JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa huu ikoje Nchini Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto utakaofanyika Septemba 29, 2022 kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

#JamiiForums
πŸ‘9
SHINYANGA: Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba #Tanzania (TMDA) Kanda ya Ziwa Magharibi, imekamata Makasha 2,200 ya Sigara bandia aina ya #SuperMatch yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.8

Meneja wa kitengo cha Uhusiano, Gaudensia Simwanza, amehoji shehena hiyo imepitaje Mipakani ikiwa Wakaguzi wanawajibika

Soma https://jamii.app/TMDASigara

#Accountability
πŸ‘4
MICHEZO: DEJAN ATANGAZA KUVUNJA MKATABA NA SIMBA SC

Mshambuliaji Dejan Georgijevic ameandika #Instagram β€œNathibitisha kuwa Mkataba wangu wa Ajira umevunjika kutokana na baadhi ya vipengele kukiukwa na Klabu ya Simba. Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga mkono na kunionesha Upendo.”

Soma: https://jamii.app/DejanSimba

#JFSports
😁11🌚3πŸ‘1
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa huu ikoje Nchini Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto utakaofanyika Septemba 29, 2022 kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

#JamiiForums
πŸ‘1
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Geita na Mara iko hatarini zaidi kutokana na kuwa jirani na Nchi ya #Uganda ambayo imekumbwa na #Ebola

Mikoa mingine ni Dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Mbeya na Dodoma ambayo ina Viwanja vya Ndege na Vituo vikubwa vya Mabasi.

Soma - https://jamii.app/EDVTZ

#JFAfya
πŸ‘5
RUVUMA: WAZEE WADAI KUNYIMWA DAWA HOSPITALI YA WILAYA

Umoja wa Wazee Wilayani Mbinga umewasilisha Malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Katibu wa Hospitali hiyo amedai Wazee wengi wana Magonjwa makubwa kuliko uwezo wa Dawa uliopo Hospitalini

Soma - https://jamii.app/WazeeMbinga

#ServiceDelivery
πŸ‘9πŸ€”3😒2
Mwanamuziki #Shakira (45) anatarajiwa kufikishwa ktk Mahakama ya Uhispania kwa tuhuma za kukwepa kodi ya takriban Tsh. 32,314,500,000

Iwapo atapatikana na hatia anaweza kufungwa Miaka 8 au faini ya Tsh. 53,169,200,000

Soma - https://jamii.app/ShakiraKodi

#JFEntertainment #Arts
πŸ€”8😱3
RIPOTI YA CAG YAWAONDOA WATUMISHI 5 WA HALMASHAURI YA MBULU

Ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi (Juma Mavumo), aliyekuwa Kaimu Mwekahazina (Ramadhan Mwakamyanda), Mweka Hazina wa sasa (Respicius Kagaruki) na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA (Nyanda Msirikale)

Mwingine ni Mhasibu wa Mapato, David Assey, aliyekopa Tsh. Milioni 6.7 kwa ajili ya matumizi ya Ofisi na kuzipeleka kwenye Akaunti binafsi

Soma - https://jamii.app/CAGMbulu

#KemeaRushwa
πŸ‘14
#JFAFYA: DTP-HepB-Hib maarufu kama β€˜Pentavalent’ ni Chanjo moja jumuishi yenye mchanganyiko wa Chanjo za kuzuia Dondakoo, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya Uti wa Mgongo na Kichomi

Chanjo hii ni ya lazima na hutolewa mara 3 kwa Mtoto, akiwa na umri wa Wiki 6, Wiki 10 na Wiki 14.

Zaidi- https://jamii.app/PentavalentVaccine

#JFAfyaJamii
πŸ‘8πŸ”₯1
DAR: BILIONI 44 ZA MIKOPO YA HALMASHAURI HAZIJAREJESHWA

Ripoti zinaeleza takriban Bilioni 60 zimetolewa ktk Halmashauri zote za Dar ila ni Bilioni 18 tu ndio zilizorejeshwa

RC Amos Makalla ameagiza kufuatiliwa kwa marejesho ya Fedha hizo zinazotolewa kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu

Soma - https://jamii.app/MikopoDar

#ServiceDelivery
πŸ‘8πŸ”₯1
#JFAFYA: Asali hubeba Masalia ya Vimelea vya Bakteria wanaoitwa 'Clostridium Botulinum' ambao ni hatari kwa Watoto wenye umri chini ya Mwaka mmoja kwa kuwa mfumo wao wa kinga za Mwili hasa kwenye Utumbo huwa bado ni dhaifu

Huathiri Mfumo wa Fahamu wa Mtoto na kumfanya kukosa Hamu ya Kula

Zaidi - https://jamii.app/AsaliWatoto

#JFAfyaJamii
πŸ‘14
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa huu ikoje Nchini Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto utakaofanyika leo Septemba 29, 2022 kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

#JamiiForums
πŸ‘4
MAREKANI: MSANII COOLIO AFARIKI DUNIA

Mkongwe huyo wa #HipHop aliyetamba na Wimbo wa 'Gangsta's Paradise' amekutwa na umauti akiwa Nyumbani kwa rafiki yake huko Los Angeles

#Coolio ambaye jina lake halisi ni Artis Leon Ivey Jr ameripotiwa kufariki kwa Mshtuko wa Moyo

Soma - https://jamii.app/CoolioRIP

#JamiiForums
πŸ‘9😒5
KICHAA CHA MBWA HAKITIBIWI KWA DAWA ZA JADI

Ofisa Mifugo Kata ya Sofu Wilayani - Mkoani Pwani, Glory Amos, ameshauri Wafugaji kuzingatia Chanjo kwa kuwa Mbwa akipata Kichaa hakuna Tiba

Kichaa cha Mbwa kinaenea kutoka kwa Wanyama kwenda kwa Binadamu (Zoonotic Disease) kupitia Virusi vya RNA na kama Mgonjwa (Mtu) hatapatiwa Matibabu uhakika wa kifo ni 100%.

Soma - https://jamii.app/KichaaChaMbwa

#JFAfya
πŸ‘9
WHO: MLIPUKO WA EBOLA UGANDA UMECHELEWA KUGUNDULIWA

Ni baada ya Uchunguzi wa awali kuonesha dalili za Mlipuko zilianza kuonekana Agosti lakini hatua hazikuchukuliwa

Timu za kukabiliana na Maambukizi zinapata ugumu kumtambua Mgonjwa wa kwanza

Zaidi - https://jamii.app/EbolaOutbreakUG

#EbolaOutbreakUG
πŸ‘7
#KENYA: Kaunti ya #Nairobi imetangaza kutupa Miili 236 iliyohifadhiwa Mochwari kwa muda mrefu na kukosa Ndugu wa kuitambua

> Ndugu/Jamaa wa Marehemu wamepewa Siku 7 kuifuata Miili hiyo iliyopokelewa kati ya Machi 2021 na Machi 2022

Soma - https://jamii.app/MaitiNRB

#HumanRights
πŸ‘6πŸ€”2
MUSEVENI: HAKUNA HAJA YA β€˜LOCKDOWN’, EBOLA HAISAMBAZWI KWA HEWA

Ni baada ya Chama cha Wahudumu wa Afya Nchini #Uganda kutaka eneo lenye Mlipuko wa #Ebola kuwekwa Karantini ili kukomesha kuenea zaidi kwa Maambukizi

Rais amesema Serikali yake ina uwezo wa kudhibiti janga hilo bila hatua hizo kuchukuliwa

Soma - https://jamii.app/EbolaLockdown

#EbolaOutbreakUG
πŸ‘7πŸ‘Ž1πŸ”₯1
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa huu ikoje Nchini Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto utakaofanyika leo Septemba 29, 2022 kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

#JamiiForums
πŸ‘5
UTAFITI DAR: 85% YA VIJANA WA KIUME WANAISHI KWA KIPATO CHA CHINI

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Repoa 85% ya Vijana wa Kiume wenye chini ya Miaka 35 wanaishi kwa kipato cha chini ya Tsh. 300,000, huku wa Kipato cha kati wakiwa 13% na uwezo wa kupata Tsh. 300,000 hadi Tsh. 1,300,000

2% pekee ndio wenye kipato cha zaidi ya Tsh. 1,300,000 kwa Mwezi

Soma https://jamii.app/VijanaDar

#Governance
πŸ‘15πŸ€”5😒2
RIPOTI: 15% YA WAFANYAKAZI WANA MATATIZO YA AFYA YA AKILI

Takwimu hizo ni za Watu bilioni 1 wenye changamoto kwa mujibu wa Ripoti ya #WHO na #ILO

Inakadiriwa bilioni 12 hupotea kila Mwaka kutokana na Msongo wa Mawazo na Wasiwasi

Soma - https://jamii.app/AfyaKazini

#MentalHealth
πŸ‘8😁1