JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa Jukwaa letu la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki (MMU) anasema ni kawaida kwa watu hasa wapendanao kuwa na migogoro ya mara kwa mara

Anashauri kusikiliza ushauri unaopewa na mwenzako badala ya kuwa mbabe, kuwahi kurudi nyumbani, kuzingatia matumizi ya pesa na kumtanguliza Mungu ili kuimarisha mahusiano yako

Msome > https://jamii.app/UshauriMMU
👍15
KATAVI: ANAYETUHUMIWA KUUA KWA KUKODIWA NAYE AUAWA

Heleni Nyankole "Beberu" anayedaiwa kufanya mauaji kwa kukodiwa ameuawa baada ya kugoma kujisalimisha

> Tukio la mwisho alilofanya ni Juni 28, 2022 alipotuhumiwa kumuua Mandalu Ndulu (36)

Soma - https://jamii.app/MauajiKatavi
👍19
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Tunawatakia wote Jumatatu njema! Wiki hii iwe njema kwako

#JamiiForums
🙏8👍7
SRI LANKA: WAANDAMANAJI KUTOONDOKA KWA RAIS HADI AJIUZULU RASMI

Viongozi wa Waandamanaji wamesema wataendelea kubaki katika Makazi ya Rais na Waziri Mkuu hadi Viongozi hao watakapoachia Madaraka rasmi

Rais Rajapaksa hajaonekana na hakutoa kauli ya kujiuzulu mwenyewe. Baadhi ya Ripoti zinadai yupo katika Meli ya Kijeshi

Soma - https://jamii.app/MakaziRaisSL

#Accountability
👍11
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums #Ajira
👍7
WATU WATANO WAUAWA NA WAASI NCHINI DR CONGO

Kati ya waliouawa kuna watoto wanne wa familia moja ambao walichomwa moto hadi kifo, watu wengine wametekwa nyara

> Inadaiwa Waasi wa Alliance Democratic Forces (ADF) wanahusika na matukio hayo

Soma https://jamii.app/5KilledInDRC
😢5👍2👎2
Bondia Tyson Fury amesema yupo tayari kutoka kwenye kustaafu na kurejea ulingoni kupigana na Anthony Joshua kwenye Uwanja wa Wembley, England bila malipo

> Fury alishinda pambano dhidi ya Dillian Whyte, Aprili 2022, na akasisitiza kuwa anastaafu

Soma - https://jamii.app/FuryJoshua

#JFSports
👍41
KILIMANJARO: Ngatipa Parmao (17) anadaiwa kuuawa kwa risasi na Askari wa Wanyamapori Julai 6, 2022 ktk Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

> Familia ya kijana huyo imedai kuna njama zimefanywa kuondoa risasi mwilini kwa mtoto mwake ili kupoteza ushahidi

Soma https://jamii.app/MauajiHifadhini

#JFMatukio
😢11👍1🔥1
JULAI 11: SIKU YA KIMATAIFA YA IDADI YA WATU

Idadi ya watu duniani ilifikia Bilioni 7 mwaka 2011, na kwa mujibu wa UN idadi hiyo itafikia Bilioni 8 Mwaka 2022

Hata hivyo changamoto mbalimbali zilizoikumba dunia miaka 11 iliyopita zikiwemo Mabadiliko ya TabiaNchi, Ukatili/Unyanyasaji na Ubaguzi bado zinaendelea

Soma - https://jamii.app/IdadiWatuDuniani

#WorldPopulationDay
👍10🔥1🎉1
#DIGITALRIGHTS: Huduma ya Intaneti imegusa karibu kila nyanja ya maisha, ikiwemo Huduma za Umma. Kutokana na umuhimu wake, Umoja wa Mataifa ulipendekeza ufikiaji wa Intaneti kuwa sehemu ya #HakiZaBinadamu

Hata hivyo, baadhi ya makundi yameendelea kuachwa nyuma kutokana na migawanyiko mingi ya kidigitali kati ya Wanaume na Wanawake, Vijana na Wazee, Miji na Vijiji

Soma - https://jamii.app/HudumaIntaneti
👍5
SIHA, KILIMANJARO: Watu 9 wamejeruhiwa ktk vurugu kati ya Wakulima na Wafugaji baada ya Wafugaji kudaiwa kuingiza mifugo iliyoharibu zaidi ya ekari 1,800 za ngano na maharage

> Watu hao wamejeruhiwa walipokuwa wakizuia mifugo kuingia shambani

Soma - https://jamii.app/VuruguSiha

#JFMatukio
👍5🤯2🤔1
DODOMA: Shule za Sekondari zimetakiwa kufunga 'CCTV Camera' ili kusaidia kubaini wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu ktk maeneo ya shule

> Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ametoa agizo hilo baada ya matukio ya wizi na uharibifu wa miundombinu kuenea

Soma - https://jamii.app/KameraShuleni

#Governance #JFUwajibikaji
👍12😁1🎉1
#ANGOLA: Mzozo mkubwa unadaiwa kujitokeza baada Serikali kupanga Mazishi ya Kitaifa ya Rais Mstaafu #JoseDosSantos nchini humo huku familia yake ikisema Baba yao alitaka kuzikwa Barcelona na kutaka matakwa ya baba yao yaheshimiwe

Soma https://jamii.app/MzozoMsibaAngola

#JFDiplomasia
👍6🤔6👏1😁1
CHINA: Mamlaka za Jiji la #Macau zimeamuru kufungwa kwa wiki moja kwa biashara zisizo muhimu zinazojumuisha zaidi ya 'Casino' 30 baada ya visa 1,536 vya #COVID19 kurekodiwa tokea Mwezi Juni

> Takriban Watu 19,000 Jijini humo wamewekwa karantini

Soma https://jamii.app/CasinoKufungwa
👍3
UTAFITI: KUONGEZEA CHAKULA CHUMVI HUPUNGUZA MIAKA YA KUISHI

Utafiti uliohusisha Waingereza wapatao 500,000 umebaini kuongeza chumvi kwenye Chakula kilicho mezani (Chakula kilichopikwa tayari) kunahusishwa na kifo cha mapema

Watafiti wamesema kuongeza chumvi kila wakati kwenye Chakula hupunguza zaidi ya miaka miwili ya kuishi kwa Wanaume na mwaka mmoja na nusu kwa Wanawake

Soma - https://jamii.app/ChumviChakula

#JFAfya
👍10👎6
MWANZA: Wakili wa 'Mfalme Zumaridi' amewasilisha ombi la kumkataa Hakimu Monica Ndyekobora na kudai kuwa, Mteja wake hana imani na Hakimu huyo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza

> Kesi imeahirishwa hadi Julai 18, 2022

Soma https://jamii.app/ZumaridiHakimu
😁6👍4🤔4
UPIMAJI DNA: Anayetaka kupima Vinasaba (DNA) ili kujua Uhalali wa Mtoto atalipia Tsh. 100,000 na hilo litatimia baada ya kufuata taratibu zinazotakiwa

> Mhusika atatoa taarifa kwa Afisa Ustawi wa Jamii ambaye ndiye atatuma maombi kwa Mkemia Mkuu

Soma https://jamii.app/KupimaDNA

#PublicHealth
👍14
DAR: MKURUGENZI WA JIJI ASIMAMISHWA KWA UBADHIRIFU

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar, Jumanne Shauri na watumishi wengine 9 wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Tsh. Bilioni 10

Ukaguzi umebaini Fedha zilikusanywa na hazikuwasilishwa Benki kama Sheria inavyoelekeza

Soma - https://jamii.app/MkurugenziDar

#JFUwajibikaji
👍8
URUSI: Rais Vladimir Putin ametia saini amri ya kurahisisha mchakato wa kupata Uraia wa Urusi kwa raia wa Ukraine

> Awali, utaratibu huo ulitumika kwa wakazi wa maeneo ya Mashariki mwa Ukraine ambayo ni Washirika wa karibu na Urusi

Soma https://jamii.app/UraiaWaUrusi
👍19🤔1
#UGANDA: RAIA WAANDAMANA KUPINGA GHARAMA ZA MAISHA

Maandamano ya kupinga ongezeko kubwa la bei ya vyakula, mafuta na bidhaa nyingine yamesababisha ghasia. Polisi wamefyatua mabomu ya machozi na kukamata waandamanaji 8

Mara kadhaa, Rais Yoweri Museveni amepuuza wito wa kupunguza Kodi, na badala yake amewataka Raia kuwa na matumizi makini zaidi

Soma - https://jamii.app/ProtestsUG
👍13