JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JACK WILSHERE ASTAAFU KUCHEZA SOKA

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 30

Wilshere alikuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara

Soma > https://jamii.app/WilshereAstaafu

#JFSports
👍9
Umoja wa Afrika umezindua Pasi ya Kielektroniki ya Chanjo ya #COVID19 itakayokuwa ni uthibitisho wa kupatiwa Chanjo, na kuwezesha usafiri rahisi ndani na nje ya Afrika

> Pia, inatarajiwa baadaye itajumuisha vyeti vingine kama Homa ya Manjano

Soma - https://jamii.app/VaccineEPassport

#JFAfya
👍12😁1
DRC: Watu 9 wameripotiwa kuuawa katika kliniki baada ya Kundi la Watu kufanya shambulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

> Washukiwa wa tukio hilo ni Waasi wa Kundi la Allied Democratic Forces (ADF) toka Uganda

Soma - https://jamii.app/9WauawaDRC
😢10👍4👎3😱1
MAAMBUKIZI YA COVID-19 UINGEREZA YAFIKIA WATU MILIONI 2.7

Maambukizi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 yanaendelea kushika kasi Uingereza, Ofisi ya Takwimu (ONS) imesema kuwa takribani watu milioni 2.7 wamepata maambukizi

Maambukizi hayo yameongezeka kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Omicron vinavyotambulika kitaalamu kwa majina ya BA.4 na BA.5

Soma - https://jamii.app/COVIDUK

#JFAfya
👍6🤔3🤯1
KENYA: Waziri wa Kilimo amesema kuwa wapo ktk mazungumzo na nchi za Zambia, Tanzania na Uganda ili kupeleka mahindi nchini humo ktk kupunguza makali ya kupanda kwa bei ya unga wa mahindi na kupunguza mfumuko wa bei

Soma - https://jamii.app/KenyaMahindi
👍15😁6👎2🤬1😢1
#JFDATA: Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Mawasiliano (ITU), 5% ya watu Duniani hawajaunganishwa kwenye Intaneti. Aidha, 18% ya watu Barani Afrika bado hawawezi kufikia Huduma hiyo

32% ya watu Duniani wanafikiwa na Mtandao lakini hawapo mtandaoni kwa sababu mbalimbali ikiwemo bei wasizozimudu, ukosefu wa vifaa, ufahamu au ujuzi

Soma - https://jamii.app/HudumaIntaneti
👍6😁2🔥1
TANZIA: Msanii mkongwe wa maigizo, Chuma Suleiman maarufu kama Bi. Hindu amefariki dunia nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam, Leo Julai 09 2022

> Ndugu wa marehemu wamesema sababu ya kifo hicho ni maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu

Soma https://jamii.app/BiHinduAfariki
😢19👍2👎1
KENYATTA: NILITAKA KUACHA URAIS MWAKA 2017

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema alitaka kuacha Urais kisha aende Kijijini baada ya Wapinzani kufungua kesi na Mahakama kuagiza Uchaguzi urudiwe

Naibu wake, William Ruto alimshawishi kutofanya hivyo

Soma - https://jamii.app/KenyattaUrais

#Accountability
👍18🤔4
SRI LANKA: WAANDAMANAJI WAVAMIA MAKAZI YA RAIS

Polisi walifyatua risasi kadhaa hewani kujaribu kuwazuia, lakini jitihada zao ziligonga mwamba

Inaripotiwa kuwa Rais Gotabaya Rajapaksa alishaondolewa eneo hilo na kupelekwa mahali salama zaidi

Soma - https://jamii.app/MakaziRais

#Democracy #Accountability
👍8😁32🥰1
NTHAWA, KENYA: Polisi wanamsaka Mwanaume mmoja kwa madai ya kutengeneza pombe haramu kwa taulo za kike zisizotumika

> Mamia ya lita za pombe hiyo zimekutwa nyumbani kwake zikiwa zimechanganywa na taulo za kike

Soma - https://jamii.app/PombeHaramu
😱10🤩7🤮7🤔5👍4🤯4😁3
Elon Musk ametangaza kuwa atasitisha ununuzi wa #Twitter kwa kuwa kampuni hiyo haikumpa ushirikiano alipohitaji taarifa za Akaunti Feki katika jukwaa hilo

> Aidha, atatakiwa kulipa takriban Tsh. Trilioni 2.3 kwa kuvunja Mkataba

Soma - https://jamii.app/MuskTwitter

#JFTech
😁16👍12
UTEUZI: Habibu Juma Saidi Suluo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA)

Anachukua nafasi ya Gilliard Ngewe aliyemaliza Mkataba. Kabla ya kuteuliwa na Rais Samia, alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu TASAC

Soma https://jamii.app/UteuziLATRA
👍9
RAIS WA SRI LANKA AKUBALI KUJIUZULU

Baada ya maandamano makubwa hatimaye Rais Gotabaya Rajapaksa amekubali kuwa atajiuzulu Jumatano Julai 13, 2022

> Spika wa Bunge ametangaza maamuzi hayo na kuwataka wananchi kutulia

Soma https://jamii.app/RaisSriLanka

#Accountability #SriLanka
👍15👎1🥰1
MDAU: UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA NI UHARIBIFU WA NGUVUKAZI

Anasema Kukosa Ajira kunawafanya Vijana wadumae katika ujuzi wao, wakose matumaini na kushindwa kujiamini

Anashauri kuwepo mifumo jumuishi ya Sera na Mifumo sikivu ya Mafunzo, iliyoundwa kwa kutumia mazungumzo kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri

Msome hapa - https://jamii.app/AjiraVijanaILO
👍7👏1
Tunawatakia wote Heri ya Sikukuu ya Eid-Al-Adha. Iwe Siku ya Furaha kwako na kwa uwapendao

Asante kwa kuendelea kutufuatilia

#EidMubarak
👍143🙏1
SOWETO, AFRIKA KUSINI: 14 WAUAWA KWA RISASI BAA

Watu wenye silaha wameshambulia na kuua watu 14, ikielezwa 12 walifariki papo hapo

Kamishna wa Polisi asema watuhumiwa walianza kufyatua risasi ovyo walipowasili eneo la tukio, na watu 10 wamejeruhiwa

Soma https://jamii.app/14KilledSA
🤔8👎3😢3👍1
STERLING MBIONI KUTUA CHELSEA

Chelsea na Manchester City zimekubaliana kuhusu uhamisho wa Raheem Sterling (27) kwa ada ya £47.5m (Tsh. 132,050,000,000)

Sterling amekubaliana na Chelsea mkataba wa miaka mitano na atalipwa Paundi 300,000 (Tsh. 834,000,000) kwa wiki.

#JFSports
👍8🔥4🥰3
UKRAINE YAMUONDOA BALOZI WAKE UJERUMANI

Hivi karibuni Balozi Andriy Melnyk alinukuliwa akiishutumu Ujerumani kutoisaidia Ukraine silaha katika vita dhidi ya Urusi

#Ukraine imefanya mabadiliko ya Mabalozi katika Nchi kadhaa zikiwemo India na Sri Lanka

Soma - https://jamii.app/BaloziUkraine

#Diplomacy
🤩6👍5🤔2🤯2😁1
MAREKANI, CHINA WAANZA MAZUNGUMZO KUMALIZA MGOGORO

Wanadiplomasia wakuu wamekutana, ikiwa ni jitihada za kupunguza mvutano unaoongezeka kati yao

Ni kikao cha kwanza tangu kuibuka kwa sintofahamu baina ya mataifa hayo yenye nguvu kiuchumi

Soma - https://jamii.app/USChina2022

#Diplomacy
👍12🥰3
RWANDA: Rais Paul Kagame amesema haoni shida akiendelea kuiongoza Rwanda kwa miaka 20 ijayo licha ya huko nyuma kuwahi kunukuliwa akisema hana mpango wa kugombea tena

> Kagame alibadili Katiba kwa kuondoa kipengele cha Ukomo wa kugombea Urais

Soma https://jamii.app/KagameRwanda

#Democracy
👍21👎15😁1