JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUCHAGUA MASOMO YA CHUO KIKUU

Mwanafunzi au Mtu yeyote anayetaka kufanya chaguzi ya fani ya kusomea Chuo Kikuu anatakiwa kuangalia nini anapenda Maishani mwake na sio akasomee kitu gani chenye Ajira

Soma zaidi - https://jamii.app/FaniChuo

#JFSoC
👍8
PERU: Polisi wamevamia Nyumba ya Rais Pedro Castillo wakimtafuta shemeji yake, Yenifer Paredes, anayetuhumiwa kwa ufisadi na utakatishaji Fedha

Rais Castillo anakabiliwa na kesi 5 na amenusurika majaribio 2 ya kuondolewa Madarakani

Soma - https://jamii.app/UvamiziRaisPeru

#Accountability
👍13
#JFMDAU: Katika harakati za kusaka Elimu Vyuoni Wanafunzi wanakutana na 'kashikashi' nyingi zinazosababisha mpaka Mtu kuachana na Masomo

- Je, uliwahi kukutana na kisa gani kilichofanya uone Chuo kama Uwanja wa vita? Uliweza kurudi kwenye mstari au bado ni majuto tu?

Mjadala - https://jamii.app/VisangaChuoni

#JFMaisha
👍11
#KENYA: MSIMAMIZI WA UCHAGUZI AKAMATWA NA KARATASI ZA KURA

Anatuhumiwa kukutwa na karatasi za kupigia kura ambazo hazijajazwa ktk Jimbo la Starehe

Amekamatwa alipokuwa akiingia ktk kituo cha kuhesabia Kura cha Jamhuri

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍11
TETESI: PSG YAANZA MAZUNGUMZO YA KUMTAKA RASHFORD

Paris Saint-Germain imeanza mazungumzo na #ManchesterUnited kwa nia ya kumsajili Marcus Rashford

Nia ya #PSG ni kukamilisha usajili huo kabla dirisha kubwa la usajili 2022/23 kufungwa

Soma > https://jamii.app/PSGRashford

#JFSports
👍8
UCHAGUZI #KENYA: RUTO ABURUZWA KWA IDADI YA WABUNGE

Raila Odinga amepata Wabunge 134 ambapo 88 wanatoka Chama chake ODM

Atakayeshinda Urais bila kudhibiti Bunge anaweza kupata wakati mgumu wakati wa kupitisha Sheria na Bajeti

Soma - https://jamii.app/RutoNaOdinga
#KenyaDecides2022
👍6
AFRIKA KUSINI: WALIOPINGA KUKAMATWA KWA RAIS JACOB ZUMA MBARONI

- Watu 20 wamekamatwa wakituhumiwa kuanzisha machafuko ya Julai 2021 yaliyopinga kukamatwa kwa Rais Mstaafu, Jacob Zuma

Takriban Watu 350 waliuawa kwenye machafuko hayo

Soma - https://jamii.app/ArrestedSA

#Governance
👍6🤔1
AGOSTI 12: SIKU YA VIJANA DUNIANI

Siku hii inaadhimishwa kutambua na kupaza sauti kuhusu ushiriki wa Vijana katika Masuala muhimu

Pia, inasisitizia Haki za Vijana kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Ajira na Afya

Zaidi, soma - https://jamii.app/IYD2022

#YouthDay #IYD2022
4👍4
MASASI: WIVU WA MAPENZI WATAJWA CHANZO CHA MAUAJI YA WANAWAKE

Jeshi la Polisi limesema takwimu za kuanzia Machi 2022 zinaonesha kuna mauaji ya Watu 8 na Polisi wanaendelea na jitihada za kuwatafuta wahusika wa Matukio hayo

Soma > https://jamii.app/MatukioMasasi

#HumanRights #GBV
👍9🤔2
DAR: Mtoto Rehema ambaye ni pacha aliyekuwa amesalia baada ya mwenzake waliyetenganishwa kufariki dunia, ameaga Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana Agosti 11, 2022

> Pacha wa kwanza Neema alifariki Julai 10, 2022

Soma - https://jamii.app/PachaRehemaAfariki
😢21👍1
AJIRA KWA VIJANA: Kwa Mujibu wa Shirika la ILO, Mlipuko wa COVID-19 umewaumiza zaidi Vijana katika Masuala ya #Ajira

Vijana wana nguvu kubwa ya kuchochea Maendeleo ikiwa watapata Maarifa na Fursa wanazohitaji ili kustawi

Soma zaidi - https://jamii.app/IYD2022

#YouthDay #IYD2022
👍2
#SIERRALEONE: RAIS ASEMA MAANDAMANO DHIDI YA SERIKALI NI UGAIDI

Takriban Watu 130 wamekamatwa ktk maandamano hayo ya kumshinikiza Rais Julius Maada Bio kujiuzulu kutokana na kupanda kwa gharama za Maisha, Rushwa na Ukatili wa Polisi

Soma - https://jamii.app/UgaidiSierraLeone

#Democracy
🤮5👍3👎2
#SOMALIA: UNHCR imesema ukame wa kihistoria Nchini humo umepelekea Watu 1,000,000 kuyakimbia makazi yao

Idadi ya wanaokabiliwa na Njaa inatarajiwa kuongezeka kutoka Watu milioni 5 hadi zaidi ya milioni 7 Miezi kadhaa ijayo

Soma - https://jamii.app/SomaliaNjaa
#HumanRights
👍4😢2
YANGA YATHIBITISHA KUACHANA NA BUMBULI

Taarifa iliyotolewa na Yanga imesema Afisa Habari, Hassan Maulid Bumbuli anaondoka Jangwani baada ya kumaliza Mkataba wake

Bumbuli ameitumikia Klabu hiyo kwa kipindi cha Miaka Mitatu

#JFSports
👍4
UCHAGUZI KENYA: #DidmasBarasa aliyeshinda Ubunge wa Jimbo la #Kimilili amejisalimisha katika kituo cha Polisi baada ya kutoweka kwa siku 3

Anadaiwa kumuua kwa risasi Msaidizi wa Mpinzani wake, Brian Olunga usiku wa Agosti 9, 2022

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍5
KOREA KUSINI: BOSI WA SAMSUNG ASAMEHEWA KUNUSURU UCHUMI

Serikali imesema Lee Jae-yong atafutiwa kifungo ili kusaidia Nchi kuondokana na mzozo wa Uchumi

Alihukumiwa kwenda jela miezi 30 baada ya kukutwa na hatia ya Ubadhirifu na #Rushwa mwaka 2021

Soma - https://jamii.app/MsamahaWaKifungo
👍12
Wataalamu wa #Afya wanasema suala la Maziwa ya Mama kuchacha yakiwa Kifuani ni Imani potofu ndani ya Jamii na ni jambo ambalo halina ukweli kwasababu Maziwa hayachachi yakiwa ndani ya Mwili

Endapo Mama ameajiriwa anashauriwa kufanya maandalizi mapema ya kukamua Maziwa na kuyagandisha kwenye Jokofu/Friji ili aweze kuyatumia kumlisha Mtoto pale likizo ya Uzazi inapomaliza

#BreastFeedingMom #WorldBreastFeedingWeek2022
👍1
Hati Inayoridhisha hutolewa wakati Mkaguzi anaporidhika kuwa Hesabu za Mkaguliwa zimetayarishwa kwa usahihi na kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu na vile vinavyotolewa na Bodi ya NBAA

Katika Ukaguzi wa Serikali Kuu, Mashirika ya Umma pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa, CAG alikagua Taasisi 712. Matokeo yanaonesha kuna ongezeko la 11% la Taasisi zilizopata Hati Zinazoridhisha

#JFUwajibikaji
👍5
#JFAFYA: Kampuni ya Johnson & Johnson imetangaza kuacha kuuza Poda yake ya Watoto Duniani kote ifikapo Mwaka 2023

Poda hizo zimezua hofu kwa watumiaji kwa madai ya kuwa na Kemikali za #talc zinazosababisha Saratani ya Ngozi

Soma - https://jamii.app/JJPowder

#PublicHealth
👍4
AFRIKA KUSINI: Zaidi ya Tai 100 katika Hifadhi ya Wanyamapori ya #Kruger, wameripotiwa kufa baada ya kula mzoga wenye sumu

Ndege hao wanatajwa kuwa katika hatari ya kutoweka duniani kutokana na idadi yao kuzidi kupungua

Soma - https://jamii.app/TaiWafaKwaSumu

#JFMazingira
👍2😢1