ARUSHA: Akishiriki Majadiliano katika Siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mercy Ndegwa, Mwakilishi wa Kampuni ya Meta amesema Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na wadau pamoja na Serikali kuboresha Mazingira ya Kidigitali ikiwemo watumiaji wa majukwaa hayo kuingiza kipato
Amesema "Tumeona platforms zetu za WhatsApp na Instagram zimekuwa zikifanya vizuri na kupiganiwa na Watu wengi, tunaona namna gani ya kuweka njia ya kuingiza Fedha (Monetization), tunafanya hivyo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kwa ukaribu wakiwemo JamiiAfrica"
Ndegwa ameongeza "Tumepitisha mambo kadhaa ikiwemo masuala ya Kodi, ambayo kabla ya kuchukua Maamuzi tunashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutimiza hilo, ili lifanyike kwa njia sahihi, pamoja na hivyo tunazidi kufikiria vitu kwa ajili ya kuboresha ‘tools’ zetu"
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia

❤1
Akizungumzia suala la Waandaa Maudhui kunufaika kupitia Majukwaa ya Kidigitali, Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica amesema "Tumezungumza na wenzetu #Meta, tunashirikiana nao na baadhi ya vikao kati yetu na wao tutafanya kwa njia ya Digitali ili Wadau wengine washiriki na waweze kutoa maoni yafanyiwe kazi. Mikutano hiyo itashirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo wa Serikalini na Sekta Binafsi"
Awali Mwakilishi wa Meta, Mercy Ndegwa alisema wameona Majukwaa yao ya Whatsapp na Instagram yamekuwa yakifanya vizuri, hivyo kwa kushirikiana na Wadau wanatafuta namna ya kuweka njia ya kuwawezesha Watumiaji wa majukwaa hayo kujipatia Fedha (Monetization)
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Awali Mwakilishi wa Meta, Mercy Ndegwa alisema wameona Majukwaa yao ya Whatsapp na Instagram yamekuwa yakifanya vizuri, hivyo kwa kushirikiana na Wadau wanatafuta namna ya kuweka njia ya kuwawezesha Watumiaji wa majukwaa hayo kujipatia Fedha (Monetization)
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍2
ARUSHA: Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) yanaendelea, leo Aprili 29, 2025 ikiwa Siku ya pili ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
Awali, Aprili 27, 2025 Washiriki na Wadau mbalimbali walishiriki katika mbio (Fun Run) za Kilometa Tano kisha Aprili 28, 2025 kulifanyika mijadala tofauti ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua
Fuatilia https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Awali, Aprili 27, 2025 Washiriki na Wadau mbalimbali walishiriki katika mbio (Fun Run) za Kilometa Tano kisha Aprili 28, 2025 kulifanyika mijadala tofauti ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua
Fuatilia https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Akizungumza katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema Wanahabari wana uwezo mkubwa wa kutengeneza ajenda ya kuwafanya Wananchi wote waelekeze Mawazo yao katika jambo fulani
Amesema “Ningekuwa na uwezo ningewashawishi watusaidie kwa nguvu zao zote kubadilisha aina ya Habari zinazosikika kwa Wananchi, Habari ina nguvu kubwa sana, inaamua aina ya chakula, mavazi na kila kitu.”
Makonda ameongeza “Wanahabari wakiamua watatusaidia kututengenezea mwelekeo wa Habari za kiuchumi na nyingine za maendeleo, hilo ni jambo zuri.”
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Amesema “Ningekuwa na uwezo ningewashawishi watusaidie kwa nguvu zao zote kubadilisha aina ya Habari zinazosikika kwa Wananchi, Habari ina nguvu kubwa sana, inaamua aina ya chakula, mavazi na kila kitu.”
Makonda ameongeza “Wanahabari wakiamua watatusaidia kututengenezea mwelekeo wa Habari za kiuchumi na nyingine za maendeleo, hilo ni jambo zuri.”
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
NIGERIA: Mahakama Kuu ya Wilaya ya Shirikisho (FCT) huko Abuja, imemhukumu Peter Nwachukwu, Mume wa Marehemu mwimbaji wa nyimbo za Injili, Osinachi, adhabu ya kifo kwa kunyongwa baada ya kumkuta na hatia kwa kumuua Osinachi kwa makusudi, Aprili 8, 2022
Ingawa taarifa za awali zilidai kuwa Osinachi alifariki kutokana na Ugonjwa wa Saratani, ushuhuda kutoka kwa Familia, waumini wenzake Kanisani na Majirani, ulifichua kuwa alikuwa mwathirika wa Ukatili wa majumbani
Mashahidi walieleza kuwa Nwachukwu alimkanyaga Osinachi kifuani kabla ya kifo chake. Baadaye Nwachukwu alishtakiwa kwa makosa 23, yakiwemo kuua kwa makusudi, vitisho vya jinai, ukatili dhidi ya Watoto na vipigo kwa Mwenzi wa Ndoa
Soma https://jamii.app/HukumuMumeOsinachi
#JamiiForums #HakiZaBinadamu #Accountability

ARUSHA: Balozi wa Saudi Arabia-Tanzania, Yahya bin Ahmed Okeish amesema kuna uwekezaji mkubwa ambao unafanywa na Taifa lake katika masuala ya Kidigitali kwa kuwa huko ndipo Dunia inapoelekea
Amesema wamewekeza kwenye Akili Mnemba (AI) kutokana na ukuaji wa Teknolojia na kwamba zaidi ya Dola Bilioni 20 (Tsh. Trilioni 53) zimewekezwa kwa ajili ya ushirikiano na Wadau wa Digitali lengo likiwa ni kuendana na Mabadiliko ya Teknolojia
Ameongeza “Mwaka 2024, Saudi Arabia ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika masuala ya ulinzi wa Kidigitali na Mawasiliano, hali hiyo iliongeza Uaminifu kwa Wawekezaji na wageni walifika katika Taifa letu.”
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Amesema wamewekeza kwenye Akili Mnemba (AI) kutokana na ukuaji wa Teknolojia na kwamba zaidi ya Dola Bilioni 20 (Tsh. Trilioni 53) zimewekezwa kwa ajili ya ushirikiano na Wadau wa Digitali lengo likiwa ni kuendana na Mabadiliko ya Teknolojia
Ameongeza “Mwaka 2024, Saudi Arabia ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika masuala ya ulinzi wa Kidigitali na Mawasiliano, hali hiyo iliongeza Uaminifu kwa Wawekezaji na wageni walifika katika Taifa letu.”
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Wadau wa Habari kupitia Maazimio waliyoyatoa katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025 wameeleza kuwa kadiri Akili Mnemba (AI) inavyoathiri Uandishi wa Habari, wanapendekeza kuwepo kwa Mifumo madhubuti ya Kitaifa ya kusimamia matumizi yake kwa Uwajibikaji katika Sekta ya Habari
Wametoa wito kwa Serikali kuweka mazingira rafiki ya Kisheria na Kiutawala yanayowezesha Vyombo vya Habari na Wabunifu wa Maudhui kupata mapato kupitia michango ya Wanachama, Usajili, Malipo kwa kila makala au Michango ya hiari kutoka kwa watumiaji.
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Wametoa wito kwa Serikali kuweka mazingira rafiki ya Kisheria na Kiutawala yanayowezesha Vyombo vya Habari na Wabunifu wa Maudhui kupata mapato kupitia michango ya Wanachama, Usajili, Malipo kwa kila makala au Michango ya hiari kutoka kwa watumiaji.
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mwakilishi wa UNESCO Nchini Tanzania, Michel Toto amesema Uhuru wa Vyombo vya Habari ni nguzo muhimu katika Jamii za Kidemokrasia
Ametoa wito kwa wadau wa Sekta ya Habari kuzingatia kuwa Uhuru wa Kujieleza, hasa katika zama za Maendeleo ya Akili Mnemba (AI), unakumbwa na changamoto mpya na tata. Pia, Usalama wa Waandishi wa Habari hasa Wanawake, unahitaji hatua za haraka na mshikamano wa wadau wote
Aidha, amesema Uhai wa Vyombo Huru vya Habari uko katika hatari kubwa kuliko wakati wowote, hivyo kunahitajkai juhudi za makusudi kulinda na kuviimarisha
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#JamiiAfrica #JamiiForums #AIandMedia #PressFreedom #WPFD2025

ARUSHA: Wadau wamesema kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, wanasisitiza umuhimu wa kuhakikisha Usalama na Heshima ya Waandishi wa Habari Nchini, wakitoa wito kwa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wanasiasa na Jamii kwa ujumla kuhakikisha Waandishi wanalindwa dhidi ya Vitisho, Unyanyasaji au Vurugu kipindi hiki nyeti
Wadau wamependekeza hatua za Kitaifa na Miongozo ya Usalama zitekelezwe mara moja ili kuruhusu Waandishi wa Habari kufanya kazi katika Mazingira salama, bila hofu wala bugudha
Wameeleza hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025, ambapo mapendekezo mengine ni Kupambana na Taarifa Potofu na Kukuza Uadilifu katika Uandishi wa Habari na Matumizi Sahihi ya Teknolojia Mpya
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Wadau wamependekeza hatua za Kitaifa na Miongozo ya Usalama zitekelezwe mara moja ili kuruhusu Waandishi wa Habari kufanya kazi katika Mazingira salama, bila hofu wala bugudha
Wameeleza hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025, ambapo mapendekezo mengine ni Kupambana na Taarifa Potofu na Kukuza Uadilifu katika Uandishi wa Habari na Matumizi Sahihi ya Teknolojia Mpya
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaulinda Uhuru wa Habari na inafanya hivyo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo Wadau wa Habari
Amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika Kitaifa katika Hoteli Grand Melia yakilenga kubadilishana mawazo na kufanya majadiliano kuhusu fursa na changamoto za Akili Mnemba (AI) katika Sekta ya Habari
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika Kitaifa katika Hoteli Grand Melia yakilenga kubadilishana mawazo na kufanya majadiliano kuhusu fursa na changamoto za Akili Mnemba (AI) katika Sekta ya Habari
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika kuboresha Mazingira ya Sekta ya Habari, Wadau wanatakiwa kutoa maoni zaidi kuhusu Sera ya matumizi ya Akili Mnemba (AI) iweje, wakati huo huo Serikali inaendelea na maboresho ya Sera ya Utangazaji ya Mwaka 2003
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo
#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itayapokea maoni ya Wadau wa Habari na itayafanyia kazi hata kama itakuwa ni masuala ya mabadiliko ya Sera, Kanuni au Sheria
Ameeleza hayo katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, ambapo Kaulimbiu ya Mwaka huu ni 'Uhabarishaji kwenye Dunia mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari'