JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#KENYA: Balozi wa Uingereza, Jane Marriott amekanusha kuishinikiza Tume ya Uchaguzi kumtangaza #WilliamRuto kuwa Rais mteule

Hii ni baada ya kusambaa kwa picha ambazo hazijathibitishwa zikimuonesha akipeana Mikono na Ruto na Chebukati

Soma https://jamii.app/KuingiliaUchaguzi

#Democracy
👍2
MAREKANI: Bilionea #ElonMusk amechukua hatua za kisheria kumuita Mwanzilishi mwenza wa #Twitter, Jack Dorsey kufika Mahakamani akiwa kama mtetezi wake juu ya kusitisha malipo ya zaidi ya Tsh. Trilioni 102 kuinunua Twitter

Soma - https://jamii.app/ElonJack

#JamiiForums #JFMatukio
👍8
UNICEF: Zaidi ya Watoto 1,000 Nchini Ukraine wameuawa au kujeruhiwa vibaya tangu kuanza kwa vita ya taifa hilo na Urusi, Februari 2022

> UNICEF imesema vifo vingi vimesababishwa na silaha za milipuko

Soma https://jamii.app/UkraineRussiaUpdates

#ChildRights #RussiaUkraineWar
👍7😢6🤔3👏2🤯1
USALAMA MITANDAONI: Kuwapa Watoto Mwongozo wanapotumia Majukwaa ya Kidijitali ni njia mojawapo ya kudhibiti hatari zinazoweza kusababishia madhara

Wakiwa Mtandaoni, Watoto wanaweza kuwa katika hatari mbalimbali zikiwemo Maudhui ya Chuki na Uonevu (Cyberbullying)

Kama Mzazi/Mlezi ni kwa namna gani unashiriki katika matumizi ya intaneti ya Mtoto wako?

Zaidi, soma - https://jamii.app/IntanetiWatoto

#DigitalRights #InternetSafety #HakiMtoto
👍3
MDAU: ZINGATIA KIPATO CHAKO KABLA YA KUMILIKI GARI

Anasema kumiliki Gari kwasasa siyo anasa bali ni moja ya nyenzo muhimu ktk Maisha ya kawaida

Anasema wapo ambao wanamiliki vyombo hivyo vya Moto lakini huanza kujutia kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu

Soma - https://jamii.app/KununuaGari

#Maisha
👍18
Rushwa kwa muda mrefu imekuwa ikitambulika kama kikwazo kikubwa cha Maendeleo. Inaweza kusababisha wizi, upotevu na matumizi mabaya ya Rasilimali

Ikiwa haitadhibitiwa, Rushwa ni tishio kwa jitihada za kupunguza umasikini na kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

#KemeaRushwa
👍3
MALAYSIA: WAZIRI MKUU WA ZAMANI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 12 JELA

Mahakama ya Shirikisho ya Malaysia leo, Agosti 23, 2022 imeidhinisha hukumu ya kifungo cha Miaka 12 jela dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Najib Razak kwa makosa ya #Rushwa

Julai 2020, Najib alikutwa na hatia ya Kuvunja Uaminifu, Matumizi Mabaya ya Mamlaka na Utakatishaji Fedha kwa kupokea takriban Tsh. Bilioni 22 kutoka 1Malaysia Development Berhad ambao ni Mfuko wa Serikali ulioanzishwa ili kukuza Maendeleo

#JamiiForums #JFGovernance #Accountability
👍4👏1
DR CONGO: Wiki moja baada ya uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mwanamke katika Mji wa Beni, Serikali imetangaza kurejea kwa Maambukizi ya #Ebola huko Kivu Kaskazini

Ni mwezi Mmoja tangu ilipotangazwa kumalizika rasmi kwa ugonjwa huo hatari

Soma - https://jamii.app/EbolaDR

#JFAfya
👍8🤔5
SENSA 2022: Wakati zoezi la Sensa likiendelea Nchini, Jamii ya #Wahadzabe wakazi wa Wilayani Mbulu wamehesabiwa baada ya Serikali kutimiza takwa lao la kupewa Nyumbu kama kitoweo

- Aidha, baadhi yao walihitaji kupewa Bangi

Soma - https://jamii.app/Hadzabe

#JFMatukio #Sensa2022
😁33🤩7👍2👏2
DAR: Wakazi wa Mtaa wa Ngobedi, Wilayani Ilala wanadaiwa kuwagomea Makarani wa Sensa kutokana na kuhesabiwa kama Wakazi wa Kisarawe

> Eneo hilo linapakana na Wilaya ya Kisarawe upande wa Magharibi na Mkuranga upande wa Kusini

Soma https://jamii.app/MgogoroChanika

#JFMatukio
👍11
SENSA ARUSHA NA KATAVI: Makarani wawili wameporwa Vifaa vyao vya Kukusanyia Taarifa (Vishikwambi) kwa nyakati tofauti

> Makarani hao walipatiwa vifaa vingine na kuendelea na kazi

Soma https://jamii.app/SensaMatukio2022

#JFMatukio #Sensa2022
👍9😱3
JESHI LA POLISI: ASKARI ALIYEMPIGA MTUHUMIWA ALIYEFUNGWA PINGU, YUPO MAHABUSU

Hii ni baada ya video kusambaa ikionesha Askari akimpiga Mtuhumiwa aliyefungwa pingu

> Kijana aliyepigwa anatuhumiwa kwa Wizi wa Simu

Soma https://jamii.app/AskariMahabusu

#JFUwajibikaji
👍12
NIGERIA: Serikali imepiga marufuku matumizi ya Wanamitindo wa kigeni na Sauti za Kigeni kwenye Matangazo yote ya Biashara na Mawasiliano kuanzia Oktoba 1, 2022

> Lengo ni kulinda vipaji vya ndani

Soma - https://jamii.app/MatangazoNG

#Governance
👍19👏1
NIGERIA: Katibu Mkuu wa Makao ya Watawa, Zita Ihedoro amesema Watu wenye silaha wamewateka Watawa wanne

- Watawa hao walikuwa wakisafiri kutoka Jimbo la Rivers kwenda Jimbo la Imo kwa ajili ya Misa ya Shukrani

Soma https://jamii.app/SistersNG

#JFMatukio #HumanRights
👍5
#SOMALIA: Baada ya shambulizi la risasi na mabomu lililoua Watu 21 na kujeruhi 117 katika Hoteli, Rais Hassan Sheikh Mohamud ameahidi vita kali ya kutokomeza Kundi la Al-Shabaab

Aidha, Serikali ya #Norway imedai katika tukio hilo la #Mogadishu kuna raia kadhaa wa Norway wameuawa

Soma - https://jamii.app/AttackInSomalia

#Governance
👍9
Ushiriki wa Wananchi ni kipengele muhimu katika #UtawalaBora. Ushiriki wao unasaidia kuimarisha #Uwajibikaji kwa Viongozi na Serikali kwa ujumla

Huwapa Wananchi fursa ya kuwa sehemu ya mchakato wa maamuzi ya Umma na Kidemokrasia. Pia, ni msingi wa Maendeleo katika Jamii

#Governance
👍7
UNICEF imesema Nchini #Ethiopia, #Kenya na #Somalia idadi ya Watu wanaokabiliwa na uhaba wa Maji imeongezeka kutoka Milioni 9.5 hadi Milioni 16.2 ndani ya Miezi 5

Nchi za Afrika Magharibi na Kati za Burkina Faso, Chad, #Mali, Niger na #Nigeria, Watoto Milioni 40 wapo katika hatari kubwa ya kukosa Maji

Soma - https://jamii.app/MajiAfrika

#HumanRights
👍10
#IRAQ: Mahakama imesitisha shughuli zake baada ya wafuasi wa Kiongozi wa Kidini, Moqtada al-Sadr kuongeza shinikizo la kuvunjwa kwa Bunge

Kiongozi huyo amesababisha uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kuamuru Wafuasi kuvamia na kudhibiti Bunge, na hivyo kuzuia uundwaji wa Serikali

Soma - https://jamii.app/IraqMoqtada

#Democracy
👍51
TUCTA YAPINGA KUFUKUZWA KAZI KWA MENEJA WA TRC

Jonas Afumwisye anadaiwa kusimamishwa kazi kutokana na kupinga Tozo za Miamala kupitia Mtandao wa #WhatsApp ambapo anadaiwa kwenda kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2003

Zaidi - https://jamii.app/MenejaTRC

#HumanRights
👍9👏2
ASILIMIA 60 YA UNYANYASAJI WA WATOTO HUTOKEA NYUMBANI

Hali ya Unyanyasaji wa Watoto Nchini imetajwa kuchangiwa na mmomonyoko wa Maadili ktk Jamii

Waziri Dkt. Dorothy Gwajima amesema Watoto wanakosa Maadili kwasababu hawatunzwi vizuri

Soma > https://jamii.app/HakiZaWatoto
#HakiMtoto
👍15