JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#RWANDA: #LilianeMugabekazi (24) ambaye alikamatwa Agosti 7 baada ya kuhudhuria tamasha la Mwanamuziki wa Ufaransa, #Tayc anakabiliwa na kifungo cha Miaka 2 kwa kuvaa “Uchafu hadharani”

Waendesha mashtaka wameomba awekwe rumande kwa Siku 30

Soma - https://jamii.app/KifungoUtupu

#GBV
👍1
ISRAEL YADAIWA KUVAMIA OFISI ZA MASHIRIKA YA HAKI ZA BINADAMU

Jeshi la #Israel limedaiwa kufanya uvamizi katika Ofisi za Mashirika 7 ya Kiraia likiyatuhumu kuwa Mashirika ya Kigaidi

> Wamechukua Kompyuta na nyaraka mbalimbali

Soma - https://jamii.app/IsraelHRights

#HumanRights
👍7👏2
KOREA KASKAZINI: Kim Yo Jong, Dada wa Kim Jong Un amemtaka Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol ‘kufunga mdomo’ baada ya kusema Nchi yake iko tayari kutoa Msaada wa Kiuchumi kwa Korea Kaskazini kama itaacha kuzalisha silaha za Nyuklia

Soma > https://jamii.app/NorthSouthKorea
👍4
MASUMBWI: MWAKINYO KUZICHAPA UINGEREZA SEPTEMBA 3, 2022

Hassan Mwakinyo (27) ambaye amepanda ulingoni mara 22 na kupoteza mapambano mawili, atapanda ulingoni kupambana na Liam Smith (34) aliyepambana mara 35 na kupoteza mapambano matatu

Soma https://jamii.app/ReturnMwakinyo

#JFSports
👍8
KAMPUNI YA #APPLE YASHAURI WATEJA KUSASISHA (UPDATE) VIFAA VYAO KWENDA IOS 15.6.1

Imesema kuna udhaifu ktk Mifumo unaoathiri #iPhones zilizoanzia modeli 6S, iPad 5th na baadaye, iPad Air 2 na zilizofuata, iPad mini 4 na kuendelea, iPad Pro zote, iPod 7th

Soma - https://jamii.app/AppleUpdates
👍4
WAZIRI NAPE: GHARAMA ZA DATA ZIMEPUNGUA TANGU RAIS SAMIA AINGIE MADARAKANI

Waziri Nape amesema Mwezi Machi 2021 bei ya juu ilikuwa ni Tsh. 40.04 kwa MB 1 na ilipunguzwa hadi kufikia Tsh. 9.35 kwa MB 1 Mwezi Agosti 2022

Soma - https://jamii.app/NapeInternet

#DigitaRights #JFGovernance
😁24🤔15👎14💩9🤬4👏1🤯1
RIPOTI: Umoja wa Mataifa unasema Sudan Kusini inaongoza kwa mazingira ya vurugu zaidi kwa watoa Misaada ya Kibinadamu Duniani, ikifuatiwa na #Afghanistan na #Syria

Watoa Misaada 5 wameuawa wakiwa kazini 2022 pekee

Soma https://jamii.app/HatariSudani

#WorldHumanitarianDay
👍3🤔1
MOSHI: Mahakama ya Hakimu Mkazi imemuachia huru Wendi Mrema aliyetuhumiwa kumuua Mama yake, Patricia Ibreack Paul (66) aliyekuwa Nesi mstaafu wa Hospitali ya KCMC

Upande wa Mashtaka umewasilisha maombi ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo

Soma - https://jamii.app/WendyMremaMahakamani
👍6😢4🤯2🤔1
MTOTO WA DOS SANTOS AKATA RUFAA KUPINGA BABA YAKE KUZIKWA ANGOLA

Tchize amekata rufaa baada ya Mahakama kuamua Mwili wa aliyekuwa Rais wa #Angola, Eduardo dos Santos kuzikwa Angola

Tchize amedai Baba yake alitaka azikwe #Barcelona, Hispania

Soma > https://jamii.app/MazikoYaDosSantos
👍3
PWANI: 21 WASHIKILIWA KWA KUHUSIKA NA MTANDAO WA WIZI

Wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa wizi uliotokea Julai 27, 2022 eneo la Mkenge

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuiba Ng’ombe 8 na kuumua mmoja wa Walinzi wa Zizi huku wakimjeruhi Mlinzi mwingine

Soma https://jamii.app/WeziMifugo
#JFLeo
AFRIKA KUSINI: Taarifa ya Waziri wa Polisi, Bheki Cele imeonesha Watu 6,424 wakiwemo Askari 18 waliuawa katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022

Hilo ni ongezeko la Watu 664 ikilinganishwa na kipindi kama hicho Mwaka 2021 Nchi ilipokuwa Karantini

Soma - https://jamii.app/CrimeSA

#HumanRights
👍5👎1
CHINA: SAMAKI WAFANYIWA VIPIMO VYA COVID-19

Mamlaka Mjini Xiamen zimeagiza samaki na wavuvi kufanyiwa vipimo vya #COVID19 baada ya kudaiwa maambukizi yanasambazwa na wanaotumia njia ya maji

Baadhi ya Wananchi wamekosoa utaratibu huo

Soma - https://jamii.app/Covid19Test

#UVIKO19
👍3😱2
UMEWAHI KUISHI BILA KAZI YA KUKUINGIZIA KIPATO KWA MUDA GANI?

Kutokuwa na Ajira au chanzo chochote cha kuingiza kipato hufanya Maisha kuwa magumu. Hali huweza kuwa ngumu zaidi endapo ukiwa na Familia inayokutegemea

Ulipopitia kipindi hiki uliwezaje kumudu kupata mahitaji ya muhimu?

Mjadala - https://jamii.app/KukosaKipato
#Maisha
👍8
Baadhi ya kauli za Waziri wa Habari na Mawasiliano kuhusu kupanda kwa gharama za Vifurushi

#JamiiForums #DigitalRights
👍2
WAZIRI NAPE: KAZI YA KAMPUNI YA MAWASILIANO SIO KUOMBA RIDHAA KWA WANANCHI

Akitolea ufafanuzi upandaji wa gharama za vifurushi vya #intaneti Nchini, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kazi ya Kampuni siyo kuomba ridhaa kwa Wananchi, isipokuwa ni kuwapa tu taarifa juu ya bidhaa mpya wanazotoa

Amefafanua kuwa Mtoa huduma hawezi tu kupandisha bei pasipo kuleta mapendekezo kwa Mamlaka (TCRA).

#JamiiForums #DigitalRights
👍1
TETESI: CHELSEA INAMTAKA HARRY MAGUIRE

Chelsea inataka kumsajili Harry Maguire wa Manchester United kwa kubadilishana na Christian Pulisic

> Inadaiwa Kocha wa United, Eric ten Hag ameanza kuwa na mashaka na kiwango cha Maguire

Soma https://jamii.app/MaguireUpdates

#JFSports
😁10👍7👎4👏1