JamiiForums
โœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#JFAFYA: Sigara huzalisha Kemikali za uraibu (Nicotine) zinazodhuru Mifumo ya Mwili wa Binadamu ikiwemo ya Damu, Moyo na Upumuaji

Pia, huzalisha Kemikali Sumu Mwilini kama Hydrogen Cyanide, Lead, Arsenic, Ammonia na Carbon Monoxide

Soma https://jamii.app/SmokingTips

#JFAfyaJamii
๐Ÿ‘5
4% YA WATANZANIA WANA MATATIZO YA MACHO

Pamoja na takwimu hizo imeelezwa 90% ya matatizo hayo yanatibika

Takwimu za Mwaka 2020 zilionesha Watu milioni 1.2 tu ndio waliofikiwa na Huduma ya Macho ikilinganishwa na uhitaji wa takriban Watu milioni 12

Soma https://jamii.app/MachoTakwimu

#JFAfya
๐Ÿ‘5
DAR: Walimu 14 wanashikiliwa wakituhumiwa kukiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za mitihani ya Darasa la 7 iliyofanyika Oktoba 5 na 6, 2022

Uchunguzi wa suala hili unaendelea na Taarifa zitatolewa na Mamlaka zinazohusika na Masuala ya Elimu

Soma https://jamii.app/WalimuWakamatwa

#KemeaRushwa
๐Ÿ‘13๐Ÿค”1
UGANDA: WAPINGA SHERIA MPYA YA MITANDAO YA KIJAMII

Kampuni kadhaa za Mtandaoni na Wanaharakati 12 wameungana kufungua kesi wakidai Sheria inaminya Uhuru na Haki za matumizi ya Mitandao na itatumika kuwanyamazisha wakosoaji wa Serikali

Soma https://jamii.app/SheriaUG

#DigitalRights
๐Ÿ‘6
ARUSHA: WATUMISHI WATAKIWA KUJILINDA NA UHALIFU WA MITANDAONI

Hii ni kutokana na Vifaa na Mifumo ya TEHAMA ambayo hutumika kupitisha #TaarifaBinafsi au za Taasisi kushambuliwa zaidi na Wahalifu wa Mtandaoni kwa njia mbalimbali

Soma https://jamii.app/UhalifuMtandaoni

#DigitalSecurity
๐Ÿ‘11
Ikiwa hata leo Watu wanaoishi katika Umasikini wanadhulumiwa Utu wao na Kudharauliwa ni jukumu la kila Mmoja Kutambua kuwa, Utu wa Mwanadamu sio tu ni #Haki ya Kimsingi bali ni Msingi wa Haki zingine zote za Msingi

Soma https://jamii.app/IDOEP2022

#EndPoverty
๐Ÿ‘9
ASTON VILLA YAMUWANIA POCHETTINO

Inadaiwa #AstonVilla inaweza kumuajiri Kocha Mauricio Pochettino achukue nafasi ya Steven Gerrard anayeweza kufukuzwa kutokana na matokeo mabaya, akishinda mechi 2 kati ya 10 za Premier League msimu huu

Soma https://jamii.app/AstonVilla

#JFSports
๐Ÿ‘4
UTAFITI TAKUKURU: Kuhusiana na muda uliotumika kupata Huduma katika Vituo vya Huduma, Sekta ya Elimu ilipata alama ya juu zaidi kwa asilimia 90.5 ikifuatiwa na Sekta ya Ulinzi/Usalama kwa asilimia 68.3 na Huduma za Umeme kwa asilimia 66

Kwa ujumla, huduma zote zilitolewa kwa wakati isipokuwa huduma za Ugani, NIDA na TASAF ambao walipata asilimia 46, asilimia 47 na asilimia 41 mtawalia.

#JamiiForums #KemeaRushwa
๐Ÿ‘4๐Ÿค”1
ATHARI ZA MOSHI WA SIGARA KWA WAJAWAZITO

Huongeza nafasi ya kuharibika kwa Ujauzito, Kujifungua kabla ya wakati, Kujifungua Watoto wenye tatizo la Mdomo Sungura, Wenye uzito Mdogo na walio na Matatizo kwenye Mapafu

Pia, Baadhi ya Watoto hufariki Siku chache baada ya kuzaliwa

Soma https://jamii.app/SmokingTips

#JFAfyaJamii
๐Ÿ‘5๐Ÿ˜ฑ1
Wataalamu wa Saikolojia, Wanasheria na Viongozi wa Dini wanakiri kuongezeka kwa maombi ya Talaka na wanaonya kuwa hali hiyo inahatarisha mustakabali wa Taifa ikizingatiwa kuwa Watoto wanapoteza Haki ya Malezi Bora ya pande mbili

Mdau anahoji kwanini Ndoa zimekuwa chanzo cha mashauri mengi kwenye Idara za Haki ikiwemo Mashitaka ya Unyanyasaji na Madai ya Kugawana Mali baada ya Wanandoa kushindwana

Soma https://jamii.app/TalakaNdoa

#JFMaisha #Malezi #Mahusiano
๐Ÿค”7๐Ÿ‘4
Uchambuzi wa hoja za CAG unaonesha, pamoja na kupata Hati Safi, Taasisi nyingi za Umma bado zina kasoro za Kiutendaji. Hivyo zinahitaji kufuatiliwa ili kudhibiti uwezekano wa kuwepo kwa Rushwa na Ubadhirifu wa Rasilimali za Umma

Mfano, Bohari Kuu ya Dawa ilipata Hati Safi ilihali ilifanya malipo ya awali kiasi cha Shilingi Bilioni 14.89 kwa Wazabuni watano bila Mikataba au makubaliano yoyote ambayo yanabainisha Misingi ya malipo hayo.

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #Wajibu
๐Ÿ‘11๐Ÿ‘1
MDAU: KWA NINI UKIMKATAA MWANAMKE KIMAHUSIANO ANAKUWA NA CHUKI KALI DHIDI YAKO?

Anasema haelewi sababu za Mwanamke kuwa na chuki sana akikataliwa hata kama sababu za kumkataa zinamashiko

Ameomba mwongozo wa namna ya kukabiliana na hali kama hii mnapokuwa eneo moja la kazi

Soma https://jamii.app/ChukiKukataliwa

#JFMaisha
๐Ÿ‘5โค2
UTAFITI TAKUKURU: Asilimia 35.6 ya Wahojiwa walisema Kampeni za Uhamasishaji wa Umma kupinga Ufisadi/Rushwa zinatosha huku asilimia 55.6 wakisema hazitoshi

Asilimia 88.8 walisema wapo tayari kushiriki kwenye Mapambano dhidi ya Rushwa/Ufisadi na Asilimia 81.8 waliona kuna Ushirikishwaji mkubwa wa Wanawake kwenye kupinga Rushwa

#KemeaRushwa #JamiiForums
๐Ÿ‘3
MDAU: UCHAGUZI WA MASOMO UANZIE KIDATO CHA KWANZA

Anashauri Elimu ya awali ya Sekondari iwe lazima kwa wahitimu wa Darasa la 7 ili wanapoanza Masomo wawe na nafasi ya kuchagua mchepuo wa Masomo ili kupunguza mzigo wa kusoma vitu vingi

Soma https://jamii.app/UshauriWaElimu

#HakiMtoto
๐Ÿ‘33๐Ÿ‘Ž3๐Ÿ‘Œ2๐ŸŒš2
RAIS SAMIA: Maendeleo sasa yanafanywa kwa Wananchi, kelele zitahamia upande mwingine

Na bahati nzuri hata upande mwingine ule wa Kisiasa nimewapa kazi wenyewe wakutane, Wazungumze watuletee tuone yale yanayotekelezeka, tukubaliane nao, tuyatekeleze kwa harakaโ€

Soma https://jamii.app/SamiaInKigoma

#Democracy
๐Ÿคฏ5๐Ÿ‘3๐Ÿค”3๐Ÿ‘Ž2๐Ÿ˜1
KOMBE LA DUNIA: SERENGETI GIRLS YATINGA ROBO FAINALI

Timu ya Taifa ya Wanawake U17 Serengeti Girls imefikisha pointi 4 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Canada Nchini India

Serengeti Girls imeungana na Japan kutoka Kundi D kusonga mbele

Soma https://jamii.app/TZU17Girls

#JFSports
๐Ÿ‘31๐Ÿ‘7๐Ÿฅฐ4๐Ÿ”ฅ3๐Ÿ‘Œ3โค2
ZITTO KABWE: Hakuna njia nyingine yoyote ya kuifanya Nchi yetu iende mbele isipokuwa njia hii unayopita (Rais Samia) ya Kujenga Maridhiano ya Kitaifa

Nikiwa Kiongozi wa Kitaifa, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa juhudi za kuwaweka Watanzania pamoja

Soma https://jamii.app/SamiaInKigoma

#Democracy
๐Ÿค”8๐Ÿ˜ข3๐Ÿ‘2๐Ÿ‘2๐Ÿคฎ2
UTANASHATI: Kuna sehemu kadhaa unaweza kupaka au kupulizia Manukato (Perfume). Ila katika hizi sehemu zote unapaswa kuchagua sehemu tatu za kupulizia

Si vyema kupulizia sehemu nyingi sana. Pulizia kwa kiasi tu, 'Perfume' nyingi sana kwa wakati mmoja sio nzuri na huweza kuwaumiza wanaokuzunguka

#JamiiForums #Maisha
๐Ÿ‘11
Nโ€™GOLO KANTE NJE MIEZI MINNE, KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Kiungo huyo wa #Chelsea na #Ufaransa amefanyiwa Upasuaji wa Nyama za Paja hivyo atakuwa nje ya Uwanja kwa muda wa Miezi minne

Kante (31) aliumia katika Mechi dhidi ya #Tottenham, Agosti 14, 2022

Soma https://jamii.app/KanteOut

#JFSports
๐Ÿค”7๐Ÿ‘2
DRC: Hali ya Sintofahamu imejitokeza baada ya Rais Fรฉlix Tshisekedi kumteua Jenerali Floribert Kisembo Bahemuka aliyefariki mnamo Mwaka 2011

Pia, alimteua Jenerali John Tshibangu aliyetoroka Jeshini Mwaka 2011 kwa uasi

Soma https://jamii.app/TeuziDRC

#Governance
๐Ÿ˜13๐Ÿคฏ5๐Ÿ”ฅ2๐Ÿ‘1