JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KIMARA-DAR: Maarifa Hadith Matala (Dereva) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Sharifa Twaha Nyamaishwa aliyekuwa utingo wa Daladala

Mtuhumiwa na Marehemu, wote wakazi wa Kimara wanadaiwa kuwa na mgogoro wa Kimapenzi kwa muda mrefu

Soma https://jamii.app/WivuWaMapenzi

#GBV
😒7πŸ€”4πŸ‘1πŸ₯°1
MDAU: UKOMO WA MIAKA YA KUSTAAFU UPUNGUZWE HADI 50

Mdau anaamini kwa kufanya hivi itapunguza tatizo la Ajira kwa Vijana Nchini

Anasema Vijana wengi wana mawazo ya Kimapinduzi, Ndoto na Maono ya Kisasa, nguvu ya ufanisi na Watu makini zaidi ktk kazi

Mjadala - https://jamii.app/Ustaafu50
#JFSoC
😁11πŸ‘7
#MEXICO: Mwili wa Mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uhalifu, #JuanArjonLopez aliyetoweka Agosti 9, umepatikana ukiwa na majeraha Kichwani huko #SanLuis

Wanahabari wasiopungua 17 wameripotiwa kuuawa Mwaka 2022 Nchini humo

Soma https://jamii.app/MwandishiAuawaMexico

#PressFreedom
πŸ‘7🀯2😒1
KENYA: Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati amesema Makamishna waliokana kutambua matokeo walihusika na hatua zote za uhakiki na kujumlisha Kura za Urais

> Asema Maafisa hao walitaka kulazimisha uchaguzi urudiwe

Soma - https://jamii.app/ChebukatiRudia

#Democracy #Accountability
πŸ‘5🀯2
TOKYO: MJUMBE WA MASHINDANO YA OLIMPIKI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Alikutwa na dola 380,000 za Marekani zilizoingizwa kupitia miamala zaidi ya 50 kwenye akaunti ya kampuni anayoiendesha kati ya Oktoba 2017 na Machi 2022

Soma- https://jamii.app/RushwaJP

#JFUwajibikaji #Rushwa
πŸ‘7
UINGEREZA: SERIKALI KUWALIPA FIDIA YA TSH. MILIONI 281 WALIOAMBUKIZWA VVU KIMAKOSA

Waliambukizwa VVU na Homa ya Ini kupitia bidhaa chafu za Damu zilizoagizwa kutoka Marekani

> Takriban Watu 2,400 wanadaiwa kupoteza Maisha

Soma - https://jamii.app/FidiaVVU

#Accountability #Afya
😒10πŸ‘6😱6πŸ€”5
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kukosa Ujuzi ni Miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha watu katika Nchi zinazoendelea kutotumia Intaneti

Hii inapelekea washindwe kufaidika na Teknolojia, ikiwa ni pamoja na kupata Taarifa na Huduma zilizopo Mtandaoni

Kuimarisha Uwezo wa Kidigitali wa Wananchi kunasaidia kupanua wigo wa matumizi ya Intaneti

#JamiiForums #DigitalRights #DigitalSkills
πŸ‘9
KENYA: UCHUNGUZI WAONESHA AFISA WA TUME YA UCHAGUZI ALINYONGWA

Timu ya Madaktari Bingwa watano wameufanyia upasuaji Mwili wa Afisa huyo

Pia, wamepeleka #Nairobi baadhi ya vielelezo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa Kisayansi

Soma - https://jamii.app/AfisaIEBC

#HumanRightsViolations
😒3πŸ‘1
AFRIKA KUSINI: UPINZANI KUWASILISHA PENDEKEZO LA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS RAMAPHOSA

Mkuu wa zamani wa Ujasusi Arthur Fraser, amedai Rais huyo alificha takriban Tsh. Bilioni 9.3 Shambani kwake Phala Phala Mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/UpinzaniSA

#Democracy #Accountability
TAMBUA HAKI ZAKO KISHERIA UNAPOKAMATWA NA POLISI

Askari anatakiwa ajitambulishe (Jina na namba ya Uaskari), Mtuhumiwa ajulishwe kwanini anakamatwa na ana Haki ya kuwajulisha ndugu/jamaa kuhusu kukamatwa

Mtuhumiwa ana Haki ya kufikishwa Mahakamani ndani ya muda usiozidi Saa 24 tangu kukamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi

Kama kuna upekuzi wa ndani ya Nyumba Askari haruhusiwi kuingia bila kuwa na hati ya upekuzi ya Mahakama

Soma zaidi - https://jamii.app/HakiZaKisheria

#JFSheria #Justice
πŸ‘12😁5πŸ™1
#CHINA: Watu 16 wamefariki Dunia na wengine 36 hawajulikani walipo kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Jimbo la #Qinghai - Magharibi mwa Nchi hiyo

Mafuriko hayo yameathiri eneo lenye zaidi ya Wakazi 6,000 na Nyumba zaidi ya 1,500.

Soma > https://jamii.app/FloodInChina

#Floods
😒5πŸ‘2
NIGERIA: WAFANYAKAZI WA KAMPUNI ZA UMEME WAFANYA MGOMO NA KUKATA UMEME

Ni Wafanyakazi wa Kampuni za Usambazaji Umeme (TCN) na (AEDC) wakitaka kuboreshewa maslahi yao

TCN wamewaambia wateja kutakuwa na kukatika kwa Umeme kutokana na mgomo huo

Soma - https://jamii.app/UmemeNigeria
😁9🀯2πŸ‘Ž1πŸ‘1
Ili Mtoto afaidike na Maziwa ya Mama lazima akae vizuri kwenye Chuchu. Mtoto kukaa vibaya kwenye Chuchu hupelekea kumeza hewa na kumsababishia Gesi na Maumivu ya Tumbo

Pia, inaweza kumsababishia Mama kupata maumivu wakati kwa kunyonyesha na hata kidonda kwenye Chuchu

Unaponyonyesha muweke Mtoto karibu yako na Mwili wake ugeukie kwako. Msapoti Mwili wote sio Kichwa tu. Shingo yake inyooke na hakikisha kidevu chake kinagusa Titi lako

Mtoto akikaa vizuri kwenye Chuchu atanyonya taratibu bila sauti, utasika wakati anameza na Mashavu yake yanakuwa duara na yametoka nje

#JamiiForums #BreastFeedingMom #WBW2022
πŸ‘11πŸ‘1
China inatarajia kutuma baadhi ya Wanajeshi wake kwenda Urusi kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya Kijeshi kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 5, 2022

> Aidha, Nchi za India, Belarus, Mongolia na Tajikistan zitashiriki mazoezi hayo

Soma https://jamii.app/ChinaRussiaJoin

#JamiiForums
πŸ‘6πŸ‘Ž1
AGOSTI 23 KUWA SIKU YA MAPUMZIKO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Agosti 23, 2022 iwe siku ya mapumziko

> Lengo ni Watanzania wawepo Nyumbani kuwapokea Makarani wa Sensa na kutoa maelezo sahihi

Soma https://jamii.app/Agosti23

#Governance
πŸ‘15πŸ‘Ž3
RC TANGA: WALIOWEKA MIILI KWENYE VIROBA WATAKUWA WAZOEFU WA UHALIFU

RC Omari Mgumba amesema Miili ilikunjwa kama ipo ktk viroba vya Kilo 20 na kuongeza kuwa dalili za awali zinaonesha mauaji hayajafanyika Tanga bali pametumika kuitupa Miili

Soma > https://jamii.app/MauajiTanga2022
#JFLeo
πŸ‘5
JAPAN YAHIMIZA VIJANA WAKE KUNYWA POMBE ILI KUKUZA UCHUMI

Serikali ya Nchi hiyo inaanda Kampeni yenye jina "Sake Viva!" ambayo itakuja na mpango wa kufanya Unywaji Pombe kuwavutia zaidi Vijana ili kukuza uchumi

Takwimu zinaonesha Watu walikuwa wakinywa kiasi kidogo cha Pombe 2020 kuliko 1995, na idadi hiyo ilishuka kutoka lita 100 kwa Wiki hadi lita 75

Soma - https://jamii.app/AlcoholJapan
😁25πŸ‘5πŸ€”2πŸ‘Ž1
ALGERIA: MOTO WA MSITUNI WAUA WATU 26, WENGINE 350 WAHAMISHWA

Watu 24 walifariki El Tarf mpakani mwa #Tunisia na 2 Kaskazini mwa Algeria

#Algeria imekuwa ikikabiliwa na Moto wa Misituni unaochangiwa na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Soma - https://jamii.app/AlgeriaFire

#ClimateChange
πŸ‘4🀯3
LISHE YA MAMA ANAYENYONYESHA

Kula milo kamili na zaidi ya mitatu kwa siku. Mlo kamili ni mlo wenye Chakula mchanganyiko angalau Chakula kimoja kutoka katika kila kundi la Chakula

Kula Chakula kingi na cha kutosha katika kila Mlo. Kula Asusa kati ya mlo na mlo. Meza vidonge vya kuongeza Damu (FEFO) kwa kipindi cha Miezi 3 baada ya kujifungua

#JamiiForums #BreastFeedingMom
πŸ‘1
JamiiForums
LISHE YA MAMA ANAYENYONYESHA Kula milo kamili na zaidi ya mitatu kwa siku. Mlo kamili ni mlo wenye Chakula mchanganyiko angalau Chakula kimoja kutoka katika kila kundi la Chakula Kula Chakula kingi na cha kutosha katika kila Mlo. Kula Asusa kati ya mlo na…
Ongeza ulaji wa Vyakula vyenye asili ya Wanyama mfano Nyama, Kuku, Mayai, Maziwa, Samaki, Dagaa n.k. Vyakula hivi vina virutubisho mbalimbali ikiwemo Madini Chuma ambayo huongeza Damu Mwilini

Kula Matunda ya aina mbalimbali na mbogamboga kwa wingi. Kunywa Maji ya kutosha kila siku (angalau glasi 8 au lita 1.5). Jikinge na Malaria kwa kulala kwenye Chandarua na jikinge na maambukizi ya Magonjwa ya zinaa

#JamiiForums #BreastfeedingMom #WBW2022
πŸ‘5