JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau anashauri kujiongezea ujuzi na maarifa ya Kiuchumi, #Afya, Kilimo, #Biashara na Kijamii kwa kusoma kozi fupi ambazo hutolewa bure Mtandaoni

Pia amesisitiza kufanya ‘Google’ na ‘YouTube’ marafiki ktk Maisha ya kila siku

Soma - https://jamii.app/TeknolojiaElimu

#DigitalWorld
👍17
IVORY COAST: Rais Alassane Ouattara ametoa Msamaha kwa Mtangulizi wake, Laurent Gbagbo aliyehukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela

Mwaka 2018 Gbagbo alikutwa na hatia ya kuhusika katika machafuko ya Kisiasa baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2011

Soma https://jamii.app/MsamahaWaRais

#Governance
👍12👎1
EPL: MAN UNITED 1-2 BRIGHTON

Manchester United ikiwa nyumbani Uwanja wa Old Trafford imefungwa goli 2-1 ktk mchezo wake wa kwanza wa Premier League 2022/23, leo Agosti 7, 2022

Cristiano Ronaldo alianzia benchi katika mchezo huo

Soma > https://jamii.app/ManUYafungwa

#EPL #MUNBHA #mufc
😁12👍11👎3🔥1
LEO KATIKA HISTORIA: Miaka 24 iliyopita leo (Agosti 07, 1998) Balozi za Marekani Dar es Salaam (Tanzania) na Nairobi (Kenya) zilishambuliwa na Magaidi

#JFHistoria
👍14👎3😢2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tunawatakia Wiki njema. Usiache kuwa WEWE siku zote!

#JamiiForums
👍16👎2
Sikukuu ya Maonesho ya Wakulima 'Nane Nane' iliadhimishwa kwa mara ya kwanza Mwaka 1977 ili kuongezea nguvu Sera ya Serikali ya wakati huo ya 'Siasa ni Kilimo'

Jamii Forums inakutakia maadhimisho mema ya Siku hii. Asante kwa kuendelea kuwa sehemu ya Familia yetu

#JamiiForums
👍13
UCHAGUZI KENYA: Benedict Manzin, Mchambuzi wa Siasa za Afrika-Kusini mwa Jangwa la Sahara amesema Wafuasi wa William Ruto na Raila Odinga wanasambaza taarifa zinazodai Wapinzani wao wana njama za kuiba kura

Mashirika ya Kiraia Nchini #Kenya na Shirika la Uangalizi yameonya kwamba Taarifa hizo potofu zinahatarisha #Demokrasia na yametaka Mitandao ya Kijamii kuchukua hatua

Soma - https://jamii.app/SMUchaguziKE

#KenyaDecides
👍12
Ukaguzi wa CAG umeonesha kumekuwa na utolewaji wa Fedha zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge kwa baadhi ya Halmashauri

Hii inaweza kusababisha Fedha za Umma kutumika vibaya na Watumishi wa Halmashauri hizo kwasababu Fedha iliyopelekwa ni kubwa kulinganisha na mahitaji halisi

#JFUwajibikaji
👍5
Wakiongozwa na Misri, #Israel na #Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa #Gaza yaliyofanyika kwa Siku tatu mfululizo

Watu 44 wameuawa ambapo kati yao Watoto ni 15, huku Wapalestina 350 wakijeruhiwa

Soma > https://jamii.app/IsraelGazaChaos

#JFLeo #GazaUnderAttack
👍6
Rushwa inakwamisha Maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii pamoja na Kisiasa. Pia ni kikwazo kikubwa kwa #UtawalaBora kwa Mataifa mengi Barani Afrika na Duniani kwa ujumla

Rushwa huathiri Ustawi wa watu binafsi, Familia na Jamii kwa ujumla. Hata hivyo, Wahanga wakubwa wa tatizo hili ni Watu wa Hali ya Chini Kiuchumi

Unashauri nini kifanyike kuimarisha Mapambano dhidi ya Rushwa?

#KemeaRushwa #JamiiForums
👍3
ETHIOPIA: WAASI WA #TIGRAY WAGOMEA MAZUNGUMZO YA AMANI

Wamesema hawawezi kuzungumza ikiwa Watu wao bado hawana huduma za Mawasiliano, Benki na Umeme

> Mnamo Mwezi Julai Waasi hao walikubali mazungumzo iwapo huduma hizo zingerejeshwa

Soma https://jamii.app/TigrayPeaceTalks

#TigrayCrisis
👍4👏1
RB LEIPZIG YAAFIKIANA NA CHELSEA KUMSAJILI TIMO WERNER

RB Leipzig imekubaliana na Chelsea kumnunua Mshambuliaji Timo Werner kwa Paundi Milioni 25.3 (Tsh. 70,840,000,000)

Werner anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ili kujiweka sawa kwa ajili ya Kombe la Dunia

#JFSports
👍8
SOMALIA: Maeneo ya karibu na Ikulu ya Rais wa #Somalia Mjini #Mogadishu yameshambuliwa kwa mabomu muda mfupi baada ya Bunge kuidhinisha Baraza la Mawaziri lenye Wajumbe 75

Somalia, taifa lililopo katika pembe ya Afrika linakabiliwa na Umasikini na janga la njaa

Soma - https://jamii.app/BomuIkuluSom
👍7
NIGERIA: Jeshi limetangaza kumuua Kiongozi wa Kundi la Boko Haram, Alhaji Modu ‘Bem Bem’ katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika Agosti 3, 2022 kwenye Jimbo la Borno

> Pia, Wanamgambo 27 wa kundi hilo wameua katika mashambulizi

Soma https://jamii.app/28KilledInNigeria

#JamiiForums
👍11
Majukwaa ya Kidigitali yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kupitia;

- Fursa za Ubunifu na #Ujasiriamali ambazo husaidia kuinua Uchumi

- Utoaji Elimu/Maarifa ya Kidigitali yanayohitajika katika Soko la #Ajira

Zaidi, soma > https://jamii.app/DigitalSDGs
👍5
DAR: Msanii wa Nigeria, Kizz Daniel anashikiliwa Kituo cha Polisi Oysterbay baada ya kupokea malipo ya kuburudisha katika Ukumbi wa Next Door Arena na kushindwa kutokea eneo husika

> Aidha, 'Passport' yake inashikiliwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/KizzDanielArrested

#Arts #JFSanaa
👍19
DR-CONGO: Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) waliopo Mashariki mwa Nchi hiyo wamewaua takriban Watu 16 akiwemo Kapteni wa Jeshi katika mashambulizi mapya dhidi ya Vijiji

> Waasi hao wanadaiwa kulenga maeneo ya Kandoyi na Bandiboli

Soma https://jamii.app/DRCRebelsAttack

#HumanRights
👍3
MANCHESTER UNITED YATAKA KUMNUNUA RABIOT

- Man. Utd imekubaliana na Juventus kumnunua Kiungo Adrien Rabiot (27) kwa ada ambayo bado haijafahamika

- Hata hivyo, Man. Utd bado inajadiliana na Wakala wa Kiungo huyo ambaye pia ni mama yake ili kuafikiana matakwa binafsi

#JFSports
👍5
UCHAGUZI KENYA: Wasimamizi 4 wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wamefukuzwa kwa madai ya kukutana na Mgombea nyumbani kwake kinyume na maadili ya Uchaguzi

Watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi wakisubiri kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MaafisaWafukuzwa

#KenyaDecides
👍12👏4
SIMBA DAY: SIMBA 2-0 SAINT GEORGE

Simba imeshinda magoli 2-0 dhidi ya Timu ya Saint George ya Ethiopia katika Tamasha la #SimbaDay, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo Agosti 8, 2022

Magoli yamefungwa na Kibu Denis na Nelson Okwa

Soma > https://jamii.app/Simba2George0

#JFSports
👍17👏1