JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Chit-Chats and Jokes amesema kuna vitu 'special' vinavyotambulisha maeneo fulani bila hata ya kuangalia 'location' ya mahali ulipo

Kwako Mdau, ni kitu gani ukikiona unajua umeingia Tanzania?

Mjadala https://jamii.app/UnajuajeUmeingiaTz

#JamiiForums #Maisha
πŸ‘1
DAR: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ratiba ya Siku za Mgao wa Umeme kuanzia Februari 22 hadi 28, 2025

Ikumbukwe TANESCO walitangaza mgao wa Umeme kwa baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar kutokana na maboresho katika kituo cha kupokea, kupoza, na kusambaza Umeme cha msongo wa Kilovolti 220 kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/RatibaMgaoUmemeDar

#HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #JamiiForums #Accountability
Kwa kiwango gani 'uchawa' unachangia kuzorota kwa #Uwajibikaji Nchini, na tunapaswa kufanya nini ili kurejesha misingi ya Uwajibikaji?

Jiunge nasi kwa mjadala wa "Kujipendekeza 'uchawa' kuzorotesha Uwajibikaji: Tunatokaje hapa?" ambapo tutajadili kwa kina kuhusu changamoto hii na hatua madhubuti za kufanikisha mabadiliko chanya kwa maslahi ya Taifa

Ni Alhamisi, Februari 27, kuanzia Saa 12 Jioni - 2 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
❀1πŸ‘1
DAR: Mwanasiasa Dkt. Willbroad Slaa (76) ameomba Mahakama ya Rufaa impatie dhamana huku akisubiri rufaa yake ya jinai kusikilizwa

Ombi hili limewasilishwa Februari 21, 2025 chini ya hati ya dharura kubwa na wakili wake, ikielezwa Dkt. Slaa amewekwa rumande kinyume cha sheria na kwamba Afya yake inaendelea kuzorota akiwa Gerezani licha ya kuwa kosa linalomkabili linastahili dhamana

Kwa mujibu wa Wakili amesema "Kufungwa kwa Dkt. Slaa katika Gereza la Keko ni kitendo kinachosababisha madhara yasiyorekebishika. Kwa misingi hiyo, tunaiomba Mahakama itoe uamuzi wa haraka juu ya maombi haya ya dhamana,"

Soma https://jamii.app/DrSlaaOmbiDhamana

#JamiiForums #JFMatukio
πŸ‘2❀1
Usikubali tamaa ya pesa ikuharibie ndoto zako na za kizazi kijacho. Kumbuka, kura yako ni sauti yako, na sauti yako ina thamani kubwa kuliko hongo ya muda mfupi.

Unapokubali pesa ili umpigie kura Mtu fulani, unauza Haki yako ya kushiriki kwenye maamuzi yanayohusu Maisha yako na jamii yako.

Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu wanaochaguliwa kwa uwezo wao, si kwa kiasi cha pesa wanachotoa ili kushinda

Kataa #Rushwa ya Uchaguzi

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji
πŸ‘1
UGANDA: Imeelezwa Kizza Besigye na Msaidizi wake walichukuliwa kinguvu huko Nairobi, na kurejeshwa Uganda, Novemba 2024, ambapo walifikishwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi wakikabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha Sheria na Uhaini

Uamuzi wa Mahakama ya Juu wa Januari 31, 2025 ulieleza raia hawawezi kushtakiwa katika Mahakama za Kijeshi, hivyo kesi yao ikahamishiwa Mahakama ya Kiraia

Hata hivyo, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kumsomea Besigye mashtaka mapya ya uhaini na kula njama ya kuiangusha Serikali, Hakimu Esther Nyadoi alieleza Mahakama yake haina mamlaka ya kuendelea na shauri hilo, kwani mashtaka hayo yanapaswa kushughulikiwa na Mahakama za juu zaidi

Soma https://jamii.app/BesigyeUhaini

#JamiiForums #Demokrasia #Governance
DAR: Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, akizungumza na Mwananchi, Februari 21, 2025 amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu watakaa vikao na kutoa utaratibu wa kuwapata Wabunge wa Viti Maalum wa Chama hicho

Amesema "Viti maalumu ni mali ya Chama cha Siasa, sasa kwa kuwa CCM ina UWT basi inapewa dhamana ya kuwapata Wabunge wa Viti Maalumu. Inawezekana mjadala ukawepo kwamba wapo kinamama walioko Jumuiya ya Wazazi, wapo kinadada walioko UVCCM, hii keki yote ya kwetu basi tuongezewe."

Ameongeza, β€œTutakapokaa vikao kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi, CCM itatoa utaratibu. Marekebisho yalifanyika kuhusu utaratibu wa kupiga kura za maoni ya kuwapata Wabunge wa majimbo, wawakilishi na Madiwani wanaotokana na CCM, lakini kutakuwa na marekebisho mengine yatakayoongeza wigo wa namna ya kuwapata Wabunge wa Viti Maalumu.”

Soma https://jamii.app/VitiMaalumCCM

#JamiiForums #Demokrasia #JFWomen #WomenInPolitics #WanawakeNaSiasa
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Baada ya kusambaa kwa video inayodaiwa ni ya Februari 20, 2025 inayoonesha Watu kadhaa waliokuwa na Gari aina ya Noah nyeusi wakimpiga na kumlazimisha Mtu ambaye utambulisho wake haujafahamika kuingia kwenye Gari hilo, Polisi imesema inafanya uchunguzi

Video iliyorekodiwa na Mwananchi inaonesha tukio hilo lilitokea mchana maeneo ya Njuweni – Kibaha, Watu hao wakipambana na kijana aliyekuwa na pikipiki na baadaye kufanikiwa kumfunga pingu na kisha kuondoka naye

JamiiForums imewasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, kuhusu tukio hilo na amesema: "Sina taarifa kamili juu ya tukio hilo, nami naliona tu, naomba mtupe muda tulifuatilie na tufanye uchunguzi wa kujua kilichotokea."

Soma https://jamii.app/KibahaNjuweni

#JamiiForums #JFMatukio #HumanRights #CivilRights
πŸ‘1
Elimu si tu kuhusu kupata maarifa, bali ni chombo cha ukombozi kinachowezesha Jamii kuelewa Haki zao, kupinga dhuluma, na kujijenga Kiuchumi na Kijamii

Haki ya kupata Elimu inapotolewa kwa kila Mtu, Watu hujifunza Historia yao, Tamaduni zao, na nafasi yao katika Jamii, hivyo kuwa na uwezo wa kudai Usawa na Haki.

#ElimuNiNguvu #HakiZaBinadamu #HakiZaKiraia #JamiiForums #ElimuNiHaki #CivilRights
PWANI: Baada ya kusambaa kwa video inayoonesha Watu kadhaa wakipambana na Kijana aliyekuwa na Pikipiki, kisha kuondoka naye kwa kumuingiza katika gari aina ya Noah, Jeshi la Polisi limesema hilo ni tukio la ukamataji lililofanywa na Askari Polisi, Februari 20, 2025 katika eneo la Maili Moja, Pwani

Taarifa ya Polisi imeeleza Mtuhumiwa ni Rajabu Hassan na alikuwa anatafutwa kutokana na tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji kwa kutumia Pikipiki ikiwa imekunjwa namba za usajili (plate number) na wakati mwingine ikiwa haina namba ya usajili kwa jina maarufu 'Vishandu'

Taarifa imeeleza wakati wa ukamataji alianzisha vurugu ili kukaidi ukamataji licha ya Askari Polisi kujitambulisha kwake, ambapo walimfikisha Kituo cha Polisi Kibaha ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili na kuwa hata ndugu zake wanazo taarifa kuwa anashikiliwa katika Kituo hicho.

Soma https://jamii.app/PolisiTaarifa

#JamiiForums #JFMatukio #CivilRights #HumanRights
❀1πŸ‘1
Je, tabia ya 'uchawa' inachangia vipi kuzorota kwa Uwajibikaji nchini? Ni kwa namna gani tunaweza kujenga Jamii inayowataka Viongozi wawajibike badala ya kuwasifu hata pale wanapokosea au kutimiza majukumu yao?

Kufahamu haya na mengine, tafadhali jiunge nasi katika Mjadala muhimu wa Uwajibikaji kupitia Xspaces ya JamiiForums, Alhamisi ya Feb. 27, kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku

Washiri watapata fursa ya kusikiliza, kutoa maoni au hata kuuliza maswali

Kujiunga Bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ELIMU: Umoja wa Walimu wasio na Ajira (NETO) wakiongea na Waandishi wa Habari wametoa mapendekezo 16 kwa Serikali ili kuipa hadhi kada ya Ualimu kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada hiyo

Miongoni mwa Mapendekezo hayo yaliyosomwa na Katibu wa NETO, Daniel Edigar Mkinga, ni kusitisha usaili mara moja kwa kada ya Ualimu na kutumia utaratibu wa awali

Mapendekezo mengine ni Vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha Mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu Mtaani na kusitisha uzalishaji wa Walimu Vyuoni hadi waliopo Mtaani wapate Ajira

Soma https://jamii.app/UalimuNaAjira

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #UnemploymentCrisis
πŸ‘1
Kupiga kura si jukumu tu bali ni njia ya kushiriki katika ujenzi wa Jamii tunayoitamani. Kila kura ina nguvu ya kuleta Mabadiliko na kuhakikisha Viongozi tunaowachagua wanawakilisha maslahi yetu kwa Haki na Uadilifu

Mwaka huu (2025) amua kuitumia Haki yako ya Kupiga Kura kikamilifu

#KuraYakoNiNguvuYako #HakiYaKupigaKura #HakiZaKiraia #CivilRights #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #SautiYakoNguvuYako #Demoracy
πŸ‘1
Je, umewahi kufikiria madhara ya kupokea pesa au zawadi ili kumpigia mtu kura? Hii ina maana ya kuruhusu ufisadi kustawi, kudumisha huduma duni, na kurudisha nyuma maendeleo ya jamii yako

Rushwa ya uchaguzi huwadhoofisha wananchi kwa kuwaweka madarakani viongozi wasiostahili, wasio na nia ya kutumikia umma, bali wenye maslahi binafsi.

Kemea #Rushwa ya Uchaguzi. Chagua viongozi kwa haki, misingi ya uadilifu na uwezo wao wa kuleta mabadiliko chanya

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji
❀1
Mdau kutoka Jukwaa la Siasa ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu ufahamu wa Kizazi cha Gen Z kuhusu Daftari la Wapiga Kura ambapo zoezi la kujiandikisha linaendelea nchini

Mdau ni njia gani inaweza kutumia ili vijana (Gen Z) waweze kushiriki katika zoezi hilo

Mjadala zaidi https://jamii.app/GenZDaftariKura

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #Accountability
❀3πŸ‘1