JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kutotekeleza Maagizo ya Kamati za Kudumu za Bunge (PAC na LAAC) kunakwamisha juhudi za kuimarisha #UtawalaBora katika Taasisi za Umma

Mapendekezo na Maagizo ya Kamati hizo yasipotekelezwa, inafifisha mawazo ya Wawakilishi wa Wananchi na kufanya Fedha zilizotumika kuliwezesha Bunge kufanya kazi yake kutoleta thamani

#WAJIBU #JFUwajibikaji
πŸ‘7
FINLAND: Baada ya video kuvuja ikimuonesha akicheza muziki katika sherehe binafsi, Waziri Mkuu, Sanna Marin (36) amefanya vipimo vya kuthibitisha kuwa hakuwa ametumia Dawa za Kulevya

> Hii ni baada ya kudaiwa kuwa alikuwa ametumia dawa hizo

Soma https://jamii.app/FinlandPolitics

#Privacy #Accountability
😁7πŸ‘3πŸŽ‰1
Mbu wanaweza kusababisha Magonjwa ambayo huhatarisha Maisha ya Mabilioni ya Watu ikiwemo #Malaria

Ili kujikinga, inashauriwa kupunguza nyasi na kufukia madimbwi yaliyo karibu na nyumba yako

Pia, ni muhimu kutumia chandarua na dawa za Mbu

Fahamu zaidi > https://jamii.app/MosquitoDay

#WorldMosquitoDay #PublicHealth
πŸ‘4
SOMALIA: Maafisa Usalama wamesema takriban Watu 12 wameuawa baada ya Kundi la Al-Shabaab kushambulia Hoteli ya Hayat iliyopo Mji wa Mogadishu

> Hoteli hiyo hutumiwa na Watu Maarufu wakiwemo Maafisa wa Serikali

Soma - https://jamii.app/AlQaeda12

#JFMatukio
πŸ‘1
Umoja wa Mataifa umesema takriban Watu Milioni 22 kutoka Pembe ya Afrika Mashariki wapo hatarini kukumbwa na baa la njaa kutokana na ukosefu wa Mvua Misimu 4

- Idadi hiyo ni ongezeko la Watu Milioni 9 tangu mwanzoni mwa Mwaka 2022

Soma - https://jamii.app/NjaaEA

#HumanRights
πŸ‘4πŸŽ‰1
MWALIMU ATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mwalimu wa Shule ya Msingi Madungu, Ali Makame Khatib anatuhumiwa kumchezea sehemu za siri na kumbaka Mwanafunzi wa darasa la tano

Mama wa Mtoto ndiye aliyetoa taarifa Polisi baada ya kuelezwa na Mwanaye Ukatili aliotendewa

Soma > https://jamii.app/PembaMatukio

#HakiMtoto
πŸ‘4
LIGI KUU: COASTAL UNION 0-2 YANGA

Magoli ya Bernard Morrison na Fiston Mayele yameipa Yanga ushindi dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha leo Agosti 20, 2022

Yanga imefikisha pointi 6 katika mechi 2

Soma > https://jamii.app/YangaCoastal

#JFSports
πŸ‘6πŸ‘4
RUBANI WASINZIA NDEGE YA ABIRIA 154 IKIWA ANGANI

Rubani 2 wamesimamishwa Kazi baada ya kusinzia Ndege ikiwa angani futi 37,000 na kupitiliza sehemu ya kutua

Waliamshwa na 'Autopilot Alarm' na kufanikiwa kutua dakika 25 baadaye Nchini #Ethiopia

Soma > https://jamii.app/PilotsFallingAsleep

#JamiiForums
πŸ‘17πŸ€”2πŸ‘Ž1
DEJAN AFUNGA, SIMBA YASHINDA 2-0

Dejan Georgijevic ameifungia Simba goli moja katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa Dar Agosti 20, 2022

> Moses Phiri alifunga goli la kwanza. Simba ina pointi 6 katika mechi 2

Soma https://jamii.app/SimbaKagera

#JFSports
πŸ‘11πŸ”₯5πŸ‘1
Wataalamu wa #Afya wanasema kutonyonyesha Watoto Maziwa ya Mama kunaleta athari za muda mfupi na mrefu katika Jamii yote kama ifuatavyo:

1. Watoto wasionyonyeshwa Maziwa ya Mama wanaweza kudumaa Kimwili na Kiakili hivyo kupunguza kiwango chao cha kujifunza na kutambua mambo mbalimbali

2. Viwango duni vya unyonyeshaji huchangia kuongeza kasi ya Magonjwa miongoni mwa Watoto wachanga/wadogo na kuongeza gharama za Matibabu na Huduma za Afya

3. Muda mfupi wa kipindi cha Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama huwa unaendana na kupungua kwa alama za utambuzi na kwa kiasi cha 2.6 (IQ scores)

#JamiiForums #BreastFeeding #WBW2022
πŸ‘3
AUGUSTINO MREMA AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21, 2022 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam

Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema Mrema alilazwa tangu Agosti 16, 2022 na kifo chake kimetokea saa kumi na mbili asubuhi

Enzi za uhai wake, Mwanasiasa huyo Mkongwe aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Pia, aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR-Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP. Hadi anafikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole

Soma - https://jamii.app/RIPMrema

#RIPMrema
😒38πŸ‘7
#MONTENEGRO: Bunge limepitisha hoja ya kutokuwa na Imani na Baraza la Mawaziri la Waziri Mkuu, Dritan Abazovic

Hatua hiyo ni kupinga kusainiwa kwa makubaliano ya muda mrefu ya kudhibiti uhusiano na Kanisa la #Orthodox la #Serbia

Soma https://jamii.app/NoConfidenceVote

#JFDemokrasia
πŸ‘3
KENYA: Rais Mteule, William Ruto ameteua Wawakilishi wa kutetea maslahi yake katika Kamati ya Mpito kabla ya kuapishwa

Kamati hiyo yenye Wanachama 20 ina jukumu la kuhakikisha makabidhiano ya Mamlaka kutoka kwa Rais Kenyatta hadi kwa mrithi wake

Miongoni mwa Wawakilishi hao ni Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi

Soma https://jamii.app/WawakilishiRuto

#Democracy
πŸ‘11
UTURUKI: WATU 32 WAPOTEZA MAISHA KWENYE MATUKIO MAWILI YA AJALI

Ajali ilihusisha Basi lililopinduka eneo la #Gaziantep Jumamosi asubuhi, na kuua Watu 16 huku 21 wakijeruhiwa

Saa kadhaa baadaye Lori liligonga umati wa Watu umbali wa kilomita 250 huko #Mardin na kuua Watu 16 wakiwemo watoa huduma ya Dharura

Soma - https://jamii.app/AjaliTurkey
😒7πŸ‘5πŸ”₯1
KUMBUKUMBU: Augustino Lyatonga Mrema anakumbukwa kwa mengi ikiwemo nguvu ya kisiasa Nchini #Tanzania

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu enzi za Utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi huku akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani

Mrema amewahi kuwa Mwenyekiti wa Vyama viwili vya #Siasa na kote aligombea Urais (NCCR Mageuzi na TLP)

Soma - https://jamii.app/EnziZaMrema
#RIPMrema
πŸ‘13
EPL: LEEDS UNITED YAIADHIBU CHELSEA 3-0

Leeds Utd ikiwa katika dimba la nyumbani, Elland Road imeifunga Chelsea goli 3-0

Katika mchezo huo beki wa kati wa Chelsea, Kalidou Koulibaly alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 85

Soma https://jamii.app/LeedsChelsea

#JFSports #EPL
😁20😱8😒6πŸ‘3πŸ€”1
TANZIA: WAZIRI WA ZAMANI, WILLIAM KUSILA AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, William Kusila (78) amefariki Dunia mchana wa leo, Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam

Soma > https://jamii.app/RIPKusila

#JamiiForums
πŸ‘7πŸ‘Ž2😒2
ROONEY AMSHAURI TEN HAG KUTOMPANGA RONALDO DHIDI YA LIVERPOOL

Wayne Rooney anaamini United inahitaji wachezaji wenye nguvu na kasi, huku akidai umri na kutokuwa β€˜fit’ kwa Cristiano Ronaldo kunamfanya kutokuwa na msaada kikosini

Soma https://jamii.app/UshauriWaRooney

#JFSports
πŸ‘13😁8πŸ€”2
URUSI: Wizara ya Mambo ya Ndani imesema takriban watu 16 wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya Lori kugongana na Basi dogo

- Basi lilikuwa limesimama ili kupisha ujenzi wa Barabara katika eneo la Ulyanovsk

Soma - https://jamii.app/RussiaAjali

#JamiiForums #JFMatukio
πŸ‘4😒2
UCHAGUZI KENYA: Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia Azimio la Umoja One, Raila Odinga leo, Agosti 22, 2022 anatarajia kuwasilisha Pingamizi la Matokeo ya Urais yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) yaliyompa ushindi William Ruto

Soma - https://jamii.app/RailaPetition

#KenyaDecides2022 #Democracy
πŸ‘3