JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIRRO ATEULIWA KUWA BALOZI, WAMBURA AWA IGP MPYA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)

Aliyekuwa IGP, Simon Sirro ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe

Soma https://jamii.app/UteuziIGPMpya

#Governance
👍22😁8🤩5🤬3🤔2
SRI LANKA: Usalama umeonekana kuimarishwa eneo la Bunge wakati Wabunge wakijiandaa kupiga Kura itakayoamua nani atakuwa Rais

Miongoni mwa wagombea watatu wa Urais ni Rais wa Mpito, Ranil Wickremesinghe ambaye anaonekana kutoungwa mkono na Wananchi wengi

Soma - https://jamii.app/UraisKuraSL

#Democracy
👍14😁1
ANGOLA: Hatimaye Watoto wa Rais wa zamani, José Eduardo dos Santos wamekubali baba yao azikwe Mjini Luanda lakini baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 24, 2022

> Hapo awali familia hiyo ilisema Rais huyo alitaka kuzikwa Mjini Barcelona-Uhispania

Soma https://jamii.app/FamiliaDosSantos
👍8😁1
SRI LANKA: Bunge limepiga Kura na kumpitisha rasmi Ranil Wickremesinghe ambaye amehudumu kama Waziri Mkuu kwa mara 6 kuwa Rais wa Nchi hiyo, akimshinda Mpinzani wake mkuu, Dullas Alahapperuma kwa Kura 134 - 82

Wabunge wamemchagua licha ya Raia wengi kuonesha wazi hawamuungi mkono

Soma - https://jamii.app/UraisKuraSL

#Democracy
👍13🤔2😁1
RAIS SAMIA: MFUMO WA TAASISI ZA HAKI JAMII KUFANYIWA MAGEUZI

Amesema miundo ya Taasisi hizo zinazojumuisha Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Magereza na nyinginezo itatazamwa ili kuona kama inaleta ufanisi

Ameeleza, "Tutatizama wale tuliowaamini kwenye maeneo hayo, mifumo yao ya ajira, mafunzo, maadili na nidhamu zipoje"

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#Governance
👍11
RAIS SAMIA: UPANDISHWAJI VYEO JESHINI KUANGALIWA

Akizungumza baada ya uapisho wa Viongozi Rais Samia amesema, "Nimetizama kila ninapokwenda, Mtu anakaribia kustaafu lakini bega lipo tupu. Nikawa nasema upandishwaji vyeo upoje kwenye haya Majeshi?"

Aidha, amesema uhusiano kati ya Raia na Taasisi za Haki Jamii utaangaliwa kwani malalamiko yamekuwa mengi

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#Governance
👍14😢1
RAIS SAMIA: TUTACHUJANA KUJENGA MAJESHI YENYE SIFA

Amesema upatikanaji wa Watenda kazi kwa Majeshi yote utatazamwa ili kujenga majeshi yenye sifa na hadhi ya kusimamia Nchi

Amesisitiza, "Kama yalishapita, huko mbele tutachujana vizuri"

Pia, amegusia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Polisi barabarani akisema, "Hudhani kama ni Mhitimu wa Chuo"

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#JFUwajibikaji
👏13👍5🤮1
KUONGEA MWENYEWE NI HALI YA KAWAIDA?

Kwa mujibu wa Jariba la Medical News Today, ni kuwa mara nyingi mtu kuongea peke yake ni tabia ya kawaida yenye manufaa mbalimbali ikiwemo kukusaidia kutafakari

Hata hivyo, baadhi ya Watu wanaweza kuona kuongea mwenyewe kunaathiri #AfyaYaAkili ikiwa kauli ni hasi na za kujikosoa wakati wote

Fahamu zaidi > https://jamii.app/SelfTalkJF

#JFAfya #PublicHealth
👍18
Mdau wa Jukwaa letu la Ajira ametoa ushauri kuhusu Lugha za Mwili (Body Language) ambazo ni vizuri kuzikwepa au kutozionesha wakati wa Usaili wa Kazi kwa kuwa zinaweza kutoa tafsiri hasi kwa wanaokusaili

Msome hapa - https://jamii.app/ElimuYaAjira

#JFMdau #Ajira
👍18
NIGERIA: Padri John Mark Cheitnum amekutwa amefariki ktk Jimbo la Kaduna ikiwa ni siku chache tangu iliporipotiwa kuwa ametekwa Julai 15, 2022

> Padri mwenzake ambaye walitekwa pamoja, Donatus Cleophas akifanikiwa kutoroka

Soma https://jamii.app/PadriAuawaNigeria
😢12👍8🥰1😁1😱1
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Mwenza wa Urais wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua amesema Rais Kenyatta alijaribu kumtisha kuhusu kumuunga mkono Ruto

> Amesema Kenyatta anatumia Mfumo wa Sheria ya Jinai kukabiliana na wale ambao hawakubaliani naye

Soma https://jamii.app/GachaguaKenyattaSaga

#Democracy
😁4👍2🤔1
TETESI: DE JONG HAUPENDI MJI WA MANCHESTER

Frenkie de Jong wa Barcelona hana mpango wa kujiunga na Manchester United, inadaiwa haupendi Mji wa Manchester na anaamini klabu hiyo haiendeshwi vizuri

> Inadaiwa anaona bora aende Chelsea au Bayern Munich

Soma https://jamii.app/DeJongUpdates

#JFSports
😁16👍6👎2🤔1
Mamlaka katika eneo lililojitenga la Somalia liitwalo Somaliland, zimesitisha shughuli za #BBC zikiishutumu kwa kudhoofisha uaminifu wa Taifa hilo

#Somaliland ilitangaza uhuru kutoka kwa Somalia ktk ya Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe mwaka 1991

Soma https://jamii.app/BBCSomaliland

#PressFreedom
👍8🤔5😁1
URENO: JOTO LASABABISHA VIFO VYA WATU 1,063

Wizara ya Afya imesema kiwango cha juu cha Joto kimefikia Nyuzi Joto 47 kikiwa ni cha juu zaidi kuwahi kutokea Nchini humo

> Pia, Joto kali lilichochea moto wa nyika ambao uliteketeza hekta 45,467 za ardhi

Soma https://jamii.app/JotoKaliUreno

#ClimateChange
👍8🤔4😢2😁1
MALAWI: Watu 76 wamekamatwa katika maandamano ya kupinga Mfumo wa Uendeshaji kesi Mahakamani, wakidai utendaji kazi ni wa taratibu, kuna rushwa na kupanda kwa gharama za maisha

> Pia, Waandamanaji hao walimtaka Rais Chakwera kuchukua hatua

Soma https://jamii.app/MahakamaMalawi

#Accountablity
👍10👎1
MUSEVENI: SIKUSEMA UGANDA IMEINGIA UCHUMI WA KATI

Kufuatia wiki kadhaa za taarifa kinzani zilizohusisha Benki ya Dunia (WB) na Ofisi ya Takwimu ya Uganda (Ubos), Rais Yoweri Museveni amesema kauli aliyotoa awali haikumaanisha Uganda tayari imeshaingia Uchumi wa Kati, bali Taifa hilo linaingia katika ngazi hiyo

Soma - https://jamii.app/MuseveniUG-MI
😁16👍4🤯3😱3
TFF YAMFUNGIA HAJI MANARA MIAKA MIWILI

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Msemaji Klabu ya Yanga, Haji Manara kujihusisha na Mpira wa Miguu ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh. milioni 20

Amekutwa na hatia kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye Fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal, Jijini Arusha

#JamiiForums #JFSports
👍33👎14😁6🤔4😱2🤬1😢1
TANZIA: Msanii wa Filamu nchini, Farida Sabu maarufu kwa jina la 'Bi Sonia' amefariki dunia leo Julai 21, 2022 akiwa Zanzibar

> Muigizaji huyo alijulikana kupitia Kikundi cha Kaole Sanaa Group

Soma https://jamii.app/BiSoniaAfariki

#JFMatukio
😢15
WAZIRI MKUU WA ITALIA AJIUZULU

Mario Draghi amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella baada ya Serikali yake ya Muungano kuvunjika

Hali hiyo imeleta sintofahamu kwa Siasa za Italia, na kuathiri Soko la Fedha. Rais Mattarella amemtaka Draghi kubaki katika nafasi ya usimamizi

Soma - https://jamii.app/ItalyPMResigns

#Governance
👍12🤔1
CHAD: Serikali imepiga marufuku mabinti wadogo kusafiri nje ya Nchi bila Wazazi au Kibali cha Wazazi

> Hatua hiyo ni katika kupambana Biashara Haramu ya Usafirishaji Watu na wimbi la Wasichana wadogo kutumikishwa kingono katika Nchi jirani

Soma https://jamii.app/MabintiChad

#HumanTrafficking
👍15👏2