JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#BUNGENI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema Mwaka 2024/25 Tume ya Utumishi wa Walimu imepanga kutumia Tsh. Bilioni 20.74 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Maendeleo

Baadhi ya matumizi hayo ni kusimamia Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu kwa kuhakikisha wanasajiliwa, wanathibitishwa kazini na kwa wale wenye sifa wanapandishwa vyeo na kubadilishiwa kada kwa wakati, kusimamia Maadili na Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Utumishi wa Umma

Pia, kukamilisha utengenezaji wa Mfumo wa TSCMIS, usimikaji wa Miundombinu ya Mtandao wa Intaneti katika Ofisi 115 za Wilaya

Soma https://jamii.app/BungeniAprili16

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji24 #KutokaBungeni
1👍1
Wadau wa Jukwaa la Urembo, Mitindo na Utanashati (Lifestyle) ndani ya JamiiForums.com wamelalamikia kero ya Watu kunuka Jasho kali kutokana na kurudia kuvaa Nguo bila kufua

Wameshauri Nguo kuvaliwa mara moja na kufuliwa hasa Nguo za ndani na kwa Wakazi wa sehemu zenye Joto

Unakubaliana na ushauri wa Wadau?

Mjadala https://jamii.app/HarufuKurudiaNguo

#JamiiForums #JFChitchats #LifeStyle #Maisha #Hygene
👍3
Baadhi ya mijadala inayoendelea kwenye Jukwaa la Mapishi ndani ya JamiiForums.com

1. Kuboresha Mfumo wa Usagaji Chakula, kuongeza Nguvu, na kupunguza Uchovu wa Mwili ni miongoni mwa Faida za Matumizi ya Tende.

Kufahamu faida nyingine bofya https://jamii.app/MatumiziTende

2. Wadau wanajadili Vyakula vyenye Lishe wanavyopaswa kupewa Watoto kuanzia Miezi 6 hadi 12 ikiwemo Supu ya Maboga, Uji wa Lishe, Maziwa, na Matunda.

Kushiriki mada hii bofya https://jamii.app/PikaLisheMtoto

3. Mdau anaelezea namna ya kutumia Ndizi zilizoiva sana katika Mapishi badala ya kuzitupa.

Kuufikia mjadala huu bofya https://jamii.app/NdiziUsitupe
👍1
Katika usimamizi wa Matumizi Mwaka wa Fedha 2022/23, Ukaguzi wa CAG ulibaini Miradi Mitano iliyotekelezwa na TANESCO na mmoja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWASA) haikulipa fidia ya Tsh. Bilioni 13.69 kwa watu 567 walioathirika

Miradi Mitano inadaiwa Tsh.Bilioni 12.67 na Mradi wa Maendeleo ya Nishati ya Jua ya Tanzania ulikuwa na nyongeza ya makadirio ya deni la Tsh. Bilioni 1.02 kama fidia, licha ya kukaribia kukamilisha Miradi (97% hadi 100%)

Soma https://jamii.app/CAGMiradi24

#JamiiForums #RipotiYaCAG24 #RipotiUkaguziMiradi #Accountability #Governance
👍1
#UWAJIBIKAJI: Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeomba kutumia jumla ya Tsh. Trilioni 10.12 katika Mwaka wa Fedha 2024/25 ambapo Tsh. Trilioni 6.7 ni Matumizi ya Kawaida

Matumizi ya Kawaida yatajumuisha Mishahara ya Watumishi wa Makao Makuu Tsh. Bil. 10.92, Taasisi Tsh. Bil. 62.57, Utumishi wa Walimu Tsh. Bil. 9.85, Mikoa Tsh. Bil. 80.18, Halmashauri Tsh. Tril. 5.36 pamoja na Matumizi Mengineyo Tsh. 1,185,339,122,500

Aidha, TAMISEMI imepanga kutumia Tsh. Trilioni 3.41 kwaajili ya Miradi ya Maendeleo ya Makao Makuu, Taasisi mbalimbali, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Halmashauri

Soma https://jamii.app/BajetiTAMISEMI

#JamiiForums #Governance #Accountability #BajetiYaSerikali2024
👍3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIASA: Katibu Mkuu wa #CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekemea kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya Vijana wa chama hicho dhidi ya Wapinzani wao akieleza Chama kinapinga utaratibu huo

Akizungumza kutoka Jijini Mbeya katika Mkutano wa Hadhara, Dkt. Nchimbi amesema "Akiinuka Kijana wa CCM akasema Wapinzani wetu wakifanya hivi na hivi lazima tuwapoteze, huyu ni kijana wetu lakini kasema jambo la kijinga tutalipinga kwasababu nchi hii ni yetu sote."

Kauli ya Balozi Nchimbi inakuja muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa #UVCCM Mkoa wa #Kagera, Faris Buruhan, kusema Wakiwapoteza wanaowatusi Viongozi Mitandaoni, Jeshi la Polisi lisiwatafute

Soma https://jamii.app/BaloziNchimbi

#JamiiForums #JFDemokrasia #Governance #HumanRights
👍91
UEFA: MBIO ZA ARSENAL ZAISHIA ROBO FAINALI

Ndoto za Timu ya #Arsenal kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu ilipotokea Msimu wa 2005/06, zimefutika baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya #BayernMunich katika mchezo wa Pili wa Robo Fainali

Arsenal imeondolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya magoli 3-2 kwa kuwa mchezo wa kwanza matokeo yalikuwa sare ya magoli 2-2

#JFSports #JamiiForums #UEFAChampionsLeague
👍2
UEFA: REAL MADRID YAINGIA NUSU FAINALI KWA KUIPIGA MAN. CITY KWA PENATI

Mbabe wa soka la Ulaya, Timu ya #RealMadrid imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga #ManchesterCity kwa penati 4-3 baada ya sare ya goli 1-1 katika dakika 120, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa magoli 4-4

Real Madrid ambayo imetwaa taji la michuano hiyo mara 14, ilipata goli kupitia kwa Rodrygo (12) kisha Kevin De Bruyne akasawazisha (76), ikumbukwe kuwa mechi ya kwanza ya timu hizo ilimalizika kwa magoli 3-3 Jijini Madrid Nchini Uhispania

Baada ya matokeo hayo, Hatua ya Nusu Fainali itazikutanisha #PSG dhidi ya #BorrusiaDortmund, #BayernMunich dhidi ya Real Madrid

#JFSports #JamiiForums #UEFAChampionsLeague
👍2
Winston Churchill (1874 - 1965) aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, alitoa ujumbe huu katika mojawapo ya hotuba zake Kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia (1939 - 1945)

#JFQuotes #AmkaNaJF #GoodMorning #JFNukuu #LeaderShip #JamiiForums
👍5
Mdau wa JamiiForums.com ameshauri Viongozi kwenda 'field' kushughulikia changamoto za Wananchi badala ya kufanya Makongamano ya mara kwa mara

Amesema utaratibu wa kuwafikia Wananchi katika maeneo yao utasaidia kufikisha moja kwa moja ujumbe uliopangwa kuwasilishwa huku utatuzi wa kero zao ukiendelea badala ya kutumia Warsha

Unakubaliana na hoja za Mdau?

https://jamii.app/WarshaVsMaendeleo

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance
👍4
Baadhi ya mijadala inayoendelea kwenye Jukwaa la Sheria (The Legal Forum) ndani ya JamiiForums.com

1. Raia ana Haki ya kufahamishwa sababu ya kukamatwa kwake, Polisi kujitambulisha, na kupewa dhamana anapofikishwa Kituoni. Mdau ameeleza kuhusu Haki za Raia anapokamatwa na Askari Polisi

Kusoma zaidi bofya https://jamii.app/RaiaHakiPolisi

2. Mdau ameomba ushauri kuhusu eneo lake alilonunua lakini limepangiwa kutumika kama eneo la wazi bila kushirikishwa au kupewa taarifa na Halmashauri ya jiji.

Unaweza kumshauri hapa: https://jamii.app/EneoMatumizi

3. Wadau mbalimbali wametoa ushauri kwa mdau kuhusu hatua anazopaswa kuchukua baada ya mwajiri wake kushindwa kuwasilisha michango yake NSSF.

Kushiriki mjadala huu bofya https://jamii.app/MchangoNssf
👍41
#AFYA: Wataalamu wa Afya wanashauri kutumia Dawa kwa wakati kwasababu Tafiti mbalimbali zimebaini kama Dawa hazikutumiwa kwa wakati kwa mujibu wa Maelekezo ya Daktari, zinaweza kushindwa kutibu Maambukizi au Ugonjwa kikamilifu.

Hii husababisha Ugonjwa kupona kwa muda kisha kujirudia au kutotibika kabisa

Soma https://jamii.app/KuzingatiaDozi

#JamiiForums #AfyaBora2024 #PublicHealth #Maisha #LifeStyle
👍2
SIERRA LEONE: Wananchi katika Mji Mkuu wa Freetown, na Miji mingine wamelazimika kukaa gizani kwa Siku 7, baada ya Watoa Huduma ya Umeme kusitisha Huduma kutokana na kutolipwa kwa muda mrefu

Kampuni ya Kituruki ya #Karpowership inayosambaza sehemu kubwa ya Umeme wa #Freetown, imesimamisha Huduma zake kutokana na deni la karibu Dola Milioni 48 (Takriban Tsh. Bilioni 123.7) licha ya mara kwa mara Wizara ya Fedha kuahidi kulipa

Aidha, Muuzaji wa Umeme kutoka #IvoryCoast (CLSG) naye amepunguza Huduma katika Miji ya Kusini-Mashariki ya #Bo, #Kenema na #Koidu kutokana na malimbikizo ya deni. Haijulikani ni kiasi gani Serikali inadaiwa

Soma https://jamii.app/UmemeSierraLeone

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #Governance
👍2