JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NINI KINAKWAMISHA UANZISHWAJI WA BARAZA LA TAIFA LA USHAURI WA ELIMU?

Kifungu cha 6 cha Sheria ya Elimu Na. 6 Sura ya 353 ya mwaka 1978 (iliyorekebishwa mwaka 2002) kinazungumzia uanzishwaji wa Baraza la Ushauri wa Elimu

Kukosekana Baraza hilo kunakwamisha majukumu yaliyoainishwa Kisheria yakiwemo: Kumshauri Waziri, Kukuza #Elimu na kushughulikia mambo mengine yanayohusu Elimu

#JFUwajibikaji
πŸ‘2
MALI: SERIKALI YAITUHUMU UFARANSA KUWAPA SILAHA WAASI

Uhusiano kati ya Nchi hizo mbili umekuwa kwenye mzozo tangu kutokea Mapinduzi ya Serikali mara mbili pamoja na uamuzi wa Utawala wa sasa wa Kijeshi wa #Mali kutangaza kushirikiana na Urusi

Soma - https://jamii.app/MaliFrance
πŸ€”3🀯3πŸ‘1
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) itaanza kusikiliza Kesi dhidi ya FΓ©licien Kabuga (87) Septemba 29, 2022

> Anatuhumiwa kwa Uhalifu wa Binadamu akiwa Rais wa Redio iliyorusha matangazo ya wito wa Mauaji ya Halaiki ya 1994 Nchini Rwanda

Soma https://jamii.app/KesiICC

#HumanRights
πŸ‘4
HAKI YA KUPATA TAARIFA: Mbali na kuwa ni Haki ya Binadamu, Haki ya Kupata Taarifa ni nguzo muhimu katika kuchochea #Uwajibikaji kutoka kwa Mamlaka ikiwemo kwenye Masuala ya Rushwa

Haki ya Kupata Taarifa ni sehemu muhimu ili kukuza #UhuruWaKujieleza, Utawala wa Sheria na kujenga uaminifu katika Jamii

#RightToInformation #Accountability
πŸ‘1πŸ‘1
TUHUMA ZA MENDY: Mwanamke mmoja amedai Benjamin Mendy wa #ManCity alimfungia katika chumba kinachofungwa na mashine kisha akambaka

> Mendy anatuhumiwa kwa makosa 10 yakiwemo 8 ya Ubakaji, Unyanyasaji wa Kijinsia na Kujaribu Kubaka

Soma https://jamii.app/TuhumaZaMendy

#JamiiForums
🀯4πŸ‘Ž3πŸ€”3πŸ‘2πŸ₯°2
#SAUDIA: Mahakama imemhukumu Salma al-Shehab kifungo cha Miaka 34 jela kutokana na kufanya Uanaharakati kwenye Mtandao wa #Twitter

> Inadaiwa Mwanamke huyo aliwasaidia Wapinzani wanaotaka kuvuruga utulivu wa Nchi

Soma - https://jamii.app/JailedTwitter

#HumanRightsViolations
πŸ‘3πŸ‘1
LATRA: Kuanzia Septemba 1, 2022 Mabasi yanayofanya Safari za Mikoani na nje ya Nchi yasiyotumia tiketi za Mtandao hayatoruhusiwa kutoa huduma

> Hadi kufikia Agosti 17, 2022 jumla ya Mabasi 2,033 kati ya 3,916 ndio yaliunganishwa na Tiketi Mtandao

Soma - https://jamii.app/LATRASept

#JFGovernance
πŸ‘2
INDIA: Raia waandamana kupinga kuachiliwa kwa Wanaume 11 waliofungwa Kifungo cha Maisha kwa kumbaka #BilkisBano alipokuwa na ujauzito wa miezi 5

> Mwathiriwa ametoa wito kwa Serikali kubatilisha uamuzi wa kuachiliwa kwa Wahalifu hao

Soma https://jamii.app/TaharukiIndia

#GBV
πŸ‘8
#KENYA: Shule zimefunguliwa huku Mamlaka zikisema kwamba ratiba ya masomo haitaongezwa ili kuruhusu wanafunzi kufidia muda uliopotezwa

Pia, Serikali imesema Shule hazitafungwa tena hata kama kutakuwa na marudio ya Uchaguzi wa Urais

Soma - https://jamii.app/ShuleZafunguliwa

#Governance
πŸ‘5
ETHIOPIA: Waasi wa Tigray wameishutumu Serikali kwa kudhoofisha juhudi za kumaliza Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe baada ya Jeshi kudaiwa kushambulia vikosi hivyo

> Serikali imesema shutuma hizo ni njia ya Waasi kuepuka kushiriki Mazungumzo ya Amani

Soma https://jamii.app/AmaniTigray

#TigrayCrisis
πŸ‘4
SIMIYU: Yohana Josephat (40) na Lucia Michael (30) wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kuwajeruhi Watoto wao (Miaka 14 na 13) kwa kuwachoma Moto sehemu mbalimbali za Mwili kwa madai ya kuiba Mahindi ndoo moja Nyumbani kwa Bibi yao

Soma - https://jamii.app/SimiyuTukio
#HumanRights
πŸ‘5πŸ€”3
#AFGHANISTAN: MLIPUKO WAUA WATU 21 NDANI YA MSIKITI

Msemaji wa Polisi, Khalid Zadran amesema Watu 21 akiwemo Imamu wa Msikiti wamefariki na wengine 33 kujeruhiwa baada kutokea Mlipuko mkubwa kwenye Msikiti uliokuwa na Watu wengi

Soma - https://jamii.app/Mosque21

#JFMatukio
πŸ‘5πŸ€”2
#UGANDA: Kamati ya Bunge ya Mamlaka za Serikali na Biashara (COSASE) imeliambia Bunge la Nchi hiyo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege, Jennifer Bamuturaki hakuwa na sifa ya kushika wadhifa huo wakati alipoteuliwa

Soma - https://jamii.app/AirlinesUG

#Accountability
πŸ‘1
LONOMIA OBLIQUA: Ni Kiwavi anayepatikana Bara la Amerika ya Kusini na anayetoa sumu kali zaidi kuliko aina nyingine zote za Viwavi, kwa mujibu wa Guinness World Records (2016)

Hutoa sumu inayopoozesha Mfumo unaoongoza kuganda kwa Damu Mwilini. Aidha, huathiri Figo, kuvujia kwa Damu kwenye Ubongo na kusababisha Muwasho wa Ngozi, maumivu makali ya Kichwa, Kutapika, Kukojoa Damu na wekundu kwenye Ngozi

Soma zaidi - https://jamii.app/LonomiaObliqua
#JFMaarifa
πŸ‘9❀1
CASEMIRO KUTUA UNITED KWA TAKRIBAN TSH. BILIONI 167

Manchester United imekubali kumsajili Kiungo huyo Mkabaji wa Real Madrid, Casemiro baada ya klabu hizo kufanya mazungumzo kwa siku kadhaa

> Anatarajiwa kufanyiwa Vipimo vya Afya mwishoni mwa juma

Soma https://jamii.app/CasemiroManUtd

#JFSports
πŸ‘11πŸ”₯2
WIZARA YA AFYA: Watu 866,285 kati ya Watu milioni 1.71 hawakurudi kwa Dozi ya Pili ya Pfizer

> Waliopata Chanjo kamili ya #COVID19 ni 51.92% ya Wananchi milioni 30.74 wenye miaka 18 na zaidi, huku lengo likiwa ni kuchanja 70% hadi Disemba 2022

Soma https://jamii.app/ChanjoRudia

#JFAfya #UVIKO19
πŸ‘2
KOMBE LA DUNIA: MAUZO YA TIKETI YAFIKIA MILIONI 2.45

Tiketi 520,532 ziliuzwa ndani ya Siku 43 (Julai 5 - Agosti 16)

- Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, #Mexico, UAE, Ufaransa, #Argentina, Brazil na Ujerumani zinaongoza kwa ununuzi

Soma - https://jamii.app/FIFATickets

#WorldCup2022
πŸ‘9
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Mark Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka EWURA

Anachukua nafasi ya Prof. Jamidu Hazzam Yahaya ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi wake umeanza Agosti 15, 2022

Soma - https://jamii.app/MwandosyaEWURA

#JFUtawala
πŸ‘14
Popote ambapo majanga hutokea, wapo wale wanaokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatoa msaada wa haraka wa kibinadamu ikiwemo Chakula, Maji, Hifadhi, Usalama na Matibabu

Inakadiriwa Watu Milioni 274 Duniani watahitaji Misaada ya Kibinadamu mwaka 2022 kutokana na Mapigano, Umasikini, Mabadiliko ya TabiaNchi na Uhaba wa Chakula

Zaidi, soma - https://jamii.app/WorldHD2022

#WorldHumanitarianDay
πŸ‘7
LIBERIA: Rais George Weah amewasimamisha Kazi Maafisa 3 baada ya Serikali ya Marekani kuwawekea vikwazo kwa madai ya #Rushwa na Ufisadi wa Mali za Umma

Miongoni mwao yupo Nathaniel McGill, Waziri wa Nchi na Mkuu wa Wafanyakazi wa Rais

Soma https://jamii.app/MaafisaUfisadi

#KemeaRushwa
πŸ‘4