JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI KENYA: Maafisa wa Tume wameitisha Kikao cha Dharura baada ya sintofahamu kutokea katika Ukumbi wa kuhakiki kura za Urais, baada ya Kompyuta kuingizwa ukumbini kinyume na Taratibu

> Mchakato wa uhakiki umeahirishwa

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘3πŸŽ‰2
MDAU: TABIA ZA FURSA​

1. Fursa ina tabia ya Kufa na Kuzaliwa. Acha mazoea kwasababu Dunia inabadilika, ikibadlika Fursa pendwa hufa na mpya huzaliwa

2. Fursa hutengenezwa. Kutengeneza Fursa ni kuliona hitaji ambalo Watu wanalo japo wao hawaoni kama wanalo

Zaidi, soma - https://jamii.app/TabiaFursa
#JFSoC
πŸ‘4
KENYA: TUME YAKANUSHA MIFUMO YA KURA KUDUKULIWA

Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya imesema mifumo yao ya kuhesabu kura haiwezi kudukuliwa

Wamesema taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu udukuzi wa mifumo ya kura si za kweli

Soma > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides #Democracy
πŸ‘3
VIJANA NA DIGITALI: Majukwaa ya Kidigitali yamefungua Fursa mbalimbali kwa Vijana ikiwemo Ajira, Ujasiriamali, Ubunifu, Maarifa/Elimu na kuongeza Ushiriki wao katika Masuala ya Kisiasa na Kidemokrasia

Ujuzi wa Kidigitali umekuwa hitaji muhimu katika maisha yetu ya kila siku, lakini kundi kubwa la watu bado linaachwa nyuma kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo gharama

Zaidi > https://jamii.app/IYD2022

#YouthDay #IYD2022 #DigitalRights
πŸ‘4
HOJA: SIRI ZA MAISHA NA MARAFIKI KATIKA KUFANIKIWA

1. Tengeneza 'Connection' na Watu ila usitengeneze urafiki kwasababu siyo rahisi Rafiki akubali upate zaidi yake. Usimwamini sana Rafiki yako kwasababu na yeye ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako

2. Ukiona kila Mtu anakurushia Mawe usijifariji kwamba Mti wenye Matunda ndio unaopigwa Mawe. Kuna Miti mingine inapigwa Mawe kwasababu ina Nyoka! Jitathmini

Zaidi, soma - https://jamii.app/SiriMaisha

#JamiiForums #Maisha
πŸ‘7😁2
UCHAGUZI KENYA: TAREHE YA KUAPISHWA RAIS KUWA SIKUKUU RASMI YA UMMA

Taarifa imetolewa na Kamati ya Makabidhiano ya Madaraka na Ofisi ya Urais ambayo itawezesha mchakato wa Makabidhiano ya Ofisi kati ya Rais mstaafu na Rais Mteule

Zaidi https://jamii.app/Kenya2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘6
MESSI AKOSEKANA KWENYE MAJINA YA KUWANIA TUZO YA BALLON D’OR

- Lionel Messi hajatajwa kwenye orodha ya Wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo kwa mwaka huu

- Tangu mwaka 2005, Messi amekuwa akitajwa kuwania tuzo hiyo aliyoishinda mara 7

Soma https://jamii.app/MessiOutBallon

#JFSports
πŸ‘7πŸ‘Ž4
POLISI: IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo, ACP Pili Omary Mande anakuwa RPC wa Lindi, ACP Marco Chillya anakuwa RPC wa Ruvuma

ACP Gaudianus Kamugisha anakuwa RPC wa Kusini Unguja

Soma > https://jamii.app/IGPWamburaUpdates

#JamiiForums
πŸ‘4πŸŽ‰2😁1
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA IEBC ATOWEKA

Daniel Musyoka ameripotiwa kutoweka na haijulikani alipo

Mara ya mwisho alionekana Agosti 11, 2022 katika Kituo cha Kuhesabia Kura, akasogea pembeni kuzungumza na simu, hakurudi

Soma > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
πŸ€”11πŸ‘4🀩4
UCHAGUZI #KENYA: RAIS KENYATTA KUKUTANA NA WATEULE WA CHAMA CHA AZIMIO

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzungumza na wateule wote wa Azimio kuhusu Matokeo ya Urais ambayo bado hayajawasilishwa kikamilifu na Tume ya Uchaguzi

Fuatilia Yanayojiri > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘6😁6
#KENYA: Wafuasi wa Raila Odinga wanadai kuna dalili za wizi wa kura katika baadhi ya maeneo ambayo William Ruto amepata kura nyingi

Wanadai kura katika vifaa vya KIEMS hazilingani na idadi iliyopo katika Makaratasi

Soma zaidi > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
πŸ‘10
KENYA: Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kama Wakala wa Mgombea Urais, Raila Odinga amesababisha mzozo kwenye Kituo cha Kuhesabu Kura cha Runyenje-Embu baada kukutwa na Fomu za Matokeo

> Wakala wa Odinga aliyekuwepo kituoni hapo siku zote alikana kumfahamu mtu huyo

Zaidi - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
πŸ‘5πŸ€”4
#KENYA: Uamuzi wa kesi iliyofunguliwa kuzuia uapisho wa Mgombea Urais William Ruto na Mgombea Mwenza wake, Rigathi Gachagua ikiwa watashinda Uchaguzi unatarajiwa kutolewa Agosti 16, 2022

Wanaharakati waliofungua kesi wanadai Gachagua hafai kushika wadhifa huo

#KenyaDecides2022
πŸ‘5
MATOKEO: TUME YA UCHAGUZI YAONDOA KURA 10,000 ZILIZOMBEBA RUTO

IEBC imesahihisha idadi hiyo kutoka eneo la Kiambu baada ya kuripotiwa makosa kwenye Fomu 34B

Takwimu zinazotajwa kuwa sahihi zinaonesha William Ruto ana Kura 41,050 na si 51,050 zilizotajwa awali

#KenyaDecides2022
πŸ‘9πŸ€”4❀1😁1
UCHAGUZI KENYA: TAREHE YA KUFUNGUA SHULE YASOGEZWA MBELE

Shule zitafunguliwa Agosti 18, 2022 badala ya Agosti 15, 2022 (Jumatatu ijayo) iliyotangazwa awali kwasababu zoezi la kuhesabu Kura bado linaendelea

Shule zilifungwa ghafla mwanzoni mwa Mwezi Agosti, kitendo ambacho Wazazi wengi hawakufurahia. Hali hiyo ilipelekea Waziri wa Elimu, George Magoha kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza

#KenyaDecides2022
πŸ‘5
MONTENEGRO: Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 34 aliyetumia bunduki ya kuwinda Wanyama, ameua Watu 11 kati yao wakiwemo Watoto wawili katika Mji wa Cetinje

> Raia walimuua Mtu huyo ambaye aliingia mtaani na kuanza kushambulia Watu kwa risasi

#JFMatukio
πŸ‘Ž6πŸ‘3πŸ€”1
MDAU: MKONO MTUPU HAULAMBWI

Anasema tumekuwa tukiwalaumu Watu waliofanikiwa Kimaisha kuwa wanapendelewa, lakini hatujui ni juhudi kiasi gani waliweka

Anashauri kujitahidi kuchangamana na kujihusisha na Watu unaokutana nao. Pia, usiwe muoga wa kuwasiliana na Watu kadiri unavyopata nafasi, na sio pale tu unapokuwa na shida

Unakubaliana na mawazo yake?

Tembelea - https://jamii.app/MkonoMtupu

#JFSoC #Maisha
πŸ‘6πŸ‘5πŸŽ‰1
MAREKANI: MWANDISHI WA 'AYA ZA SHETANI' ASHAMBULIWA KWA KISU

- Salman Rushdie, Mwandishi wa Fasihi ambaye amekuwa akikabiliwa na kitisho cha kuuawa kutokana na Uandishi wake, amechomwa Kisu Mjini #NewYork na yuko katika Hali mbaya

Soma - https://jamii.app/RushdieStabbed
πŸ‘13πŸ€”2
#KENYA: SERIKALI YASITISHA RUZUKU YA UNGA

Uamuzi huo utakaowatalazimu Wananchi kununua Unga wa Mahindi kwa bei ya juu, umechukuliwa baada ya Mfuko wa Hazina ya Taifa kushindwa kulipa Ruzuku kutokana na uhaba wa Fedha

Soma - https://jamii.app/RuzukuYaUnga

#Governance
πŸ‘4😒1
UDUMAVU KWA WATOTO IRINGA NI 47%

Takwimu za udumavu kwa Watoto chini ya umri wa Miaka mitano Iringa zinaonesha, Watoto 47 kati ya 100 wamedumaa

Wazazi wametakiwa kuwapa Lishe bora Watoto ikiwemo Samaki na Maziwa

Soma > https://jamii.app/UdumavuIringa

#JFAfya #HakiMtoto
πŸ‘6