JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ARUSHA: Diwani wa Kata ya #Sinoni, Michael Kivuyo amesema Wananchi wakishirikiana na Kikosi cha Uokozi wanashiriki zoezi la kutafuta Wanafunzi 7 ambao hawajulikani walipo baada ya Gari la Shule ya Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo, Asubuhi ya leo Aprili 12, 2024

Amesema “Waliokuwa kwenye gari ni Wanafunzi 11, Dereva na Matroni. Wanafunzi Watatu, Dereva na Matroni wameokolewa, mwili mmoja umepatikana, Wananchi wameingia mtoni, wengine wamepewa usafiri kufuata uelekeo wa mto ili kuwatafuta ambao hawajapatikana.”

Inadaiwa Dereva wa ‘School Bus’ alipofika eneo la tukio alionywa na Bodaboda kutopita wakimsisitiza kuwa kasi ya maji ni kubwa, akalazimisha kupita akiwaambia alipita hapo awali kabla ya kuwabeba Wanafunzi. Baada ya ajali na dereva kuokolewa, Bodaboda hao wakaanza kumshambulia kwa kumpiga, akaokolewa na Wasamaria wema

Soma https://jamii.app/GhatiMemorial

#JFMatukio #JamiiForums
👍91
#DEMOKRASIA: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni Taasisi isiyo Huru kwasababu Watendaji na Wateule wake Wanawajibika kwa Rais

Amesema "Waangalizi wa Uchaguzi tangu mwaka 1995 wamesema hivyo, Mtendaji Mkuu, Wajumbe na Watumishi wake wote ni Wateule wa Rais na kwa mujibu wa #Katiba yetu, Watumishi hao wanafanya kazi kwa niaba ya Rais ambaye ni mamlaka yao ya nidhamu"

Akizungumza kupitia #CloudsFM, Lissu ameongeza kuwa "Kwa mujibu wa Katiba, Tume ina uwezo wa kutengeneza Majimbo ya Uchaguzi kwa ridhaa ya Rais, kwa maana nyingine ni kwamba Rais asipotoa ridhaa, Tume haina uwezo wa kutengeneza Majimbo ya Uchaguzi"

Soma https://jamii.app/LissuTume

#JamiiForums #JFDemokrasia #Siasa #Governance #CivilRights
👍3
Mdau huyu kutoka Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ametoa ushuhuda kuhusu uraibu wa Kubeti ulivyomharibia mipango yake kwa kupoteza Fedha alizotarajia kuwekeza

Jambo gani limewahi kukupotezea Fedha zako ukaishia kujilaumu hadi leo?

Soma https://jamii.app/KubetiBalaa

#JamiiForums #StoriZaJF #Maisha #JFStories
👍6
#MICHEZO: Klabu ya Young Africans (#YangaSC) imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya Klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP). #Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa Mchezaji katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo

Kutokana na uamuzi huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia Klabu ya Yanga kufanya usajili kwa Wachezaji wa ndani.

Soma https://jamii.app/FIFAYangaAnnexe3

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Sports
😭8👍5
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com ameomba mamlaka husika kushughulikia kukosekana kwa Huduma ya Treni kutoka TAZARA hadi Kigogo Sokoni maarufu kwa jina la "Treni ya Mwakyembe" ambayo imesitisha safari zake kwa takriban wiki mbili na hivyo kuongeza adha ya usafiri kwa Wananchi kutokana na uchache wa usafiri mwingine wa Umma katika njia hiyo

Zaidi soma https://jamii.app/HudumaHakunaTreni

#JamiiForums #JFHuduma #SocialJustice #Accountability #ServiceDelivery
👍5
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Watumiaji wa Dawa za Kulevya nchini #SierraLeone watumia mabaki ya Mifupa ya Binadamu kutengeneza dawa za kulevya maarufu kama “Kush”

Hali hii imepelekea Rais wa nchi hiyo kutangaza rasmi kuwa #DawaZaKulevya ni Janga la Taifa

#JamiiForums
👍3
DAR: Serikali imesema Mradi wa Bonde la Msimbazi utaanza Aprili 15, 2024 ambapo utaanza kwa Ubomoaji wa Nyumba katika eneo la Jangwani zilizopo kando ya Mto Msimbazi

Mradi huo utasimamiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (#TARURA) ambapo taarifa imeeleza hadi kufikia Februari 29, 2024 ilikuwa imelipa Fidia ya Tsh. Bilioni 52.61 kwa wamiliki wa nyumba 2,155 kati ya 2,329

Mradi huo unatarajiwa kuchukua Miaka 5 na utagharimu Dola za Marekani Milioni 260 (Tsh. Bilioni 675) kwa kujenga Karakana mpya ya Mabasi ya Mwendokasi eneo la Ubungo Maziwa na Miundombinu ya Kuzuia Mafuriko

Soma https://jamii.app/NewJangwani

#JamiiForums #JFHuduma #Governance #Accountability #ServiceDelivery
3👍1
Nini Mtazamo wako kuhusu kubadilishwa kwa jina la Tume ya Uchaguzi kuwa Tume huru ya Uchaguzi?

Mjadala zaidi https://jamii.app/JinaTumeUchaguzi

#JamiiForums #Governance #CivilRights #Democracy
😁2
Unamshauri Mdau achukue uamuzi gani kuhusu masomo yake?

Kwa mjadala zaidi tembelea Jukwaa la Elimu ndani ya JamiiForums.com

#JamiiForums #JFStories #Maisha #JFHakiElimu
👍5