JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Uongozi bora haununuliwi, unachaguliwa kwa uadilifu. Kiongozi anayetanguliza pesa ili achaguliwe anajali maslahi yake zaidi ya Wananchi

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu, Usidanganywe na pesa, chagua kiongozi mwenye maono na dhamira ya kweli kwa maendeleo ya Jamii yako

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka kuboresha mazingira ya usalama wa Barabara za Kisemvule-Mkuranga huku akitoa wito kwa madereva kuheshimu alama za Barabarani ili kulinda usalama wa Watu na Vyombo vya Usafiri vinavyotumika

Soma https://jamii.app/ZebraKufutikaMkuranga

#JFUwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #JamiiForums
SINGIDA: Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Wakazi wa Mtaa wa Ginery maeneo ya Singida Sekondari wamekuwa wakiteseka kutokana na ubovu wa Barabara, Barabara hiyo imeanza kufanyiwa maboresho

Mdau alidai mara nyingi wamekuwa wakipewa ahadi za maboresho lakini hakuna utekelezaji, hivyo akatoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kushughulikia changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/KeroBarabaraSingida

#JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #Governance
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change Mwaka 2022 alipendekeza Kampeni zinazofanyika ili Kumkomboa Mwanamke ziende sambamba na Uelimishwaji wa Wanaume ili kuepuka kuvunja Haki za Wanaume wakati wa kumpatia Mwanamke Haki zake

Anasema Kampeni zisijikite upande mmoja bila kutoa mwanya kwa Mwanaume kuwa kwenye nafasi ya kutengeneza dhana yenye tafsiri chanya juu ya Mwanamke aliyekombolewa hasa kwenye kujua Haki zake

Aidha, anasema Jamii hususani Wanawake wanapaswa kutambua kuwa Mkakati wa Haki sawa kwa wote sio Silaha ya Kudidimiza Haki za Wanaume.

Soma zaidi https://jamii.app/HakiKeVsHakiMe

#JamiiForums #HumanRights #SOC2022 #GBV #HakiZaKiraia #CivilRights #JFWomen
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kudhibiti foleni ya malori barabara ya Morogoro (Ubungo hadi Kimara) hasa wakati wa usiku ambapo magari mengine na usafiri wa Umma yanayotoka kazini

Soma https://jamii.app/FoleniMaloriMorogoro

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
👍1
Wadau wa Jukwaa la Siasa ndani ya JamiiForums.com wanasema Serikali iache kusema inatoa Huduma za Kijamii 'Bure' bali itumie neno 'Nafuu' kwasababu huku Mtaani neno bure halionekani kwenye Uhalisia

Wanasema wakati mwingine Mtu anayepatiwa Huduma inayodaiwa kutolewa 'Bure' anapotakiwa kulipia chochote hutokea Ugomvi na Wahudumu kwa kudhani wanataka kumuibia Pesa yake lakini kumbe tamko la bure lipo Kisiasa zaidi na sio Kiutendaji

Soma https://jamii.app/TamkoBureKisiasa

#JamiiForums #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Accountability #HakiZaKiraia #JFMdau2025