sitalihesabu jambo hilo kuwa ni jambo la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 (4) bali utaratibu wa Kisheria utafanya kazi."

Soma https://jamii.app/BasheUtekaji2017

#JamiiForums #JFKumbukizi #JamiiAfrica #HumanRights #Transparency #Siasa
👍1