JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imeanza kusafisha maeneo ya Mto Ngerengere, Mazimbu Manispaa ya Morogoro ili kuweka mazingira safi, kuruhusu maji kupita kwa urahisi na kupunguza athari wakati wa mafuriko

Afisa wa Maji Bonde la Wami Ruvu Kidakio cha Ngerengere, Mhandisi Nangu Makula amesema zoezi hilo litaenda umbali wa Mita 900 (Mazimbu hadi Kihonda)

Ikumbukwe Desemba 8, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito kwa taka zitolewe katika mto huo kwa kuwa zimechangia maji kuingia mtaani, akatolea mfano wanaokuwa hatarini zaidi ni Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mahlangu

Soma https://jamii.app/MtoNgerengereUsafi

#Accountability #ServiceDelivery #JamiiForums #ClimateChange
πŸ‘1
Je, unataka Viongozi waadilifu, wenye dira na nia thabiti ya kuleta mabadiliko chanya? Au unataka kulalamika kwa Miaka mitano ijayo kwasababu ya uamuzi mbaya? Kila kura inahesabika, na kila sauti ina umuhimu

Usikubali kushawishiwa kwa ahadi za muda mfupi, pesa au zawadi zisizo na maana. Badala yake, tafakari kwa kina kuhusu nani ana uwezo wa kubadilisha Maisha yako na Maendeleo ya Jamii yako.

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
πŸ‘1
Kesi ya Haki (Right to Fair Trial) inapokosekana Watu wanaweza kunyimwa Haki yao ya msingi ya kutetewa, kupewa adhabu isiyo ya Haki au hata kuhukumiwa kwa makosa wasiyoyafanya

Mahakama zinapaswa kuwa huru na zisizoingiliwa na Serikali, Vyombo vya Usalama au Mashinikizo ya Kisiasa

Aidha, Mtuhumiwa ana Haki ya kukata Rufaa ikiwa anahisi kuwa kesi yake haikusikilizwa kwa Haki

Soma zaidi https://jamii.app/RightToFairTrial

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #KesiYaHaki #HakiZaBinadamu #UtawalaWaSheria
Mdau kutoka la Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu sababu za Kizazi cha "Gen Z" kufukuzwa kazi ndani ya muda mfupi akitumia utafiti uliofanywa na Tovuti ya Intelligent.com

Je, unakubaliana na maoni haya?

Mjadala zaidi https://jamii.app/GenZKufuzwaKazini

#JamiiForums #LifeStyle #GenZWorkplace
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu akizungumza na Waandishi wa Habari na kuelezea wanachomaanisha pale wanaposema 'No Reform, No Election'

Zaidi https://jamii.app/PressLissuFeb12

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #Democracy
Mdau wa JamiiForums.com anadai kuna changamoto wakati wa kuhuisha Leseni za Daladala zilizopewa vibali Mwaka 2023 katika 'ruti' ya Mbezi - Bagamoyo kwa maelezo kuwa wamepewa kimakosa

Anaeleza wamefanya kazi kwa takriban Miaka 2 halafu Mwaka wa tatu huu wanaambiwa wamepewa leseni kimakosa, anahoji Je, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA) inawatendea Haki wamiliki na Abiria wanaosafiri kupitia njia hiyo?

JamiiForums imewasiliana na Afisa Mfawidhi LATRA - Pwani, Aisha Kuwa kuhusu hoja hiyo, amesema β€œKwa Mkoa wangu wa Pwani hilo jambo halijafika kwangu. Kwa kawaida wakikataliwa kupewa Leseni huwa kuna maelekezo wanapewa, nadhani hilo ngoja tulifuatilie kwa ukaribu kujua kinachoendelea.”

Soma https://jamii.app/LATRAMbeziBMoyo

#JamiiForums #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MARA: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, John Heche akizungumza katika hadhara iliyompokea alipowasili Tarime amesema yeye na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu wapo tayari kupoteza maisha ili kulinda msimamo wa Chama wa kutetea Wananchi

Soma https://jamii.app/HecheTarime

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #Democracy
πŸ”₯2
Siku ya Redio huadhimishwa Februari 13 kila mwaka ili kuhamasisha umuhimu wa Redio katika Kuhabarisha Jamii na kukuza Uhuru wa Kujieleza

Mdau, tujikumbushe zamani, tuma salamu kwa Watu watatu Kidijitali kwa 'kuwatag'

Soma https://jamii.app/WorldRadioDay

#JamiiForums #WorldRadioDay2025 #FreedomOfSpeech #DigitalRights
Shiriki katika Mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?" kupitia X Spaces ya JamiiForums

Usikose kujiunga nasi leo Februari 13, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi Saa 2:00 Usiku

Kushiriki, bofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameishauri Serikali kuangalia mikataba kwa lengo la kutoa fursa kwa Wakandarasi wazawa kupata nafasi katika miradi mbalimbali, ametoa ushauri huo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 13, leo Februari 13, 2025

Soma https://jamii.app/WakandarasiFeb

#JamiiForums #Governance
Akijibu hoja ya Mdau wa JamiiForums.com kuwa kuna kero kwa Abiria wanaopanda Daladala za Mbezi - Mlandizi kwamba muda wa Jioni zinakatisha ruti, Afisa Mfawidhi wa #LATRA Mkoa wa Pwani, Aisha Kuwa amesema wanachukua hatua kudhibiti hilo

Aisha amesema β€œTumekuwa tukiendelea na ukaguzi kuanzia Asubuhi hadi Jioni, hayo Magari ambayo Mdau ameyalalamikia sio Jioni tu hata Mchana au Asubuhi wapo wanaofanya hivyo."

Ameongeza β€œPia, ruti zote kuanzia Mbezi kwenda Mlandizi, Mbezi – Kwala, Mbezi - Mzenga tumesitisha utoaji wa leseni mpya kwa kuwa inaonekana Gari ni nyingi tofauti na idadi ya Abiria ndio maana kuna muda wahusika wanasitisha ruti kwa kuwa wanaona hasara kwenda na Abiria wachache hadi mwisho."

Soma https://jamii.app/LATRAPwaniLeseni

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Wadau mbalimbali ndani ya JamiiForums.com wametoa wito kwa Mamlaka husika kushughulikia changamoto ya Ulipwaji wa Fedha za Kujikimu kwa Waajiriwa Wapya wa Serikalini katika Kada ya Afya kwani wanategemea malipo kujikimu kimaisha

Soma https://jamii.app/MalipoKadaYaAfya

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2025
πŸ‘1