JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com kutoka eneo la Goba Matosa, Dar es Salaam ameomba Mamlaka husika kushughulikia kero ya ubovu wa Barabara ya Kawawa inayoanzia Msikiti wa Mzaramuni hadi Bondeni kwasababu inawapa usumbufu Wakazi wa eneo hilo

Zaidi soma https://jamii.app/BarabaraMatosa

#JamiiForums #JFHuduma #SocialJustice #Accountability #ServiceDelivery
#JFMDAU: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa #Mbeya ameomba mamlaka husika ishughulikie changamoto ya Huduma ya Maji katika baadhi ya maeneo ya Mbeya, akidai uhaba wa maji ya bomba unasababisha Wakazi wa Mkoa huo kutegemea maji ya mvua na visima ambayo si salama kwa #Afya

Zaidi soma https://jamii.app/MbeyaKeroMaji

#JamiiForums #JFHuduma #SocialJustice #Accountability #ServiceDelivery
πŸ‘7❀2
Bondia #KarimMandonga amepoteza pambano dhidi ya Mada Maugo kwa kupigwa katika Raundi ya 6 kwa TKO kwenye pambano lililofanyika Mkoani Morogoro

Ngumi iliyopigwa kwenye kidevu katika pambano hilo la Raundi 6 ilimfanya Mandonga apoteze mwelekeo, ndipo mwamuzi Pendo Njau akaingilia na kumaliza pambano

Baada ya pambano, Maugo amesema β€œMwalimu wangu ambaye ni mke wangu aliniambia niwe na utulivu ulingoni, hilo nimelitimiza, nikikutana na Mandonga popote pale bado nitampiga tena.”

Upande wa Mandonga amesema β€œMaugo hawezi kunisumbua, ni mchezo tu, uwezo wa kunipiga hana.”

Soma https://jamii.app/MandongaApigwa

#JFSports #JamiiForums
πŸ‘9😁4πŸ”₯1
#MALI: Serikali ya Kijeshi imepiga Marufuku Vyombo vya Habari kuripoti Matukio ya Vyama vya #Siasa na Mashirika ya baada ya kusitisha Shughuli zote za Kisiasa Nchini humo hadi pale itakapoamuriwa tena ikidaiwa ni kwa ajili ya kulinda Utulivu wa Umma

Amri hiyo imetolewa baada ya Vyama zaidi 80 vya Kisiasa na Mashirika ya Kiraia kutoa taarifa ya pamoja Aprili Mosi, 2024 wakitaka ufanyike #Uchaguzi wa Rais haraka iwezekanavyo ili kuondoa Utawala wa Kijeshi

Imeelezwa vitendo vya Uasi vinavyoendeshwa na Vyama vya Siasa na washirika wake vinaongezeka

Soma https://jamii.app/MaliBanPolitics

#JamiiForums #Governance #CivilRights #HumanRights #Democracy #PressFreedom
❀3πŸ‘3
#TABORA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Wananchi wameshafikisha malalamiko yao kwa Mamlaka husika kuhusu Shule ya Msingi Kiswahilini kukosa Huduma muhimu lakini hakuna msaada wala majibu yoyote yanayotolewa ukizingatia Shule ni mpya

Soma zaidi https://jamii.app/HudumaKiswahilini

#Governance #JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFHakiElimu
πŸ‘2❀1
#SHINYANGA: Kituo cha Afya cha Mwalugulu kilichopo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama kimebainika kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Vifaa baada ya kununua na kutumia Majokofu ya nyumbani katika kuhifadhi Damu

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume aliyefanya ukaguzi kituoni hapo amesema β€œWataalamu wametuthibitishia haya sio Majokofu ya Damu, huyu Mzabuni tumemlipa bila kukagua, tumeagiza Majokofu ya kutunzia Damu tumeletewa majokofu ya Matunda.”

Aidha, Dkt. Mfaume ameagiza kuondolewa kwa Mfamasia wa Halmashauri kwa kutoa taarifa ya uongo wakati wa ukaguzi pamoja na Wajumbe wa Usimamizi wa Shughuli za Afya kituoni hapo kuonywa kwa Barua

Soma https://jamii.app/BloodFreezer

#JamiiForums #JFAfya #Governance #Accountability #PublicHealth #JFHuduma
πŸ‘1
ARUSHA: Wanafunzi Saba wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la Shule ya Msingi Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji Mitaa ya Dampo, Sinoni

Inadaiwa chanzo ni dereva kushindwa kulidhibiti gari kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, taarifa kutoka eneo la tukio zinadai Wanafunzi Watatu wameokolewa na mwili mmoja umepatikana, Dereva wa gari naye ameokolewa na yupo chini ya ulinzi

JamiiForums ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema β€œNipo kwenye msafara, ila hizo taarifa nimezipata, kikosi cha Uokozi kipo eneo la tukio na Wanafunzi saba hawajulikani walipo wengine wameokolewa, taarifa kamili tutaitoa baadaye.”

Soma https://jamii.app/GhatiMemorial

#JFMatukio #JamiiForums
😭4πŸ‘3❀2
Wadau mbalimbali ya JamiiForums.com wanataja mambo waliyojifunza Kimaisha wakiwa kwenye Umri wa Miaka 20 mpaka 30

Nawe ulijifunza jambo gani katika Umri huu ambalo unatamani wengine wajifunze mapema?

Mjadala https://jamii.app/NiliyojifunzaMiaka20

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #LifeLessons