JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
INDONESIA: WATU ZAIDI YA 600 WAHAMISHWA KUTOKANA NA HATARI YA VOLKANO

> Shirika la Kijeolojia la #Indonesia limeonya kuhusu hatari ya Mlipuko wa Volkano ktk Mlima #Merapi

> Mlipuko wa mwisho ulitokea 2010 ambapo zaidi ya watu 300 walifariki

Soma https://jamii.app/MerapiEruption
UNICEF: WATOTO MILIONI 140 WATAZALIWA 2021

- Kwa Januari 1, 2021 Watoto zaidi ya 371,504 walizaliwa Duniani

- Zaidi ya nusu yao walizaliwa India, China, #Nigeria, Pakistan, #Indonesia, Ethiopia, Marekani, Misri, #Bangladesh, na DRC

Soma - https://jamii.app/NewBabies2021
#ChildSafety
KAMPUNI YA BOEING KULIPA FAINI TSH. TRILIONI 5.7

> Italipa faini kwa kosa la kuficha Taarifa za Kiusalama za Ndege za 737 Max, zilipelekea ajali #Ethiopia na #Indonesia na kuua watu 346

> Sehemu ya pesa hiyo ni fidia kwa familia zilizoathirika

Soma https://jamii.app/BoeingFined
#INDONESIA: WANAWAKE WASIO BIKRA WARUHUSIWA KUJIUNGA NA JESHI

Kwa miaka mingi ili Mwanamke ajiunge na Jeshi la Nchi hiyo alifanyiwa vipimo ikiwemo kuingizwa vidole sehemu za Siri

Vipimo hivyo vinahesabika kuwa uyanyasaji wa kijinsia

Soma https://jamii.app/NonVirginArmy

#WomenRights
#INDONESIA: Watu 174 wamefariki na takriban 180 wamejeruhiwa kwenye vurugu zilizotokea ktk Uwanja wa Mpira baada ya Arema FC kufungwa 3-2 na Persebaya Surabaya

#FIFA imesema Polisi hawakutakiwa kutumia mabomu ya Machozi katika vurugu hizo

Soma https://jamii.app/129Indonesia

#JFSports
😢7👍6🤔3😱2👎1
#Indonesia imesitisha uuzaji wa Dawa za Kutibu kifua kufuatia vifo vya Watoto 99 huku kukiwa na visa 206 vya majeraha ya papohapo ya Figo kwa Watoto

Dawa hizo ni #Promethazine Oral solution, Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold syrup

Soma https://jamii.app/DawaMaumivuFigo

#JFAfya
👍6
FIFA YAIONDOA INDONESIA KUWA MWENYEJI WA KOMBE LA DUNIA U20

#FIFA imeamua hivyo baada ya Serikali ya #Indonesia kukataa kuipokea Timu ya #Israel kutokana na Mgogoro wa Kidiplomasia baina ya Mataifa hayo

Michuano imepangwa kufanyika Mei 20 - Juni 11, 2023, FIFA itatangaza Nchi mwenyeji hivi karibuni

Soma https://jamii.app/WorldCupU20

#JFSports #Diplomasia #U20WorldCup
👍81👎1🔥1
#JFDATA: Tangu Mwaka 1990 - 2022, Nchi nne zilizotajwa kuwa na Watu wengi zaidi ni China (Bilioni 1.42), India (Bilioni 1.41), Marekani (Milioni 337) na #Indonesia (Milioni 275)

Hata hivyo, #India inakadiriwa kuwa Nchi yenye watu wengi zaidi kufikia 2050 ikifuatiwa na China, Marekani na #Nigeria inayotarajiwa kuwa na Watu Milioni 375

Zaidi, soma https://jamii.app/WPP2022

#JamiiForums
3👍2
KENYA: Baada ya kuhusishwa katika kashfa ya Uagizaji wa tani 125,000 za Mafuta ya kula bila ushuru, kuuzia Wafanyabiashara wa jumla, na kuikosesha Serikali mapato ya Ksh. Bilioni 6, sawa na takriban Tsh. Bilioni 102.3, Azimio la Umoja limemtaka Waziri wa Biashara ajiuzulu

Ushahidi zaidi ulionyesha baadae Shirika la Kitaifa la Biashara la Kenya (#KNTC) lilinunua Mafuta kutoka kwa Wafanyabiashara hao, badala ya kuagiza moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji Nchini #Malaysia au #Indonesia na kuuzia Wananchi

Soma https://jamii.app/MosesKuriaKujiuzulu

#Accountability #Governance
👍4
INDONESIA: Rais #SamiaSuluhuHassan amewasili Nchini #Indonesia kwa ajili ya ziara ya Januari 24 na 25, 2024 ambayo imetokana na mwaliko wa mwenyeji wake, Rais #JokoWidodo ambaye alifanya ziara Nchini Tanzania, Agosti 2023

Rais Samia amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Pahala Nugraha Mansury kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang Jijini Jakarta

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, January Makamba alisema lengo la ziara ni kukuza uhusiano wa Kidiplomasia, kuibua fursa za uwekezaji zitakazowanufaisha Wananchi wa Tanzania na kusaini Hati kadhaa za Makubaliano ikiwemo Sekta ya Nishati na Afya

Soma https://jamii.app/SamiaIndonesia

#Diplomacy #Governance #TanzaniaIndonesia #JamiiForums
👍3