JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Watoto hujifunza kwa kuangalia, si kwa kusikiliza tu. Ikiwa tunataka wawe Wapole, Waadilifu na wenye Heshima, basi nasi tuwe mfano wa hayo. Maneno yana nguvu, lakini matendo yetu ndiyo yanayowalea.

#MaleziBora #JamiiAfrica #JamiiForums #GoodMorning #AmkaNaJF #ParentingInAction
MBEYA: Mimi ni Mkazi wa Isyesye, tunashukuru kwa maboresho ya barabara yanayofanyika lakini anayehusika kutengeneza njia ya michepuko (diversion) hajatengeneza na zilizopo hazipitiki, tunapata shida sana

Mkandarasi anafunga barabara pasipo kuweka alama za kuonesha tunatakiwa kupita wapi matokeo yake tunapita vichochoroni kwenye njia zisizo rasmi, hiyo ni mbaya kwa Vyombo vya Usafiri vinavyotumika

Soma https://jamii.app/MbeyaMkandarasi

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability
πŸ‘1
Friedrich Merz (69) amechaguliwa kuwa Kansela wa Ujerumani katika duru la pili la Upigaji Kura katika Bunge la Shirikisho (Bundestag), hiyo ni baada ya kushindwa kwenye duru la kwanza na sasa anachukua nafasi ya Olaf Scholz

Merz ambaye anaongoza muunganiko wa Vyama vya CDU (Christian Democratic Union), Chama ndugu CSU cha Bavaria, na SPDy (Social Democratic Party) unaoshikilia viti 328 Bungeni, amepata kura 325 kati ya 630, akivuka kiwango cha kura 316 kinachohitajika kwa wingi wa moja kwa moja

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Kansela kupoteza Kura katika awamu ya kwanza katika Bunge la Bundestag kwa Miaka 76, hali iliyozua maswali kuhusu mshikamano ndani wa muungano wao

Soma https://jamii.app/UchaguziUjerumani

#JamiiForums #Democracy #Governanc
TABORA: Akiwa katika ziara ya kutembelea vituo vya kuhakiki na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC), amesema β€œMwananchi atakayeona kuna Mpiga Kura ambaye amekosa sifa, awe huru kutumia Fomu Namba 5B ili kumuondoa huyo ambaye amekosa sifa.”

Soma https://jamii.app/UandikishajiTabora

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jaffo amefanya ziara katika Soko la Kariakoo na kueleza kuna ukiukwaji wa Sheria za Nchi unaofanywa na Wageni kwa kushirikiana na wazawa, kwa kufanya biashara bila kuwa na vibali vinavyotakiwa

Ametoa maelekezo ya kufanyika kwa msako wa kubaini wanaofanya biashara bila kufuata taratibu za Kisheria kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo Mei 7, 2025

Ikumbukwe, Aprili 16, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito kwa Serikali kuweka mifumo madhubuti ya kudhibiti, kusimamia na kuelekeza uwekezaji wa kigeni ili kuhakikisha kuwa faida za uwekezaji huo zinawanufaisha Watanzania wengi zaidi

Soma https://jamii.app/JaffoKariakoo

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu #CHADEMA Bara, Benson Kigaila amesema baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho, Mwenyekiti wao mpya Taifa, #TunduLissu aliendeleza mashambulizi dhidi ya Wanachama waliokuwa wakimuunga mkono #FreemanMbowe hali ambayo anadai iliwaonesha kuwa bado wapo katika kipindi cha Uchaguzi

Aidha, amesema baada ya uchaguzi huo, waliomuunga mkono Mbowe waliendelea kushambuliwa na wafuasi wa Lissu na kwamba suala hilo limeleta ubaguzi, huku akidai baadhi ya wafausi kadhaa ambao walimuunga mkono Mbowe wanavuliwa Uanachama

Soma https://jamii.app/G55Mei7

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA - Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita

Soma https://jamii.app/G55Mei7

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu amesema uamuzi wa yeye na wenzake kadhaa waliokuwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama Taifa kutangaza kujitoa katika chama hicho mwelekeo wao hautakuwa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (#CCM) kama inavyotafsiriwa na wengi

Soma https://jamii.app/G55Mei7

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Salum Mwalimu anasema #CHADEMA kimepoteza dira na nguvu ya ushawishi

Salum ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, anasisitiza chama hicho kinaendeshwa kwa matamko na sio vikao halali na kuwa wenye mawazo mbadala wanapingwa

Soma https://jamii.app/G55Mei7

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
πŸ‘1😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baada ya waliokuwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama Taifa ya CHADEMA kutangaza kujiondoa katika chama hicho mbele ya Waandishi wa Habari, hawakuruhusu maswali kutoka kwa Wanahabari hao kwa maelezo kuwa wawape mwaliko katika Vyombo vyao vya Habari watajibu hoja zao

Maelezo hayo yametolewa na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama hicho, John Mrema

Soma https://jamii.app/G55Mei7

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
πŸ‘6😁1
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com anasema Watoto wengi ambao walijuana na Wazazi wao ukubwani/kulelewa na Mzazi mmoja huwa na maswali mengi ambayo wengi hawayaulizi, huku Wazazi nao wakiwa na maelezo mengi sana ya nini kilitokea, lakini hawajui waanzie wapi kuwaeleza Watoto

Soma zaidi Mjadala huu https://jamii.app/WazaziMsamahaWatoto

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFStories #JFChitChats #LifeLessons
Mdau, unajuaje kama hiyo 'style' ya kunyoa inakupendeza? Huwa unaambiwa na Watu au unajiona mwenyewe kwenye kioo au ulimwambia Kinyozi akuchagulie?

Tembelea Mjadala huu zaidi https://jamii.app/StyleKunyoaMe

#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle #Utanashati #JFStories #JFChitChats
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia Suluhu ametangaza kifo cha Makamu wa Rais wa Kwanza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya ambaye amefariki leo Mei 7, 2025 alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena

Soma https://jamii.app/RIPCleopMasuya

#JFMatukio #JamiiForums #Governance
😒3
ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com kutokea Pemba anasema kuna changamoto ya kukosekana Gari la Majitaka kwenye Mitaa yao, huku akidai kipindi hiki cha mvua, kama jitihada hazitafanyika inawezekana athari zikawa kubwa ikiwemo Majitaka kuanza kusambaa Mtaani

Soma https://jamii.app/PembaGariMajitaka

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #PublicHealth #Afya
πŸ₯΄1