JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kada wa CHADEMA, Mdude Nyagali anadaiwa kukamatwa usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2025 akiwa katika makazi yake Mbeya na Watu wanaodaiwa kujitambulisha kuwa ni Polisi

Taarifa iliyochapishwa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi imeeleza kuwa inadaiwa Watu hao walibomoa mlango wa nyumbani kwa Mdude na kisha kuingia ndani wakiwa na silaha za moto, ambapo walimpiga na kuondoka naye

JamiiForums inaendelea na jitihada za kutafuta taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhusu taarifa hizo zilizotolewa na Mwabukusi

Zaidi soma https://jamii.app/MdudePolisi

#HakiZaBinadamu #Demokrasia #HumanRights #SocialJustice
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanasiasa James Mbatia amezungumzia tukio la kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Charles Kitima akidai waliofanya tukio hilo wanaonekana ni Watu wenye mafunzo ya juu na kwamba walilenga kumdhulumu uhai wa Kiongozi huyo wa Dini

Ikumbukwe tukio hilo lilitokea Aprili 30, 2025, baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, Jumanne Muliro akasema wanamshikilia Rauli Mahabi “Haraja” na uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo

Soma https://jamii.app/MbatiaOnKitima

#JamiiForums #HumanRights #JFMatukio
👍2
Mdau kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu maslahi ya Watumishi wa Sekta Binafsi, baada ya Serikali kuongeza Mishahara kwa asilimia 35.1 kwa Wafanyakazi wa Umma wanaolipwa kima cha chini, huku kukiwa bado na hali ya sintofahamu kwa upande wa Wafanyakazi wa Sekta Binafsi

Wafanyakazi wa Sekta binafsi wamekuwa wakilalamikia Mazingira duni ya Kazi, Mishahara midogo isiyoendana na gharama za Maisha, kutokuwepo kwa Mikataba ya Ajira iliyo wazi na ya Haki, nk

Kwa mtazamo wako, nini kinakwamisha upatikanaji wa maslahi bora kwa Wafanyakazi wa Sekta Binafsi?

Mjadala https://jamii.app/MishaharaSektaBinafsi

#JamiiForums #JamiiAfrica
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amekosoa utaratibu uliotokea Mahakama ya Kisutu kuhusu uamuzi wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu kusikilizwa kwa njia ya Mtandao badala ya kufikishwa Mahakamani, akidai uamuzi huo ulikuwa wa Hakimu na siyo Mahakama

Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2

#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi ametoa wito kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kutoa maelekezo na kama hatatimiza hilo awajibike kuhusu tukio la Raia kukamatwa, kuzungushwa kwenye Magari na baadaye baadhi yao kutupwa kwenye Msitu

Amesema hayo akikumbushia matukio kadhaa yaliyotokea Aprili 24, 2025 wakati wa mchakato wa kufuatilia shauri linalomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika Mahakama ya Kisutu

Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2

#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
2👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi akizungumza na Wanahabari, leo Mei 2, 2025 ametoa wito kuwa kuna umuhimu wa uwepo wa chombo kinachoweza kusimamia utendaji wa Mamlaka mbalimbali za Serikali ikimemo Jeshi la Polisi ili kuongeza Uwajibikaji

Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2

#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
👍1
KAGERA: Meneja wa Wakala wa Barabara (#TANROADS) Mkoa, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya amesema ujenzi wa Barabara njia Nne Bukoba kutoka Rwamishenye - Makutano ya Barabara ya Stendi ya Mabasi unaendelea baada ya kusuasua kwa muda, akieleza unatarajiwa kukamilika Novemba 2025

Kutokamilika kwa Barabara hiyo kumelazimisha Wananchi kutumia njia mbadala kwa kuzunguka kupitia Nyakanyasi, ambapo Mhandisi Ntuli amesema “Wananchi wamekuwa na maswali, hatujalala, kazi inaendelea, tunaendelea na ukarabati wa Daraja la Kanoni.”

Ikumbukwe Desemba 6, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alihoji kuhusu mchakato huo kwa kuandika “Ujenzi wa Njia Nne Bukoba unasuasua, Mamlaka hazifahamu Barabara hiyo ndio mlango wa Uchumi wa Mji?”

Soma https://jamii.app/BarabaraKagera

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema madai ya Waandishi wa Habari kudaiwa kupigwa na Jeshi la Polisi wanatakiwa kwenda Mahakamani ili kupata Haki. Pia, ametoa wito kuwa raia hawatakiwi kujifanya ‘Wadwanzi’ bila kuangalia hatari zinazoweza kutokea mbele, hawatakiwi kulaumu Jeshi la Polisi

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
1
MBEYA: Jeshi la Polisi Mkoani humo limekanusha taarifa zinazolituhumu Jeshi hilo kuhusika katika tukio la kuvamia Nyumba ya Kada wa CHADEMA, Mdude Nyagali, kumpiga, kumjeruhi na kisha kuondoka naye kusikojulikana na kusema kuwa wanaendelea na ufuatiliaji

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo Mpaluka Said (Mdude) azitoe ili kufanikisha kumpata pamoja na taarifa za Watu waliohusika katika tukio hili ili waweze kukamatwa

Taarifa ya Jeshi hilo imeeleza Mei 02, 2025 majira ya asubuhi, walipokea taarifa kutoka kwa Sije Mbugi Emmanuel (Mke wa Mdude) kuwa majira ya saa 08:00 usiku wakiwa wamelala, Watu wasiofahamika waliwavamia baada ya kuvunja mlango na kuingia ndani na kisha kumjeruhi Mdude sehemu mbalimbali za Mwili wake na kutoweka naye

Soma https://jamii.app/PolisiMbeyaMei2

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Timu ya #Simba imepata ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni siku chache tangu Simba ilipoingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF)

Mashujaa FC ilitangulia kufunga kupitia kwa Jaffar Kibaya dakika ya 5, Simba ikasawazisha kupitia kwa Leonel Ateba dakika ya 65 kwa njia ya penati ambaye pia aliongeza la pili dakika ya 90+15 kwa penati pia

Simba imeendelea kubaki nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi ikifikisha pointi 60 katika michezo 23, nyuma ya Yanga yenye alama 70 yenye michezo 26, huku Mashujaa FC ikiwa nafasi ya 10 kwa kuwa na alama 30 katika michezo 27

Soma https://jamii.app/SimbaMashujaaFC

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
👍31
DAR: Balozi mbalimbali Nchini ikiwemo Marekani, Sweden na Umoja wa Ulaya wamelaani tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025

Balozi hizo zimesisitiza kutafutwa kwa Haki kupitia uchunguzi wa haraka na wa wazi

Upande wa Ubalozi wa Marekani umeeleza “Tunalaani vikali vitendo vyote vya ukatili, hasa vile vinavyolenga kunyamazisha wito wa Haki, Maridhiano na Haki za Binadamu.”

Soma https://jamii.app/USEmbassyOnKitima

#JamiiForums #Democracy #Accountability #Kuelekea2025
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Wanahabari, leo Mei 2, 2025, Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, amesema taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, ni ya awali na hivyo haitakiwi kulishwa maneno ikiwemo kusema alivamiwa na Walevi

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amewataka Wananchi kuendelea kuwa na imani na Jeshi la Polisi wakati uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima ukiendelea

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
👎1
Tunakutakia Mapumziko mema ya mwisho wa Wiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend
👍2
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba wa kufanya uchunguzi juu ya tukio la Kada wa #CHADEMA, Mdude Nyagali ambaye imeelezwa alivamiwa, akapigwa na kuchukuliwa na Watu ambao utambulisho wao haujajulikana

LHRC imesema tukio hilo lililotokea katika Makazi ya Mdude, Mkoani Songwe na mengine ya namna hii yanayoendelea kuvunja Haki za Binadamu Nchini yanatakiwa kuchukuliwa natua na Mamlaka hiyo

Pia, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Fulgence Massawe, amesema wamelitaka Jeshi la Polisi Songwe kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa shambulio hilo la kikatili

Soma https://jamii.app/LHRCKuhusuMdude

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance