JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JULAI 7: SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

Siku hii inalenga kukuza matumizi ya Lugha hiyo kama nguzo ya Umoja, Ustawi na Amani

#Kiswahili ni miongoni mwa Lugha zinazotumiwa zaidi Afrika, na kwa Mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) ni kati ya Lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi duniani, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya Milioni 200

Soma - https://jamii.app/SikuKiswahili

#KiswahiliLanguageDay #JFLugha
👍18👏4👎1
#JFDATA: Idadi ya Vijana wasio katika Ajira, #Elimu au Mafunzo (Not in Employment, Education or Training) inaongezeka

Ripoti ya ILO inasema Vijana Barani Afrika wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na Uchumi unaokua lakini usioweza kutengeneza Ajira za kutosha

Serikali zinashauriwa kuandaa Mipango Kazi ya Kitaifa inayolenga #Ajira kwa Vijana

Soma zaidi - https://jamii.app/AjiraVijanaILO
👍8
UINGEREZA: BORIS JOHNSON KUJIUZULU

Kwa mujibu wa BBC, Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatarajiwa kujiuzulu kama Kiongozi wa Chama baada ya Mawaziri wake na Wabunge kutomuunga mkono

Mchakato wa Uongozi mpya utafanyika, na inatarajiwa kufikia Oktoba Waziri Mkuu mpya atakuwa amepatikana. Ripoti za awali zinadai kwa wakati huu, Johnson anadhamiria kuendelea kuhudumu kama Waziri Mkuu

Soma - https://jamii.app/BorisOUT

#Accountability
👍14
SI KOSA ASKARI AKIKUOMBA LESENI UKAWA HUNA KWA WAKATI HUO

Mdau wa Jukwaa la Sheria ndani ya JamiiForums.com anatoa Elimu kuwa Askari wa Usalama Barabarani anapomuomba Dereva leseni barabarani kama akiwa hana kwa muda huo sio kosa Kisheria

Kifungu cha 77 cha Sheria ya Usalama Barabarani kinamtaka Dereva wa Chombo cha Moto kutembea na leseni

Kifungu cha 77(1) cha Sheria hiyo kinasema Dereva ana muda wa siku tatu za kutoa au kuonesha leseni yake, akishindwa hapo ndipo linaweza kuwa kosa

Soma - https://jamii.app/DerevaLeseni

#JFSheria
👍40👏7🔥1🥰1
Mdau ndani ya JamiiForums.com anasema kila mtu anatamani kutimiza malengo aliyonayo hususani ya kuishi maisha bora na salama

Anashauri kuwa na nidhamu ya fedha na kufanya kazi kwa bidii

Msome - https://jamii.app/MdauMalengo

#JFMaisha
👍1310
Waziri wa Afya amewataka Watoa Huduma za Afya Nchini kutolazimisha Chanjo ya #COVID19 kwa Watu wanaofika vituoni kwa ajili ya kupata huduma, kufanya hivyo ni Kinyume cha Miongozo na Maadili ya Taaluma za Watoa Huduma

Soma - https://jamii.app/ChanjoSiLazima

#JFAfya #UVIKO19
👍16👏1
RASMI: BORIS JOHNSON ATANGAZA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU WA UINGEREZA

Boris Johnson ametangaza maamuzi hayo leo Julai 7, 2022 akisema anaacha kazi bora Duniani

> Ataendelea kuwepo ofisini hadi chama chake kitakapochagua Kiongozi mwingine

Soma - https://jamii.app/BorisAjiuzulu

#Accountability
👍23🤔1
MAUAJI YA WATU 7 WA FAMILIA MOJA: Jeshi la Polisi Kigoma limezuia maziko ya James Januari (4) ili kuchukua sampuli ya damu ya mwili huo na pia miili 6 ambayo imeshazikwa inaweza kufukuliwa ili kukamilisha ushahidi wa sampuli ya damu

Soma - https://jamii.app/Miili7Kigoma
👍8😢5
NIGERIA: Watu wenye silaha wameshambulia gereza katika Mji wa Abuja na kusababisha wafungwa zaidi ya 600 kati ya 994 kutoroka

> 300 kati yao wamekamatwa na kurejeshwa, huku juhudi za kuwatafuta wengine zikiendelea

Soma - https://jamii.app/InmatesEscapeInNigeria
👍10
JAPAN: WAZIRI MKUU WA ZAMANI APIGWA RISASI

Shirika la Habari la NHK linaripoti kuwa, Shinzo Abe amekimbizwa Hospitalini baada ya kujeruhiwa kwa risasi mgongoni wakati akitoa hotuba katika Mji wa Nara

Abe alidondoka na alionekana akitoka damu

Soma - https://jamii.app/ShinzoAbeShot
👍12🤔5👎3🤯2
MAN. UTD YAMUACHA RONALDO KATIKA ZIARA

Cristiano Ronaldo ameongezewa muda wa kubaki nyumbani wakati Kikosi cha Manchester United kinasafiri kuanza ziara ya maandalizi ya msimu ujao

> Bado haijajulikana kama Ronaldo atauzwa au la

Soma - https://jamii.app/ManURonaldo

#JFSports
👍7😁2
Mashambulizi yametokea Mashariki mwa DRC kati ya Jeshi la Congo na M23 licha ya Rais wa Rwanda na wa DRC kukubaliana kupunguza uhasama kuhusiana na mapigano hayo

> Pande zote mbili zimekuwa zikishutumiana kuanzisha uchokozi

Soma - https://jamii.app/DRCM23Clashes
👍10
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
👍3
KENYA: Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini humo, Fred Matiang'i ametangaza Siku ya Jumatatu (Julai 11, 2022) kuwa ya mapumziko ili kuruhusu Sikukuu ya Eid El-Adh'haa kusherehekewa

Kwa Tanzania, Sikukuu hiyo imetangazwa kuwa Siku ya Jumapili (Julai 10, 2022) na Sherehe za Kitaifa zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam

Soma - https://jamii.app/EidKenya

#JamiiForums
👍4🤔2😁1🎉1
ALIYEKUWA WAZIRI MKUU WA JAPAN, SHINZO ABE AFARIKI DUNIA

Muda mfupi baada ya Ripoti za kupigwa risasi wakati akihutubia katika Kampeni, Shirika la NHK limeripoti kuwa Shinzo Abe ambaye ni Waziri Mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi Nchini Japan amefariki dunia

Shambulio limetokea katika Mji wa Nara, na inaripotiwa kuwa Mtuhumiwa amekamatwa

Abe (67) alihudumu kama Waziri kati ya 2006 - 2007, na akaongoza tena katika nafasi hiyo kuanzia 2012 - 2020

Soma - https://jamii.app/ShinzoAbeShot
😢20👍4
Issa Said Mbogo (Fundi wa Vifaa vya Umeme) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuchezea Vifaa vya Kudhibiti Mwendo kwenye Mabasi (VTS), akidaiwa kuvuruga mifumo hiyo ili Madereva wa Mabasi waendeshe kwa mwendo kasi

> Amekamatwa Nzega-Tabora

Soma - https://jamii.app/FundiAkamatwa
👍12👏4
GHANA: Wahudumu wa Afya washauriwa kujiandaa na uwezekano wa mlipuko wa #Marburg baada ya kurekodi visa viwili vya virusi vya ugonjwa huo ulio familia moja na Virusi vya #Ebola

> Dalili za Virusi hivyo ni Kuhara, Homa, Kichefuchefu na Kutapika

Soma - https://jamii.app/MarburgVirusGhana

#JFAfya
🤔4👍21
RIPOTI: Kupanda kwa Bei za Vyakula na Nishati kutokana na Vita inayoendelea #Ukraine kumepelekea takriban Watu Milioni 71 kutoka Nchi zinazoendelea kutumbukia katika umasikini

Baadhi ya Mataifa yaliyoathiriwa zaidi ni Burkina Faso, Ghana, Sudan, Haiti, Pakistan na #SriLanka

Soma - https://jamii.app/UNDPReport
😢5👍1👎1
MAHAKAMA YARIDHIA HALIMA MDEE NA WENZAKE KUPINGA KUFUKUZWA CHADEMA

Halima Mdee pamoja na wenzake 18 wameruhusiwa kufungua shauri la kupinga uamuzi wa CHADEMA kuwavua Uanachama baada ya Mahakama Kuu kukubaliana na hoja za maombi yao

Soma - https://jamii.app/MahakamaMdeeCDM

#JFSiasa
😁17👍7👎1
RAIS WA ZAMANI WA ANGOLA AFARIKI DUNIA

José Eduardo dos Santos aliyeongoza Angola kuanzia mwaka 1979 - 2017 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79

Inaripotiwa amefariki Barcelona Nchini Uhispania kufuatia maradhi ya muda mrefu

Soma - https://jamii.app/DosSantosDead
😢10😁6👍5