JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai sehemu ya miundombinu ya Vyoo vya Wanaume katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi - Kimara Mwisho imefungwa haitumiki kwa muda, hivyo anahoji Mamlaka zinazokusanya mapato kituoni hapo kila siku hazioni uhitaji wa kuboresha miundombinu hiyo?

Soma https://jamii.app/VyooKimara

#ServiceDelivery #JFHuduma #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PEMBA: Wananchi wa Kijiji cha Andikoni, Shehia Chumbageni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba walazimika kuwabeba wagonjwa wakiwa kwenye vitanda katika mabega kutokana na ubovu wa barabara ili kupata Huduma za Afya

Wakizungumza na Halisi Media Online, baadhi ya Wananchi wamesema wanapitia wakati mgumu kutokana na ubovu wa Barabara na kwamba mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid, amesema Serikali ina mpango wa kujenga barabara hiyo

Soma https://jamii.app/BarabaraAndikoniPemba

#JamiiForums #Accountability #Governance
👍2
Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ametoa wito kwa Wananchi wa eneo la Mlima Kenya kuwasusia Wasanii kutoka eneo hilo waliokutana na Naibu Rais Kithure Kindiki, akiwatuhumu kwa kuisaliti jamii ya eneo hilo kwa kuzingatia maslahi yao binafsi.

Hata hivyo, Naibu Rais Kithure Kindiki ametetea Mkutano huo, akisema kuwa ulikuwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kushughulikia changamoto za Wasanii, hasa kuhusu unyonyaji unaofanywa na 'magenge ya kati' katika Sekta ya Ubunifu

#Kindiki pia aliwashutumu baadhi ya Wanasiasa kwa kutumia vibaya Wasanii katika Kampeni na kuwashawishi kutunga nyimbo za uchochezi kwa malipo duni

Soma https://jamii.app/GachaguaNaWasanii

#JamiiForums #JamiiAfrica #KenyanPolitics #Democracy #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
IRINGA: Wananchi wa Kiwalamo, Wilaya ya Kilolo wakiwa wamembeba mgonjwa kwenda Kidabaga kwa miguu ili akatibiwe, changamoto ya barabara imekuwa kero kwa muda mrefu

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya, Rebecca Sanga Nsemwa amesema “Nimefika eneo la tukio, nimeelekeza TARURA washughulikie Barabara japokuwa sio sehemu kubwa iliyoharibika, huku kwetu mvua ikinyesha kunakuwa na changamoto ya aina hiyo kutokana na asili ya udongo ulivyo.”

Ameongeza “Yule aliyebebwa ni mjamzito, Daktari alishawajulisha ndugu zake kuwa wakiona dalili ambazo si nzuri apelekwe hospitali mapema lakini wao walichelewa, pamoja na hivyo 'Ambulance' ilifika na kumchukua. Nitoe wito kwa Wananchi wafikisha Wagonjwa hospitali mapema badala ya kusubiri hali iwe mbaya.”

Soma https://jamii.app/MiundombinuKilolo

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Balozi wa Tanzania Nchini Cuba, Humphrey Polepole, katika kipindi chake cha #ShuleYaUongozi Septemba 11, 2021, alizungumzia Watu wanaosema hawapendi Siasa akisema Siasa ndio inaamua maisha. Aliongeza kuwa Raia yoyote anayewajibika lazima aulize maswali kuhusu mambo yanayofanywa na Serikali

Zaidi https://jamii.app/KuhojiPolepole

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #Democracy #Uwajibikaji #Accountability #Transparency
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema Awamu ya Tano hakukuwa na Mwanasiasa aliyefungua mdomo wala hakukuwa na mikutano, kauli hiyo ameitoa kutokana na kile alichoeleza kuna Mwanasiasa rafiki yake aliyezungumza na Wanahabari na kuhoji maamuzi ya Rais

Musukuma amesema hayo Bungeni, leo Mei 26, 2025 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Soma https://jamii.app/MusukumaOnGwajima

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amesema Jeshi la Uhamiaji na Jeshi la Polisi lingewapeleka kulima raia wa kigeni waliokamatwa na kurejeshwa nchini kwao hivi karibuni na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linatakiwa kuendelea kufanya kazi yake kwa mwendo ule ule

Amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo Mei 26, 2025

Soma https://jamii.app/MusukumaMei26

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#Bungeni: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema "Adui wa nchi yoyote, ikiwemo yetu, katika karne hii ya 21 si lazima aje na vifaru ndipo ahesabike kuwa ni mvamizi. Anaweza kuja kwa njia ya magenge ya wanaharakati wenye ajenda ya kuvuruga amani kama tulivyoshuhudia hivi karibuni."

Amezungumza leo Jumatatu, Mei 26, 2025, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2025/26

Soma https://jamii.app/BashungwaAmani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #Accountability #Uwajibikaji
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu (DICTI) kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Leo Magomba amesema katika Bara la Afrika Watu wanaotumia intaneti ya uhakika ni Asilimia 38 hivyo ameeleza kuwa zinahitajika juhudi za pamoja kuchochea ongezeko

Aidha, ameeleza katika Mkutano wa 14 wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF) utakaofanyika Mei 29 hadi 31, 2025, Wadau wanatarajia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo yanayoweza kuchochea ongezeko hilo

Amebainisha mambo kadhaa yatayojadiliwa, namna ya kuongeza upatikanaji wa intaneti kwa wote, kuondoa tofauti ya matumizi kati ya Mijini na Vijijini na kuimarisha usalama wa Mtandao pamoja na kujadili suala la Teknolojia ya Akili Mnemba (AI)

Soma https://jamii.app/TakwimuZaIntaneti

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica #DigitalRights
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanasiasa Jerry Muro amezungumzia ujumbe uliotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima kwa kusema “Sijui unatafuta nini baba yangu, kuna kitu fulani, naona una kitu, kuna kitu unakitafuta, lakini hakuna kitu kimefanyika Rais Samia hajawahi kutolea maelekezo.”

Muro amesema hayo akijibu hotuba ya Askofu Gwajima aliyoitoa Mei 24, 2025 alipozungumzia masuala mbalimbali ikiwemo matukio ya utekaji

Soma https://jamii.app/MurroOnGwajima

#Siasa #Democracy #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Wanahabari, leo Mei 26, 2025, Mwanasiasa Jerry Muro kuhusu Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema "Kama kweli umediriki kujivua nafasi yako ya Ubunge na Uaskofu na nafasi yako ya Ujumbe wa Kamati ya CCM kwa lengo tu la kushindana na Rais Samia, Biblia inasema yatupasa tutii mamlaka maana mamlaka inatoka kwa Mungu, hata kama Rais wetu ni wa ovyo kiasi gani, lazima tumtii."

Soma https://jamii.app/MuroAmtajaGwajima

#Siasa #Democracy #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Afrika inapiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya kidigitali, lakini bado tunahitaji Sera bora na ushiriki wa kila mmoja wetu

Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF2025) kuanzia Mei 29-31 linawaleta pamoja Wadau wa Teknolojia, Serikali, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na Vijana ili kujadili masuala muhimu ya Utawala wa Mtandao (Internet Governance) Barani Afrika

Kwa wadau wote wa Teknolojia na Mtandao, Jukwaa hili litakuwa la Mazungumzo, Ushirikiano na kubadilishana Mawazo

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica
Rais wa Marekani Donald Trump amesema hafurahishiwi kabisa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya anga Ukraine yanayotajwa kuwa makubwa kabisa tangu vita hiyo ianze mwaka 2022, yaliyosababisha vifo 12 na majeruhi kadhaa

Urusi ilituma makombora na drones takriban 360 usiku wa Jumapili, Mei 25, 2025 makombora ambayo wachambuzi wamesema ni idadi kubwa zaidi ya makombora kuwahi kutumwa Ukraine katika usiku mmoja tangu vita hiyo ianze mwaka 2022

Ikumbukwe, Wiki iliyopita, Trump na Putin walizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa 2 kujadili pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano. Trump alisema mazungumzo hayo “yalienda vizuri sana” na kwamba Urusi na Ukraine ziko tayari kuanza mazungumzo ya moja kwa moja ya kuelekea kusitisha vita.

Soma https://jamii.app/MakomboraPutin

#JamiiForums #JamiiAfrica #RussiaVsUkraine
1👍1
Kada wa Chama cha Demokrasia na Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia alikuwa mtia nia wa Ubunge katika Jimbo la Magu - Mwanza (Uchaguzi Mkuu Mwaka 2020), Juma Kaswahili inadaiwa hajulikani alipo, leo ikiwa ni siku ya tano

Kada huyo ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA, Januari 2025 alikuwa katika Timu ya Kampeni ya Tundu Lissu, inadaiwa Watu wake wa karibu hawajui alipo na simu zake zote hazipatikani, mara ya mwisho alionekana hadharani Mei 12 katika Mkutano wa chama Igoma, Mwanza

Upande wa Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia amesema “Bado tunaendelea kufuatilia ila tumejulishwa aliondoka Kanda ya Ziwa mara baada ya Mkutano, akapanda Basi la Shabiby na alizungumza na Mbyella kuwa tayari amefika Dar ila hajisikii vizuri na hiyo ilikuwa Mei 19, 2025.”

Soma https://jamii.app/JumaKaswahili

#JamiiForums #HumanRights #Democracy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum (Mjini Magharibi-CCM), Tauhida Gallos akizungumza Bungeni amesema "Tuwaambie Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuna kenge wa ndani halafu kuna kenge wa nje, shughulikeni na kenge wa ndani mmalize na hao wa nje."

Amesema hayo leo Mei 26, 2025 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Soma https://jamii.app/WananchiKenge

#Siasa #JamiiForums #AfricanPolitics #Democracy
👍2