JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MATUMIZI MAKUBWA YA CHUMVI NI HATARI KWA AFYA YA MOYO

Chumvi mbichi inayoongezwa baada ya chakula kuiva ikitumika kwa wingi inaweza kusababisha shinikizo la juu la Damu ambalo moja ya madhara yake ni kutanuka kwa Moyo

Pia, Juisi za kusindika au kuongeza Sukari pindi unapotengeneza pamoja na kula kwa wingi Vyakula vya Wanga ni hatari kwa Moyo

Soma https://jamii.app/ElimuAfya

#JFAfya
πŸ‘17
NDONDI: IBRAHIM CLASS AMPIGA RAIA WA MEXICO KWA KO RAUNDI YA 9

Bondia Mtanzania Ibrahim Class amefanikiwa kushinda dhidi ya Alan Pina kutoka Mexico katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika Mlimani City, Dar es Salaam

Baada ya kuonesha upinzani mkali kuanzia raundi ya kwanza, Pina alipigwa ngumi mbili kali raundi ya 9 zilizomuangusha chini na kulazimika kupewa huduma ya kwanza ulingoni baada ya kuonekana kutojitambua kwa muda

#JFSports
πŸ‘21πŸ‘4
BURKINA FASO: Kapteni Ibrahim Traore ametangaza Mapinduzi ya kumuondoa Madarakani Kiongozi wa Kijeshi, Paul-Henri Damiba, kuvunja Serikali, kusimamisha Katiba na kuweka Katiba ya mpito

> Ni Mapinduzi ya pili ya Kijeshi ndani ya Miezi 8

Soma https://jamii.app/UostersBF

#Democracy
😁14πŸ”₯4πŸ‘4😒3πŸ‘2
MAREKANI: WATU 45 WAFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA KIMBUNGA IAN

Kimbunga hicho kinachoanza kutoweka kimeharibu takriban Nyumba 80,000 katika Mji wa Fort Mayers, na kuwaacha gizani zaidi ya Watu Milioni 1.8 kwenye Jiji la #Florida

Soma https://jamii.app/IANUSA

#Ian #JFMatukio
πŸ‘5
OKTOBA MOSI: SIKU YA WAZEE DUNIANI

Siku hii ni maalum kwa ajili ya kupinga Dhana na Imani potofu kuhusu Wazee na Uzee, na kutambua umuhimu na mchango wao katika Jamii

Kauli Mbiu ya Mwaka huu inalenga kuleta mwanga katika Suala la Wazee wasiofaidika kikamilifu na Maendeleo ya Kidijitali

Soma https://jamii.app/SikuWazeeDuniani

#UNIOPD2022
πŸ‘9❀3πŸ”₯1
TANZIA: DAKTARI MTANZANIA AFARIKI DUNIA KWA EBOLA

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amethibitisha kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Mohamed Ali (37) aliyefariki nchini Uganda baada ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ebola Septemba 26, 2022.

Waziri wa Afya Nchini Uganda aliripoti kifo cha Dkt. Mohammed aliyekuwa akipatawa matibabu katika Hospitali ya Fort Portal RRH kupitia Twitter

Zaidi https://jamii.app/DktAliDies

#JamiiForums #PublicHealth
😒12πŸ‘3❀1πŸ‘Ž1
RIPOTI: #TANZANIA NI NCHI YA PILI KWA KUAMINI USHIRIKINA AFRIKA

Ripoti ya Kitengo cha Utafiti cha Kituo cha Sheria na #HakiZaBinadamu, imeonesha hali hiyo inatokana na matukio ya Imani za Kishirikina ikiwemo Mauaji ya Wazee 117 kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Mei 2018

> Mkoa wa Tabora umeongoza kwa matukio mengi huku #Cameroon ikiwa nafasi ya kwanza Afrika.

Soma https://jamii.app/UchawiTZ

#HumanRights
😁14πŸ‘9πŸ€”5🀑3🀯2
#EBOLA: Ni Ugonjwa utokanao na Kirusi cha Ebola na ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kwa mara ya kwanza Ugonjwa huu ulibainika Mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (#DRC) na #Sudan

Chanzo hasa bado hakipo bayana lakini Popo aina ya #Pteropodidae wanaonekana kuwa wabebaji wa Kirusi hicho

#JamiiForums #EbolaOutbreak #PublicHealth
πŸ‘7
ARUSHA: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA WAMAASAI KUHAMISHWA LOLIONDO

Hakimu Charles Nyachae amesema walalamikaji ambao ni Wafugaji wa Jamii ya Kimasai walishindwa kuthibitisha madai yao kuwa waliteswa na kuondolewa kinguvu

Wamasai waliiomba Mahakama Kuzuia Kufukuzwa, Kukamatwa, Kuwekwa Kizuizini au Kuteswa na kutaka fidia ya Tsh. Bilioni 1 kwa walioathirika na uhamishaji huo

Soma https://jamii.app/Maasaicase

#HumanRights
πŸ‘4
NI WAJIBU WETU KUHAKIKISHA WAZEE WANAISHI KWA AMANI NA FURAHA

Idadi kubwa ya Wazee wanapitia changamoto za Kiafya, ni wakati huu ambapo wanahitaji Matunzo na Faraja ili kuishi Maisha yenye Furaha bila Wasiwasi wala Huzuni

Ukosefu wa ufafanuzi kuhusu Mabadiliko ya tabia kwa Wazee, unaweza kusababisha kunyanyaswa na Watu wao wa karibu

Soma https://jamii.app/MatunzoWazee

#UNIOPD2022
πŸ‘4
#KENYA: Raila Odinga aliyegombea Urais mara 5 na kushindwa, amesema ameamua kukubali matokeo bila kuitisha maandamano ili kuepuka kushitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kama kungetokea Machafuko

Zaidi https://jamii.app/RailaConcede

#Democracy #Elections
😁16πŸ‘8πŸ”₯2
KUTEMBEA HATUA 10,000 KWA SIKU NI NZURI KWA #AFYA YA MOYO

Kuacha Uvutaji wa Sigara, Unywaji Pombe uliokithiri na kula vyakula bora kunasaidia kujikinga na Magonjwa ya Moyo

32% ya vifo Duniani vinatokana na Magonjwa yasiyoambukiza hususani Moyo

Soma: https://jamii.app/ElimuAfya

#JFAfya
πŸ‘17πŸ‘Ž1
ALIYEMGONGA TWIGA FAINI TSH. MILIONI 34.9

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ignas Gara amesema dereva huyo wa Lori anatakiwa kulipa faini baada ya Twiga kufariki

> Kwa sasa dereva anatibiwa chini ya ulinzi wa Polisi

Soma: https://jamii.app/KuuaTwiga

#Governance
πŸ‘6πŸ‘Ž3
RUSHWA YA NGONO: MFUMO WA KULINDA WATOA TAARIFA UIMARISHWE

Kulindana na Ukosefu wa Uwazi katika Mifumo kunatajwa kuwa chanzo cha uvujaji na vitisho kwa Watoa Taarifa dhidi ya Wahadhiri au Watumishi wa Vyuo wenye Mamlaka

Utafiti uliohusisha Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma (2020) umebaini baadhi ya waliojitolea kutoa Taarifa walipata vitisho vya kuhatarisha Kazi, Taaluma na Maisha yao

#VunjaUkimya
πŸ‘8
NAMNA BORA ZA UTUNZAJI WA MISWAKI

Usifunike Mswaki wako baada ya kuutumia, wala kusafisha kwa β€˜Sanitizer’, β€˜Spirit’, Kemikali zozote kali au kwa kutumia mionzi ili kuua bakteria

Safisha mswaki kwa maji tiririka, kisha uhifadhi kwa kuusimanisha pia usitumie Mswaki wa mtu mwingine

Soma https://jamii.app/ToothbrushCareTips

#JFAfya
πŸ‘15
JEBRA KAMBOLE: TUTAKATA RUFAA KESI YA KUONDOLEWA WAFUGAJI LOLIONDO

Amesema kesi iliyotolewa uamuzi na EACJ ni ya "Uvamizi wa Serikali" wa 2017, haihusiani na "Mateso ya Wamasai" ya Juni 2022 ambayo bado ipo Mahakamani

Soma https://jamii.app/JebraRufaa

#Uwajibikaji #SocialJustice
πŸ‘14πŸ‘2😁1
KUPATA TAARIFA MTANDAONI: Kila Mtu ana Haki ya kutafuta na kupokea Taarifa kupitia Mtandao

Wananchi wana Haki ya kupata na kutumia ipasavyo Taarifa za Serikali ambazo zinatakiwa kutolewa kwa wakati husika na kwa namna ambayo wengi watazifikia

#RightToInformation
πŸ‘7
#INDONESIA: Watu 174 wamefariki na takriban 180 wamejeruhiwa kwenye vurugu zilizotokea ktk Uwanja wa Mpira baada ya Arema FC kufungwa 3-2 na Persebaya Surabaya

#FIFA imesema Polisi hawakutakiwa kutumia mabomu ya Machozi katika vurugu hizo

Soma https://jamii.app/129Indonesia

#JFSports
😒7πŸ‘6πŸ€”3😱2πŸ‘Ž1
MOSHI: PADRI ANAYEDAIWA KUBAKA ATAKIWA KURUDI KWA WAZAZI WAKE

Padri Sosthenes Bahati Soka (41) amefukuzwa kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya kubaka Watoto 3

Maamuzi hayo yamezingatia Sheria ya Kanisa namba 1,722 inayotaka Mtuhumiwa kutengwa

Soma https://jamii.app/PadriSoka

#HakiMtoto
πŸ‘10
ENGLAND: MAKOCHA WAANZA KUPINGA VAR

Baadhi yao wanataka VAR ifikiriwe upya kwa kuwa waamuzi wameendelea kufanya makosa

Waliolalamika ni Kocha wa Tottenham (Conte), Kocha wa Fulham (Silva) na Mwenyekiti wa Crystal Palace (Parish)

Soma: https://jamii.app/EnglandVAR

#JFSports
πŸ‘13