JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Umoja wa Ulaya umeidhinisha vikwazo vipya dhidi ya #Russia ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kuagiza dhahabu kutoka nchini humo na kuzuia mali za #Sberbank

> Usafirishaji wa dhahabu ndio chanzo kikuu cha mapato ya Urusi

Soma https://jamii.app/NewEuSanctions

#JFDiplomasia
👍8👎7🥰3😁1
KENYA: FACEBOOK YAFUTA MAELFU YA MAUDHUI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Facebook imeondoa machapisho zaidi ya 37,000 yaliyohamasisha chuki na 42,000 kwa kukiuka Sera yake ya ghasia

Pia, imekataa matangazo 36,000 ya kisiasa kwa kutofuata Sheria zake

Soma - https://jamii.app/FacebookKenya

#Kenya2022
👍7
Elimu ya Digitali ni hitaji muhimu la Mafanikio katika mazingira ya sasa

Hata hivyo, Mafunzo na Vifaa katika Shule na Vyuo vingi barani Afrika bado haviendani na kasi ya ukuaji wa Teknolojia

Wanafunzi wengi wanaotaka Ujuzi wa TEHAMA hawana njia nyingine na hulazimika kulipia mafunzo, hali hii ni kikwazo kwa wasioweza kujikimu kimaisha

Soma zaidi > https://jamii.app/UjuziTEHAMA
👍9
SIHA: Madiwani na Mbunge wamekataa kupokea Mradi wa Maji wa Gararagua uliojengwa kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 1.7 kwa madai umejengwa chini ya kiwango

> Meneja wa RUWASA-SIHA amesema hakuna tatizo lolote katika mradi huo na yaliyopo ni ya kawaida

Soma https://jamii.app/MradiSiha

#JFUwajibikaji
👏8👍4🔥2😁1
LINGARD ATIMKIA NOTTINGHAM FOREST

Mchezaji wa zamani wa Man. United, Jesse Lingard (29) amejiunga na Nottingham baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja

Amechagua kujiunga na Klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu licha ya kuwaniwa pia na West Ham United na Everton

#JFSports
😁8👏4👍3👎1🤯1
PAPE SAKHO ASHINDA TUZO YA GOLI BORA CAF

Ameshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka katika Tuzo za CAF. Alifunga Goli hilo dhidi ya ASEC Mimosas, Februari 13, 2022

Amewashinda Gabadinho wa Orlando na El Moutaraji wa Wydad

Soma > https://jamii.app/GoliBoraCAF

#CAFAwards2022 #JFSports
👍349😁2
COLOMBO, SRI LANKA: Vikosi vya Usalama vimevamia kambi ya Waandamanaji na kuwafukuza waliokuwa nje ya Ofisi ya Rais

Baada ya kuapishwa, Rais Ranil Wickremesinghe alionya kuwa watakaoweka makazi kwenye majengo ya Serikali watachukuliwa hatua

Soma https://jamii.app/SLProtestors

#Democracy
👍5👎3
KITU GANI HUSABABISHA CHUKI KAZINI?

Mdau wa JamiiForums.com anasema ni dhahiri Binadamu tunatofautiana, lakini chuki, visasi, ubaya na mengine yasiyopendeza huletwa na nini?

Anauliza: Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo? Unajua zaidi yao na unaonekana tishio? Au inatokea tu Mtu kukuchukia bila sababu ya msingi?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/ChukiKazini

#JFMaisha
👍7🤔4🤩1
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi imesema kukamatwa kwa Wakandarasi wa Smartmatic International BV kutaathiri Uchaguzi kwa kuwa hao ndio Wawekaji na Wasimamizi ya Teknolojia ya Uchaguzi

> Mamlaka hazijaweka wazi sababu za kuwashikilia Wakandarasi hao

Soma https://jamii.app/UchaguziKenya2022

#Kenya2022
👍5🤩5
Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2021 ya Taasisi ya Article 19, #UhuruWaKujieleza unaendelea kupotezwa polepole lakini kwa nguvu kubwa katika maeneo mbalimbali duniani

Bila mtiririko huru wa mawazo na ukosoaji, Jamii haiwezi kuchochea ustawi wa wengi. Katika Nchi yoyote, Raia wanapokosa Uhuru wa Kuzungumza inakuwa ngumu kutatua matatizo yanayohitaji kutatuliwa

Soma zaidi - https://jamii.app/UhuruKujieleza1

#FreedomOfExpression
👍51
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAPINGA KUFUKUZWA CHADEMA MAHAKAMANI

Katika Shauri walilofungua, wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA kuwavua Uanachama baada ya kukubali kuapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum bila ridhaa ya Chama

Soma - https://jamii.app/Wabunge19Kesi

#JFSiasa
👍4🤔1
Pengo kati ya Wanaume na Wanawake katika upatikanaji na matumizi ya Intaneti ni changamoto duniani kote. Asilimia kubwa ya watu Bilioni 2.9 ambao hawafikiwi na Huduma hiyo ni Wanawake na Wasichana

Tatizo hili lipo zaidi kwa Nchi Masikini, ikiwemo zilizopo Barani Afrika ikielezwa baadhi ya sababu kubwa ni Kipato, Eneo na Elimu

Soma zaidi - https://jamii.app/PengoDigitali2

#DigitalRights
😁4👍2
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#Ajira
UGONJWA WA #MONKEYPOX: Wataalamu wa Afya wa #WHO wamekutana kujadiliana kuona kama kuna ulazima wa kutangaza ugonjwa huo kuwa ni hali ya dharura

> Kuna kesi 15,400 za maambukizi ya Virusi hivyo katika Nchi 71 tangu Mei 2022

Soma https://jamii.app/MonkeypoxUpdates

#JFAfya
👍5
DAR: Watu 9 wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na tukio la Ujambazi lililotokea usiku wa kuamkia leo Julai 22, 2022 ktk Kiwanda cha Sheri-Keko, Wilaya ya Temeke

> Wamekutwa na gari (T201 DXN) aina ya Toyota Hiace ikiwa imebeba mali za wizi

Soma https://jamii.app/WahalifuDar
👍7👎1
DODOMA: Serikali imewapa siku 7 Wakazi wa Msalato waliojiorodhesha kudai fidia katika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato wakitambua wao si wamiliki halali wa viwanja, kufuta majina yao Ofisi za Serikali ya Mtaa

> Watakaokaidi watachukuliwa hatua

Soma https://jamii.app/ArdhiDodoma

#JFUwajibikaji
👍5
UBAKAJI NA ULAWITI MBIONI KUKOSA DHAMANA

Serikali inakusudia kurekebisha Sheria ili kuwezesha kuwajibishwa kwa Watuhumiwa wa makosa hayo kikamilifu

> Ni baada ya utafiti kuonesha Watuhumiwa hutoroka au kumalizana na Waathirika kinyume cha Sheria

Soma https://jamii.app/UbakajiDhamana

#JFUwajibikaji
👍7
KENYA: Jacob Ochola, (62) anayedai kuwa Mtoto wa kwanza wa Rais Mwai Kibaki, amefungua shauri la kutaka kutambuliwa na familia ya Hayati huyo kama Mwanafamilia na sehemu ya Warithi

> Pia, ametaka familia kuweka wazi iwapo ametajwa kwenye wosia

Soma https://jamii.app/KibakisAllegedSon

#JamiiForums
👍18🤔3👎1🤯1
RUSHWA YA NGONO VYUONI: UNESCO imezindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma kushughulikia ukatili wa aina hiyo

> Unadhani nini kifanyike kuondoa ukatili wa kijinsia Vyuoni Nchini?

Soma https://jamii.app/UkatiliVyuoni

#GenderViolence #KemeaRushwa #HumanRights
👍16🤩1
MALEZI: Tabia ya Watoto kupelekwa kwa Babu na Bibi kisha kutojaliwa katika matunzo imetajwa kuongezeka Mkoani Njombe

Inaelezwa, wanaathirika wengi wa ukatili ni wale wanaolelewa na Babu na Bibi zao huku Wazazi wakiwa na migogoro au majukumu mengine

Soma https://jamii.app/HakiZaMtotoNjombe

#HakiMtoto
👍5😢1