JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa ikoje Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto unaoendelea sasa kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

Ungana nasi - https://twitter.com/i/spaces/1gqGvyLLPEwKB
πŸ‘3
DKT. FAT-HIYA: Satarani inaongoza kwa vifo hapa Tanzania na Duniani kote, kwa Muhimbili ni kama Wagonjwa 800 kwa Mwaka wanaogundulika

Tatizo kubwa ni kuwa Wagonjwa wengi wanakuja kwenye Matibabu wakati ambao Ugonjwa unakuwa umeenea sehemu kubwa, na inakuwa vigumu kutibu kwa wakati huo

Saratani ya Figo ndiyo inaongoza kwa umri wa Miaka 3-4, na Saratani ya Matezi inafuata kwa Watoto chini ya Miaka 10. Pia, kuna Saratani za Ini na Misuli.

#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘8
DKT. FAT-HIYA: Dalili zinazoonekana sana ni Uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Huendelea kwa kufanya Watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana Mishipa ya Mwili na Utumbo

Pia, Mtoto anaweza kuanza kukosa choo vizuri, kukojoa Damu, au kuishiwa Damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya Saratani

Wakati mwingine Homa pia huonekana, Homa hizi huwa hazisikii matibabu ya kawaida tunayoyafahamu. Tumbo linaweza kujaa, Maji kujaa kwenye Mapafu, Mtoto hakui vizuri na anaweza kupata changamoto za Upumuaji.

#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘3
DKT. SHAKILU JUMANNE: Mzazi anapokuwa anamuogesha Mtoto awe na kawaida ya kumchunguza, Mfano kumminya sehemu ya Tumboni au pembeni ya Tumbo, ukibaini kuna uvimbe mfikishe Hospitali mapema

Kuna kesi nyingi zinatokea Wazazi wanakuja tayari tatizo limekuwa kubwa, ukiwauliza wanasema waliona wakajua ni Uvimbe wa kawaida na utaisha.

#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘7
DKT. FAT-HIYA: Kuna madhara makubwa ya kuwatibu Watoto bila kujua chanzo sahihi cha Ugonjwa, Matibabu tofauti husababisha Saratani kuongezeka

Baadhi ya Wazazi hutumia Dawa za Asili ambazo wanadhani hazina Kemikali. Dawa hizi hazina Dozi kamili na zina Kemikali nyingi, zinaweza kusababisha kufeli kwa Figo na Maini.

#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘6
DKT: SHAKILU: Watoto wengi hupata Saratani kwa sababu ambazo nyingi hazijulikani, lakini chanzo kikuu ni mgawanyiko ya mabadiliko ya Vinasaba
-
Asilimia ndogo sana ya Saratani hutokana na kurithi, pia Watoto wenye VVU wanahatari kubwa ya Kupata aina fulani za Saratani.
-
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘4
DKT. SHAKILU: Sumu Kuvu inatokana na namna ya uhifadhi wa Nafaka baada ya Mavuno. Mfano Karanga na Maharage

Hakuna uhusiano wa Sumu Kuvu na Saratani ya Watoto, Sumu Kuvu husababisha Saratani ya Ini kwa Watu wazima.

Mjadala - https://twitter.com/i/spaces/1eaKbrkkmpQKX

#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
πŸ‘8
TABORA: Watumishi 4 wa Chuo cha VETA waliohusika na ujenzi wa Kibanda cha Mlinzi kwa Tsh. Milioni 11, wamepandishwa Kizimbani wakishtakiwa kwa Matumizi Mabaya ya Mamlaka na Kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Milioni 22.8

Soma - https://jamii.app/Kibanda11

#KemeaRushwa
πŸ‘10πŸ€”4
MARA: MBARONI AKIDAIWA KUMBAKA BINTI ALIYEPOOZA

Juma Ligamba (45) mkazi wa Kijiji cha Kibubwa anatuhumiwa kufanya Ukatili huo kwa Binti (19) ambaye amepooza sehemu kubwa ya Mwili wake tangu akiwa na Wiki tatu baada ya Kuzaliwa

Soma - https://jamii.app/UkatiliMara

#DomesticViolence
😒3πŸ‘2πŸ‘Ž1πŸ€”1
SAUDI ARABIA: Balozi wa #Tanzania Nchini humo, Ali Jabir Mwadini, amesema hakuna Utaratibu unaowatambua Watanzania wanaofanya Kazi za Ndani

> Amesema wanaofanya hivyo hawafuati Utaratibu rasmi wa Kiserikali kuwezesha Ubalozi kuwa na taarifa zao

Soma - https://jamii.app/TraffickingSDA

#HumanTrafficking
UINGEREZA: WAFANYAKAZI TAKRIBAN 400 WA BBC KUPOTEZA AJIRA ZAO

Uamuzi huo ni sehemu ya Programu ya kupunguza gharama za uendeshaji na kuhamia katika Majukwaa ya Kidijitali

Shirika hilo la Utangazaji limesema hatua hiyo ni kutokana na Watu wengi kupendelea kupata Habari Mtandaoni pamoja na changamoto za Kiufadhili

Soma - https://jamii.app/AjiraBBC

#DigitalWorld
πŸ‘Ž9πŸ‘7😁2
RIPOTI: Tanzania imetajwa kwenye Nchi zenye Kiwango Duni cha Maisha ya Dijitali ikishika nafasi 107 kati ya nchi 117 Duniani zilizofanyiwa Utafiti na Surfshark

> Sababu ni Kasi Ndogo na Gharama Kubwa za Intaneti, Usalama na Sera za Nchi, Upatikanaji wa Huduma za Uhakika na Udhaifu wa Miundombinu ya Kielektroniki

Soma - https://jamii.app/DijitoTZ

#DigitalRights
πŸ‘28😁7πŸ₯΄3🀯1
RAIS SAMIA: TAFITI ZIFANYIKE KWANINI VIJANA WAKIFIKIA UMRI WA KUPATA WATOTO WANAHANGAIKA

Amesema ”Ni Mitindo ya Maisha (kuwa slim lady) au utasikia Supu ya Pweza, tatizo lipo kwenye Lishe"

β€œTukiacha mambo yaende hivi tutakuwa na Taifa la Watu goigoi, itafika mahali hatutajua Mke ni nani na Mume ni nani"

Zaidi - https://jamii.app/LisheDuni

#JFAfya
πŸ‘11😁6πŸ‘3πŸ”₯2
RAIS SAMIA: WAKUU WA WILAYA HAMFANYI KAZI, MNASUBIRI MKEKA

Amesema, ”Wakuu wa Wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka. Sikusema nitawabadilisha leo au kesho, kwahiyo kama hamfanyi kazi nyie ndio wangu.

β€œWakuu wa Mikoa nataka ripoti za Wakuu wenu wa Wilaya”

Soma - https://jamii.app/LisheDuni

#Accountability
πŸ‘13
AFGHANISTAN: Bomu la kujitoa mhanga limelipuka katika Kituo cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu na kuua Watu 23 katika Mji wa Kabul huku wengi wao wakiwa ni Wasichana

> Aidha, Watu wengine 36 wamejeruhiwa katika mlipuko huo

Soma https://jamii.app/BomuKabul

#HumanRights #JamiiForums
😒4πŸ‘2πŸ‘Ž2
WAZIRI UMMY: WATOTO MILIONI 3 NCHINI WAMEDUMAA UBONGO

Amesema Lishe bora ni Msingi wa Afya na Uchumi wa Mtu Mmoja, Familia na Taifa kwa ujumla

Asema β€œWatoto Milioni 3 wamedumaa, hawafundishiki. Hawawezi kuwa wabunifu wala kujifunza mambo mapya”

Zaidi - https://jamii.app/LisheDuni

#JFAfya
πŸ‘7
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima, amesema tabia ya unafiki wa Kisiasa ya baadhi ya Watanzania kusifia kila jambo na kujipendekeza kwa Viongozi ili wapate vyeo inazidi kuliua Taifa

Soma https://jamii.app/PadriUnafiki

#Uwajibikaji
πŸ‘17πŸ‘3
KANISA KATOLIKI LAMSIMAMISHA PADRI ANAYETUHUMIWA KUBAKA WATOTO

Padri Sostenes Bahati Soka wa Jimbo la Moshi Mkoani #Kilimanjaro anakabiliwa na Mashtaka matatu ya Ubakaji Wanafunzi wenye umri wa Miaka 12 na 13

Amesimamishwa hadi Mashtaka yake yatakapomalizika

#DomesticViolence
πŸ‘10
#UGANDA: WAATHIRIKA WA EBOLA WATAKIWA KUTOSHIRIKI NGONO KWA SIKU 90

Dkt. Ataro Ayella, Mtaalamu wa Magonjwa ya Kliniki, amesema #Ebola inaweza kuambukizwa kwa Ngono na virusi vinaweza kukaa kwenye Mbegu za Kiume hadi Siku 90

Soma - https://jamii.app/EbolaSex

#EbolaOutbreakUG
πŸ€”8πŸ‘5
CPJ: WANAHABARI TAKRIBAN 28 WAMEKAMATWA NCHINI IRAN KATIKA MAANDAMANO

Mapema wiki hii, #CPJ ilitoa wito kwa Mamlaka za Iran kuwaachia wote waliokamatwa kwa kuripoti Maandamano ya kifo cha #MahsaAmini

Pia, imetoa wito wa kurejeshwa kwa huduma ya #Internet

Zaidi https://jamii.app/WaandishiIran

#PressFreedom