JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Rais Samia amesema Utumishi wa Umma ndio injini ya Uendeshaji wa Nchi, hivyo Viongozi wateule wa Tume ya Maadili ya Utumishi wafanye kazi ya kuwakumbusha Watu Maadili

Amesema "Mtu unamteua ila akifika pale yeye anawaza, nikifika watanijua, nataka baada ya Miaka Miwili niwe 'Somebody', badala ya kutumikia Nchi anajitumikia mwenyewe"

Soma https://jamii.app/SamiaMaadiliUtumishi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com amehoji iwapo ni sahihi kuripoti Polisi au ustawi wa jamii pale unapoona jirani anafanya unyanyasaji au ukatili kwa Watoto au msaidizi wake wa kazi, swali hili lililoibua mjadala kuhusu mipaka ya faragha na wajibu wa kijamii.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa kulinda Watoto ni jukumu la kila mmoja wetu katika jamii na si sahihi kufumbia macho ukatili na unyanyasaji wa aina yoyote. Ukiona, chukua hatua kwa kukemea au kutoa taarifa kwa mamlaka husika

Mdau, unadhani ni sawa kuripoti pale jirani anapofanya unyanyasaji au ni kuingilia maisha ya watu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuripotiMtotoAnayeteswa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle
Jukwaa la Utawala wa Mtandao Barani Afrika (AfIGF) litafanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 29 hadi 31, 2025, ambapo Wadau wa Mtandao kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika na Duniani watakutana

AfIGF itaunganisha Wadau kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta binafsi, Wataalamu wa Kiufundi na Vyuo Vikuu

Litakuwa jukwaa la Mazungumzo, Ushirikiano na kubadilishana Mawazo juu ya masuala muhimu ya Utawala wa Mtandao (Internet Governance) Barani Afrika

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica
πŸ‘2
AFRIKA KUSINI: Mchezo wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika umemalizika kwa sare ya Goli 1-1 kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, kati ya #MamelodiSundowns dhidi ya Pyramids

Goli la wenyeji limepatikana dakika ya 54 kupitia kwa Lucas Costa, huku wageni #Pyramids wakasawazisha dakika ya 90+4 mfungaji akiwa ni Walid El Karti

Hivyo, Bingwa anatarajiwa kujulikana Juni 1, 2025 ambapo mchezo wa pili utapigwa kwenye Uwanja wa 30 June Jijini Cairo Nchini Misri

Soma https://jamii.app/MamelodiPyramids

#JFSports #JamiiForums #JFCAFCL
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akiongea na Waandishi wa Habari leo, Mei 24, 2025 amesema kuwa kumekuwa na mlolongo wa matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea nchini

Askofu Gwajima ameongeza kuwa kutokana na matukio hayo ameamua kuitisha Mkutano na Waandishi wa Habari ili kuongelea kuhusu suala hilo na kisha kutoa Ushauri wake

Soma https://jamii.app/KauliAskofuGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
❀1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema hawezi kuamini kwamba Vyombo vya Usalama havina taarifa kuhusu Utekaji wa Watu ila inawezekana wakifuatilia wanakuta kikundi kilichomchukua Mtu kimetengenezwa na Mwanasiasa fulani kwa faida zake

Ameyasema hayo leo, Mei 24, 2025 akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uwepo wa Matukio mbalimbali ya Utekaji Watu

Soma https://jamii.app/KauliAskofuGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Askofu Josephat Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, ametolea Mfano ikitokea Abdul (Mtoto wa Rais Samia) achukuliwe na Watu halafu kesho aokotwe akiwa hana Macho, tutajisikiaje?

Ametolea mfano kile kilichofanyika kwa Mdude, kifanyike na kwa Mtoto wake au wa Waziri Mkuu au wa IGP tutajisikiaje huku akihoji kwanini wanaopotea wanachukuliwa kama Mbuzi

Soma https://jamii.app/KauliAskofuGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights
πŸ‘6
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Dkt. Josephat Gwajima, amesema Wakuu wa Vyombo vya Usalama wanapoondolewa kutokana na kutokubaliana na baadhi ya mambo ya Wanasiasa basi ipo Siku atatokea ambaye atakuwa anakubali kila kitu

Amesema "Ushauri wangu, wakuu wa Vyombo vya Usalama ili wafanye kazi zao kwa umahiri, wasiondolewe kwenye kazi zao kwa mapenzi ya Mwanasiasa aliyewaweka ili waweze kukataa baadhi ya mambo kwa maslahi ya Nchi."

Soma https://jamii.app/KauliAskofuGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Democracy
πŸ‘2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Askofu Josephat Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe amesema kuna umuhimu wa kubadili Sheria ya kuwaondoa Wakuu wa Vyombo vya Usalama kwenye nafasi zao, kwamba yeyote anapotaka kuondolewa kuwe na sababu na ziwasilishwe Bungeni ili zijadiliwe ili kuwaondolea presha watendaji hao

Akizungumza na Wanahabari leo Mei 24, 2025, ameongeza β€œKuwa na Nchi imara tunatakiwa kuwa na Vyombo vya Serikali ambavyo vikiona jambo ni hatari kwa Nchi vinasema hapana, na wakisema hivyo wasidhurike wao na familia zao.”

https://jamii.app/AskofuGwajimaMei24

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amesema hayo akiongea na Waandishi wa Habari leo, Mei 24, 2025 kuhusu matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea nchini

Soma https://jamii.app/KauliAskofuGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
Katika Maisha, mara nyingi wale wanaofanya mabaya huendelea kwa Amani kana kwamba hawaguswi, ilhali wale wanaojitahidi kuwa Waaminifu na Waadilifu hupitia maumivu na changamoto nyingi kama misumari inayogongwa kila mara. Ukweli huu unauma, lakini mara nyingi ndivyo ilivyo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend #GoodMorning #AmkaNaJF #Lifelessons
❀1πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum amewakosoa wanaomuombea mabaya Rais Samia Suluhu na kusema wanaofanya hivyo anawaombea kwa Mungu wapate Kiharusi

Amesema hayo Mei 23, 2025 alipotembelea Soko jipya la Nyama Choma la Kumbilamboto lililopo Vingunguti akiwa na Viongozi mbalimbali wa JMAT

Soma https://jamii.app/ApateStroke

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
Siku chache baada ya Serikali ya DR Congo kuonesha nia ya kumfungulia mashtaka ya uhaini na makosa ya kivita pamoja na kumhusisha na Kundi la Waasi wa M23, Rais wa zamani wa Nchi hiyo, Joseph Kabila (53) amesema inachofanya Serikali ni utawala wa mabavu

Kabila amemkosoa Rais Tshisekedi kwa kudhoofisha Katiba, Bunge kwa kushindwa kumwajibisha Rais, mfumo wa Haki kutumiwa kwa malengo ya Kisiasa, pia amekosoa Serikali inavyoshughulikia masuala ya uchumi, ufisadi na Deni la Taifa, ambalo alisema limepanda maradufu hadi zaidi ya Dola Bilioni 10 (Tsh. Trilioni 27)

Amesema β€œJeshi la Kitaifa limebadilishwa kuwa Vikundi vya Mamluki, Makundi yenye silaha, Wanamgambo wa kikabila na majeshi ya kigeni ambayo si tu yameshindwa kutimiza majukumu yao bali pia yameitumbukiza Nchi kwenye machafuko yasiyoelezeka.”

Soma https://jamii.app/KabilaMay24

#JamiiForums #Governance #Siasa
❀1
Je, wewe ni Mdau wa Teknolojia na Mitandao?

Kuanzia Mei 29 hadi Mei 31, 2025 Jukwaa la 14 la Utawala wa Mitandao Afrika litawakutanisha Wadau mbalimbali wa Teknolojia na Mitandao

Litakuwa Jukwaa la Mazungumzo, Ushirikiano na kubadilishana Mawazo juu ya masuala muhimu ya Utawala wa Mtandao (Internet Governance) Barani Afrika

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica
ZANZIBAR: Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) inaendelea kwenye Uwanja wa Amaan Complex. Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika, #Simba inaongoza kwa Goli 1-0 dhidi ya #RSBerkane

Goli limefungwa na Joseph Mutale dakika ya 17

Soma https://jamii.app/SimbaRSBerkane

#JFSports #JamiiForums #JFCAFCC
ZANZIBAR: Licha ya Timu ya #Simba kupata sare ya Goli 1-1 katika Fainali ya Pili ya CAF kwenye Uwanja wa Amaan Complex, hiyo haikuwa na faida kwao baada ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwenda kwa #RSBerkane ya Morocco

Simba ambayo imecheza pungufu muda mwingi wa kipindi cha pili baada ya Yusuph Kagoma kupata Kadi Nyekundu dakika ya 50 ilipata goli lake kupitia kwa Joshua Mutale dakika ya 17 huku wageni wakifunga kupitia kwa Soumaila Sidibe dakika ya 90+3

Hivyo, Simba imeukosa Ubingwa kwa kuwa mchezo wa kwanza RS Berkane ilishinda kwa magoli 2-0, hivyo matokeo ya jumla kuwa 3-1

Soma https://jamii.app/SimbaBerkane

#JFSports #JamiiForums #JFCAFCC
❀1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons