JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: WAENDESHA MASHTAKA WAPINGA VIELELEZO KUHUSU UPEKUZI WA TRUMP KUWEKWA WAZI

Waendesha mashtaka wamesema Nyaraka zilizowasilishwa zina maelezo nyeti ya mashahidi waliohojiwa pamoja na vielelezo vya siri vya Mahakama

Soma - https://jamii.app/MashtakaTrump

#JFUwajibikaji
πŸ‘10
WATOTO 157 WAFARIKI KWA SURUA ZIMBABWE

Maambukizi ya Surua Nchini #Zimbabwe na vifo yameongezeka mara mbili ya ilivyokuwa Wiki iliyopita

Watoto waliofariki ni 157 huku wenye maambukizi ni zaidi ya 2,000. Wengi wao hawakupata Chanjo

Soma > https://jamii.app/VifoVyaSurua

#JFAfya
πŸ€”5πŸ‘4
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, Madiwani wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za kiutendaji za Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizotakiwa zitekelezwe na Menejimenti, na kuathiri dhana ya #UtawalaBora

Taasisi ya #WAJIBU inashauri majukumu ya Madiwani yajikite kwenye kufanya uangalizi ikiwa ni pamoja na: Uwakilishi wa Kata zao katika mikutano ya Baraza, Usimamizi wa matumizi ya Rasilimali za Halmashauri na Kutetea Maendeleo ya Kijamii na Utatuzi wa Migogoro

#JFUwajibikaji
πŸ‘7πŸ‘Ž7πŸ‘2
MAREKANI: CIA NA MIKE POMPEO WASHTAKIWA KWA KUINGILIA FARAGHA ZA WAANDISHI NA WANASHERIA

Wabunge kadhaa pia wamelishutumu Shirika hilo kwa kutunza taarifa za siri za Mawasiliano za Wamarekani

- CIA wamekataa kuzungumzia kesi hiyo

Soma - https://jamii.app/CIAPompeo

#DataProtection
πŸ‘7πŸ€”1
SIERRA LEONE: Mkosoaji mashuhuri wa Serikali ya Rais julius Maada Bio, Hassan Dumbuya ameuawa wakati wa uvamizi wa Polisi waliokuwa wakiwasaka wahusika wa maandamano

Kifo chake kimezua wasiwasi kuhusu mauaji ya kiholela ya Wapinzani

Soma - https://jamii.app/MkosoajiAuawa

#HumanRights
πŸ‘Ž7πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Haijalishi ni aina gani ya Ukatili ambao Mtoto anakumbana nao, uzoefu wake unaweza kusababisha athari kubwa katika Maisha yake kama vile majeraha ya kimwili, magonjwa ya zinaa, wasiwasi na huzuni

Wadau wote wanapaswa kushirikiana kujenga Jamii ambazo zinakataa vitendo vyote vinavyowanyang’anya Watoto Haki zao.

#JamiiForums #HakiMtoto #ChildRights
πŸ‘8
#MALAYSIA: Mahakama ya juu zaidi inatarajiwa kusikiliza ombi la mwisho la Waziri Mkuu wa zamani, Najib Razak la kubatilisha hukumu ya kifungo chake cha miaka 12

Najib Razak (69) aliondolewa Madarakani 2018 kufuatia kashfa ya ufisadi wa Mabilioni ya Dola. Alihukumiwa Miaka 12 gerezani mnamo Julai 2020.

Soma - https://jamii.app/NajibCase

#Accountability
πŸ‘3
#KENYA: MADAKTARI KUCHUNGUZA SABABU ZA KIFO CHA AFISA WA TUME YA UCHAGUZI

Mchunguzi wa Serikali na Daktari aliyeteuliwa na Familia watafanya Uchunguzi kubaini sababu za kifo cha Afisa huyo aliyetoweka kwa Siku tano na Mwili kuokotwa Mto #Meriko

Soma - https://jamii.app/UchunguziIEBC
πŸ‘4
UCHAGUZI #KENYA: EU YATOA WITO WA SULUHU YA AMANI KTK MATOKEO YA URAIS

Baada ya #RailaOdinga kukataa Matokeo ya Urais, Umoja wa Ulaya umependekeza mzozo na wasiwasi uliopo kuhusu Uchaguzi Mkuu utatuliwe kwa taratibu za Kisheria

Soma - https://jamii.app/SuluhuKenya

#KenyaDecides2022
πŸ‘8
TANGA: Miili ya Watu wawili imeokotwa ikiwa imefungwa ndani ya Mifuko ya Sandarusi (viroba) katika Kitongoji cha Dibabara

Mashuhuda wanadai waliona Gari - Toyota Landcruiser eneo la tukio na baada ya kuondoka wakabaini uwepo wa Miili hiyo

Soma > https://jamii.app/TukioTanga

#JFLeo
πŸ€”14πŸ‘4😒3
TANESCO KUZIMA MFUMO WA KUNUNUA LUKU KWA SIKU 4

Meneja Mwandamizi wa TEHAMA wa TANESCO, Cliff Maregeli ametaja sababu kuwa ni matengenezo kinga kwenye Kanzidata ya Mfumo wa LUKU

> Huduma haitapatikana Agosti 22 mpaka 25 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi

Soma - https://jamii.app/LukuTanesco

#JFGovernance
😁8πŸ‘6
#GHANA: Baraza la Uuguzi na Ukunga linamchunguza Mtengeneza Maudhui wa #TikTok, anayedhaniwa kuwa Mwanafunzi wa Uuguzi baada ya kuchapisha Video inayodaiwa kutishia kuua Wagonjwa kwasababu alilazimishwa kusomea Taaluma hiyo

Zaidi - https://jamii.app/TiktokerGhana

#PublicHealth #JFAfya
πŸ‘1
MAREKANI: RAIS BIDEN ASAINI MUSWADA WA KODI, AFYA NA TABIA NCHI KUWA SHERIA

Rais #JoeBiden ametia saini Muswada wa Dola Bilioni 700 ambao unalenga kupambana na Mabadiliko ya #TabiaNchi na gharama za #Afya huku akipandisha kodi kwa Matajiri

Soma - https://jamii.app/BidenSheria

#JFLeo
πŸ‘6😁1
TANZIA: Mwanamuziki wa #Rwanda, Yvan Buravan (27) amefariki Dunia baada ya kusumbuliwa na Saratani ya Kongosho

Buravan alianza kupata umaarufu 2016 na amefanya kazi nyingi ikiwemo ya Just a Dance (Remix) aliyoshirikiana na AY wa #Tanzania

Soma > https://jamii.app/BuravanDies
#JFSanaa
πŸ‘5😒3
UPDATE: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeahirisha zoezi la matengenezo Kinga kwenye Kanzidata ya Mfumo wa LUKU

Mapema leo, lilitangaza huduma ya LUKU kukosekana kuanzia Agosti 22 hadi 25, kuanzia Saa 4 usiku hadi 1 asubuhi

Soma https://jamii.app/MaboreshoYaahirishwa

#JFUwajibikaji
πŸ‘7
NJOMBE: JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO WAKE ILI ATAJIRIKE

Joseph Mwajombe (33) alitenda kosa Agosti 7, 2022 alipompakia Binti yake (15) kwenye Pikipiki akitoka Shuleni na kumwambia 'Freemason' wamemuagiza afanye naye mapenzi ili apate utajiri

Soma - https://jamii.app/Jela30Kubaka

#GBV
πŸ‘1
LEBANON: Jaji aamuru kuachiwa kwa Bassam al-Sheikh Hussein (42) aliyekuwa kizuizini kutokana na kuvamia benki akiwa na bunduki akitaka apewe fedha zake

> Kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, benki nchini humo zimeweka ukomo wa kiwango cha kutoa fedha

Soma https://jamii.app/LebaneseMan

#JamiiForums
πŸ‘13😁2
KENYA: RAIS MTEULE AAHIDI UTAWALA WAKE KUTOINGILIA MAWASILIANO YA WATU

William Ruto amesema atairudisha Nchi hiyo kwenye Utawala wa #Demokrasia na kwamba Mtu yeyote anaweza kuzungumza chochote na Mtu yeyote

Soma - https://jamii.app/RutoGovt

#DigitalRights #DataProtection
πŸ‘4😁2
NDOA ZA UTOTONI: Polisi na Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilayani Shinyanga wamezuia ndoa kati ya Binti wa miaka 15 na Kijana wa miaka 17 iliyokuwa ifanyike Agosti 20, 2022 kwa mahari ya ng'ombe 10 na Tsh. 200,000

Soma https://jamii.app/NdoaYaUtotoniYazuiwa

#HakiMtoto
πŸ‘8πŸ‘Ž3πŸ€”1
MISRI: GAVANA WA BENKI KUU AJIUZULU

Kujiuzulu kwake kunakuja wakati Serikali yao ikiwa kwenye mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kupata mkopo wa kusaidia kukabiliana na changamoto za Mfumuko wa Bei

Soma - https://jamii.app/GavanaEgypt

#JFGovernance #Accountability
πŸ‘4