JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Tume ya Uchaguzi imesitisha Uchaguzi wa Ugavana katika Kaunti za Kakamega na Mombasa, kutokana na makosa ya uchapishaji kwenye karatasi za kupigia kura

Tarehe nyingine ya Kupiga kura itatangazwa hapo baadaye

Soma https://jamii.app/UchaguziUgavana

#KenyaDecides
👍13🔥2
WAKENYA KUAMUA RAIS AJAYE

Taifa hilo litamchagua Rais wake wa Tano leo Agosti 9, 2022

Wapiga Kura wanaotarajiwa kushiriki zoezi ni 22,120,458

Wagombea Urais ni pamoja na George Wajackoyah, David Mwaure, William Ruto na Raila Odinga

Fuatilia Yanayojiri > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides
👍12🔥3
PICHA: Mgombea Urais wa Kenya, William Ruto amepiga Kura katika Shule ya Msingi Kosachei huko Sugoi. Mgombea Mwenza wake, Rigathi Gachagua naye amepiga Kura eneo la Mathira, Kaunti ya Nyeri

Mgombea Mwenza wa Raila Odinga kupitia Azimio la Umoja, Martha Karua amepiga Kura huko Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga na Mgombea David Waihiga Mwaure amepiga Kura yake Jijini Nairobi

#KenyaDecides2022
👍12🎉2
KENYATTA APIGA KURA: Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amepiga kura eneo Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu huku akiwataka Wakenya kuipa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) muda na nafasi ya kujumlisha na kutangaza matokeo kwa uhuru

Amesema "Matumaini ya Wakenya wengi kuwa uchaguzi huu utakuwa Huru na Haki, Watu wapige kura na kurudi nyumbani kwa amani"

#Democracy #KenyaDecides2022
👍9👏1
KENYA: Mgombea Ubunge wa Kenya Kwanza, Hamisi Butichi anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa na mapanga na silaha nyingine katika Kituo cha Kupigia Kura

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
🤔7👍4
KENYA: Raia 11 wamewasilisha ombi ktk Mahakama ya Juu kuzuia kuapishwa kwa William Ruto na Rigathi Gachagua ikiwa watashinda, wakisema kuapishwa kwao kutakuwa ni ukiukwaji wa Katiba

> Wawili hao wametajwa kuwa na kashfa za Ufisadi na Uhujumu Uchumi

Soma - https://jamii.app/KuapishwaRuto

#Democracy #KenyaDecides2022
👍18
UCHAGUZI KENYA: Mwanaume mmoja amejeruhiwa kwa risasi katika eneo la Eldoret nje ya ofisi ya mmoja wa Wagombea Ugavana wa Uasin Gishu

> Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa kilichotokea unaendelea

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides #Democracy #Kenya2022
👍6🤔1
KENYA: Mgombea wa Urais wa UDA, William Ruto amesema yupo tayari kukubali matokeo ya mchakato wa Uchaguzi Huru na wa Haki

> Ruto amesema kwa kawaida matatizo ya Uchaguzi huja pale ambapo Wagombea hukataa matokeo

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#Democracy #KenyaDecides2022
👍8🤔1
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Mwenza wa Urais wa UDA, Rigathi Gachagua alilazimika kusubiri kwa muda mrefu baada ya Mfumo wa Kibiomertiki kushindwa kumtambua

> Hata hivyo alipiga kura kupitia Orodha ya Wapiga Kura iliyochapishwa

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍81
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesimamisha Uchaguzi wa Wabunge wa Jimbo la Rongai, Kaunti ya Nakuru baada majina ya Wagombea, Masanduku ya Kura na Karatasi za Kupigia Kura kukosekana kwenye Vituo vya Kupigia Kura

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍6
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
NAIROBI, KENYA: Mgombea Urais kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga amesindikizwa na kundi kubwa la Wafuasi wake katika Kituo cha Kura kilichopo Shule ya Msingi Old Kibera alipokwenda kupiga kura

> Odinga anagombea nafasi hiyo kwa mara ya 5

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#Democracy #KenyaDecides2022
👍12
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Urais wa Chama cha Roots, Prof. George Wajackoyah ameshindwa kupiga kura katika Kituo cha Matungu baada ya mfumo wa biometriki kutomtambua

Taratibu za kuwezesha Upigaji kura zinaendelea

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍7
KENYA: Polisi wa kupambana na ghasia wamepelekwa katika Jimbo la Rongai baada Uchaguzi wa Wabunge kuahirishwa

> Waandamanaji wenye hasira wamechoma matairi ya gari nje ya Kituo cha Kupiga kura cha Mercy Njeri

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍6😁1
#JFDATA: Uchaguzi Mkuu wa Kenya unafanyika leo Agosti 9, 2022 ambapo Wapiga Kura 22,120,458 wamesajiliwa huku Vituo vya Kupigia Kura vikiwa 46,229

Wagombea wapatao 16,108 wanawania katika Nafasi mbalimbali. Miongoni mwa Nafasi 6 zinazowaniwa ni Urais, Ugavana, Useneta na Ubunge

#KenyaDecides2022 #Democracy
👍9
KENYA: Wanamgambo wa Al-Shabaab wameripotiwa kuvamia lori lililokuwa na Raia waliokuwa wanaelekea kupiga kura, kuwaamuru kushuka na kisha kulichoma moto

> Wanadaiwa kuwaonya Wenyeji kutoshiriki zoezi la Upigaji wa Kura

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍11👎5
UCHAGUZI KENYA: Raia 6,567,869 wamepiga Kura kufikia saa 6 mchana, ikiwa ni 30% tu ya Wapiga Kura wote Nchini humo

Aidha, Wakenya wanaoishi katika Nchi 12 ikiwemo #Tanzania wanaruhusiwa Kupiga Kura katika Vituo vilivyoidhinishwa

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍15
KENYA: Tume ya Uchaguzi imeidhinisha Vituo 238 kutumia Sajili za Mikono kupiga kura, ikiwa Mfumo wa Biometriki utasumbua

> Vituo 84 ni katika Jimbo la Makueni na 154 kutoka Matungu, Mumias-Mashariki na Magharibi

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍2
KENYA: Mbunge wa Nakuru, David Gikaria anayetetea nafasi yake ktk Uchaguzi wa 2022, anashikiliwa na Polisi baada ya kutokea mabishano kati yake na Askari katika Kituo cha Kupiga Kura

> Gikaria anawania Ubunge kupitia UDA

Soma https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
👍4