DKT. FAT-HIYA: Satarani inaongoza kwa vifo hapa Tanzania na Duniani kote, kwa Muhimbili ni kama Wagonjwa 800 kwa Mwaka wanaogundulika
Tatizo kubwa ni kuwa Wagonjwa wengi wanakuja kwenye Matibabu wakati ambao Ugonjwa unakuwa umeenea sehemu kubwa, na inakuwa vigumu kutibu kwa wakati huo
Saratani ya Figo ndiyo inaongoza kwa umri wa Miaka 3-4, na Saratani ya Matezi inafuata kwa Watoto chini ya Miaka 10. Pia, kuna Saratani za Ini na Misuli.
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya

👍8
DKT. FAT-HIYA: Dalili zinazoonekana sana ni Uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Huendelea kwa kufanya Watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana Mishipa ya Mwili na Utumbo
Pia, Mtoto anaweza kuanza kukosa choo vizuri, kukojoa Damu, au kuishiwa Damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya Saratani
Wakati mwingine Homa pia huonekana, Homa hizi huwa hazisikii matibabu ya kawaida tunayoyafahamu. Tumbo linaweza kujaa, Maji kujaa kwenye Mapafu, Mtoto hakui vizuri na anaweza kupata changamoto za Upumuaji.

👍3
DKT. SHAKILU JUMANNE: Mzazi anapokuwa anamuogesha Mtoto awe na kawaida ya kumchunguza, Mfano kumminya sehemu ya Tumboni au pembeni ya Tumbo, ukibaini kuna uvimbe mfikishe Hospitali mapema
Kuna kesi nyingi zinatokea Wazazi wanakuja tayari tatizo limekuwa kubwa, ukiwauliza wanasema waliona wakajua ni Uvimbe wa kawaida na utaisha.
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
Kuna kesi nyingi zinatokea Wazazi wanakuja tayari tatizo limekuwa kubwa, ukiwauliza wanasema waliona wakajua ni Uvimbe wa kawaida na utaisha.
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
👍7
DKT. FAT-HIYA: Kuna madhara makubwa ya kuwatibu Watoto bila kujua chanzo sahihi cha Ugonjwa, Matibabu tofauti husababisha Saratani kuongezeka
Baadhi ya Wazazi hutumia Dawa za Asili ambazo wanadhani hazina Kemikali. Dawa hizi hazina Dozi kamili na zina Kemikali nyingi, zinaweza kusababisha kufeli kwa Figo na Maini.
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
Baadhi ya Wazazi hutumia Dawa za Asili ambazo wanadhani hazina Kemikali. Dawa hizi hazina Dozi kamili na zina Kemikali nyingi, zinaweza kusababisha kufeli kwa Figo na Maini.
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
👍6
DKT: SHAKILU: Watoto wengi hupata Saratani kwa sababu ambazo nyingi hazijulikani, lakini chanzo kikuu ni mgawanyiko ya mabadiliko ya Vinasaba
-
Asilimia ndogo sana ya Saratani hutokana na kurithi, pia Watoto wenye VVU wanahatari kubwa ya Kupata aina fulani za Saratani.
-
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
-
Asilimia ndogo sana ya Saratani hutokana na kurithi, pia Watoto wenye VVU wanahatari kubwa ya Kupata aina fulani za Saratani.
-
#JamiiForums #ChildCancer #JFAfya
👍4
DKT. SHAKILU: Sumu Kuvu inatokana na namna ya uhifadhi wa Nafaka baada ya Mavuno. Mfano Karanga na Maharage
Hakuna uhusiano wa Sumu Kuvu na Saratani ya Watoto, Sumu Kuvu husababisha Saratani ya Ini kwa Watu wazima.
Mjadala - https://twitter.com/i/spaces/1eaKbrkkmpQKX