JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LINGARD ATIMKIA NOTTINGHAM FOREST

Mchezaji wa zamani wa Man. United, Jesse Lingard (29) amejiunga na Nottingham baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja

Amechagua kujiunga na Klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu licha ya kuwaniwa pia na West Ham United na Everton

#JFSports
😁8πŸ‘4πŸ‘3πŸ‘Ž1🀯1
PAPE SAKHO ASHINDA TUZO YA GOLI BORA CAF

Ameshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka katika Tuzo za CAF. Alifunga Goli hilo dhidi ya ASEC Mimosas, Februari 13, 2022

Amewashinda Gabadinho wa Orlando na El Moutaraji wa Wydad

Soma > https://jamii.app/GoliBoraCAF

#CAFAwards2022 #JFSports
πŸ‘34❀9😁2
COLOMBO, SRI LANKA: Vikosi vya Usalama vimevamia kambi ya Waandamanaji na kuwafukuza waliokuwa nje ya Ofisi ya Rais

Baada ya kuapishwa, Rais Ranil Wickremesinghe alionya kuwa watakaoweka makazi kwenye majengo ya Serikali watachukuliwa hatua

Soma https://jamii.app/SLProtestors

#Democracy
πŸ‘5πŸ‘Ž3
KITU GANI HUSABABISHA CHUKI KAZINI?

Mdau wa JamiiForums.com anasema ni dhahiri Binadamu tunatofautiana, lakini chuki, visasi, ubaya na mengine yasiyopendeza huletwa na nini?

Anauliza: Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo? Unajua zaidi yao na unaonekana tishio? Au inatokea tu Mtu kukuchukia bila sababu ya msingi?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/ChukiKazini

#JFMaisha
πŸ‘7πŸ€”4🀩1
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi imesema kukamatwa kwa Wakandarasi wa Smartmatic International BV kutaathiri Uchaguzi kwa kuwa hao ndio Wawekaji na Wasimamizi ya Teknolojia ya Uchaguzi

> Mamlaka hazijaweka wazi sababu za kuwashikilia Wakandarasi hao

Soma https://jamii.app/UchaguziKenya2022

#Kenya2022
πŸ‘5🀩5
Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2021 ya Taasisi ya Article 19, #UhuruWaKujieleza unaendelea kupotezwa polepole lakini kwa nguvu kubwa katika maeneo mbalimbali duniani

Bila mtiririko huru wa mawazo na ukosoaji, Jamii haiwezi kuchochea ustawi wa wengi. Katika Nchi yoyote, Raia wanapokosa Uhuru wa Kuzungumza inakuwa ngumu kutatua matatizo yanayohitaji kutatuliwa

Soma zaidi - https://jamii.app/UhuruKujieleza1

#FreedomOfExpression
πŸ‘5❀1
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAPINGA KUFUKUZWA CHADEMA MAHAKAMANI

Katika Shauri walilofungua, wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA kuwavua Uanachama baada ya kukubali kuapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum bila ridhaa ya Chama

Soma - https://jamii.app/Wabunge19Kesi

#JFSiasa
πŸ‘4πŸ€”1
Pengo kati ya Wanaume na Wanawake katika upatikanaji na matumizi ya Intaneti ni changamoto duniani kote. Asilimia kubwa ya watu Bilioni 2.9 ambao hawafikiwi na Huduma hiyo ni Wanawake na Wasichana

Tatizo hili lipo zaidi kwa Nchi Masikini, ikiwemo zilizopo Barani Afrika ikielezwa baadhi ya sababu kubwa ni Kipato, Eneo na Elimu

Soma zaidi - https://jamii.app/PengoDigitali2

#DigitalRights
😁4πŸ‘2
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#Ajira
UGONJWA WA #MONKEYPOX: Wataalamu wa Afya wa #WHO wamekutana kujadiliana kuona kama kuna ulazima wa kutangaza ugonjwa huo kuwa ni hali ya dharura

> Kuna kesi 15,400 za maambukizi ya Virusi hivyo katika Nchi 71 tangu Mei 2022

Soma https://jamii.app/MonkeypoxUpdates

#JFAfya
πŸ‘5
DAR: Watu 9 wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na tukio la Ujambazi lililotokea usiku wa kuamkia leo Julai 22, 2022 ktk Kiwanda cha Sheri-Keko, Wilaya ya Temeke

> Wamekutwa na gari (T201 DXN) aina ya Toyota Hiace ikiwa imebeba mali za wizi

Soma https://jamii.app/WahalifuDar
πŸ‘7πŸ‘Ž1
DODOMA: Serikali imewapa siku 7 Wakazi wa Msalato waliojiorodhesha kudai fidia katika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato wakitambua wao si wamiliki halali wa viwanja, kufuta majina yao Ofisi za Serikali ya Mtaa

> Watakaokaidi watachukuliwa hatua

Soma https://jamii.app/ArdhiDodoma

#JFUwajibikaji
πŸ‘5
UBAKAJI NA ULAWITI MBIONI KUKOSA DHAMANA

Serikali inakusudia kurekebisha Sheria ili kuwezesha kuwajibishwa kwa Watuhumiwa wa makosa hayo kikamilifu

> Ni baada ya utafiti kuonesha Watuhumiwa hutoroka au kumalizana na Waathirika kinyume cha Sheria

Soma https://jamii.app/UbakajiDhamana

#JFUwajibikaji
πŸ‘7
KENYA: Jacob Ochola, (62) anayedai kuwa Mtoto wa kwanza wa Rais Mwai Kibaki, amefungua shauri la kutaka kutambuliwa na familia ya Hayati huyo kama Mwanafamilia na sehemu ya Warithi

> Pia, ametaka familia kuweka wazi iwapo ametajwa kwenye wosia

Soma https://jamii.app/KibakisAllegedSon

#JamiiForums
πŸ‘18πŸ€”3πŸ‘Ž1🀯1
RUSHWA YA NGONO VYUONI: UNESCO imezindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma kushughulikia ukatili wa aina hiyo

> Unadhani nini kifanyike kuondoa ukatili wa kijinsia Vyuoni Nchini?

Soma https://jamii.app/UkatiliVyuoni

#GenderViolence #KemeaRushwa #HumanRights
πŸ‘16🀩1
MALEZI: Tabia ya Watoto kupelekwa kwa Babu na Bibi kisha kutojaliwa katika matunzo imetajwa kuongezeka Mkoani Njombe

Inaelezwa, wanaathirika wengi wa ukatili ni wale wanaolelewa na Babu na Bibi zao huku Wazazi wakiwa na migogoro au majukumu mengine

Soma https://jamii.app/HakiZaMtotoNjombe

#HakiMtoto
πŸ‘5😒1
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Rais Kenyatta anamalizia Muhula wake kama Kiongozi wa Kenya, pia ameshakabidhi Uenyekiti wa EAC kwa Rais wa Burundi, Γ‰variste Ndayishimiye

#Governance
πŸ‘11❀1
MAUZO YA NAFAKA: UKRAINE NA URUSI ZASAINI MAKUBALIANO

Ni makubaliano ya kuruhusu mauzo ya nafaka kutoka Bandari ya Bahari Nyeusi ya Ukraine yanayolenga kupunguza uhaba wa Chakula duniani

Vita ilisababisha Bandari kufungwa na kukwamisha usafirishaji

Soma https://jamii.app/RussiaUkraineWar

#FoodSecurity
😁11πŸ‘5
MAREKANI YATOA SILAHA ZA TSH. BILIONI 627 KWA UKRAINE

Msaada unahusisha roketi 4 za HIMARS, ndege 580 ndogo zisizo na rubani, risasi 36,000 za bunduki za M777

> Marekani imetumia jumla ya Tsh. Trilioni 19 kuisaidia Ukraine tangu kuanza kwa vita

Soma https://jamii.app/MsaadKwaUkraine

#Transparency
πŸ€”12πŸ‘Ž8πŸ‘7πŸ‘3πŸ”₯2
CHUNYA-MBEYA: Change Mawanga (32) amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka na kumlawiti Mtoto (4) wa dada yake

Ukatili huo unashamiri Wilayani Chunya kutokana na imani kuwa mtu akibaka au kulawiti mtoto hupata dhahabu

> Nini kifanyike kukomesha ukatili huu kwa Watoto?

Soma https://jamii.app/JelaUbakaji

#HakiMtoto
πŸ‘12