JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBEYA: Baadhi ya Waumini wa Usharika wa Mbalizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde, jana Aprili 17, 2022 walimzuia mchungaji, Atupele Mlawa kuingia Kanisani wakimtuhumu kutumia vibaya mali za kanisa

Soma - https://jamii.app/VuruguKKKT
#UKRAINE YAKAMILISHA MCHAKATO WA AWALI KUJIUNGA NA EU

Hatua inayofuata baada ya hapo ni kuanza mchakato rasmi wa kuelekea kujiunga na Umoja wa Ulaya (EU)

Mchakato huo unatarajiwa kukamilika Juni 2022 katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja huo

Soma - https://jamii.app/UkrainekujiungaEU
PEMBA: KESI 42 ZA UDHALILISHAJI WANAFUNZI ZAREKODIWA MWAKA 2021

Udhalilishaji huo ni pamoja na ubakaji, mimba kwa Wanafunzi na ulawiti

Wilaya ya Wete kuna kesi 11, Wilaya ya Micheweni (10), Wilaya ya Chake Chake (10) na Wilaya ya Mkoani (11)

Soma - https://jamii.app/UdhalilishajiPemba
CAG: UTENDAJI KAZI WA NIDA HAURIDHISHI

Ukaguzi wa 2020/21 umebaini NIDA ilizalisha Vitambulisho 1,705,693 huku lengo likiwa Vitambulisho 12,194,307

Aidha, ililenga kuzalisha Namba za Vitambulisho 1,900,000 lakini ilizalisha Namba 1,061,295 pekee

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022
ULINZI WA KIDIGITALI NI HITAJI MUHIMU

Katika zama za hizi za kidigitali, takriban kila mtu anatumia Mtandao/Teknolojia na hii inawapa wavamizi shabaha mpya

Ni muhimu kwa watu na Taasisi kutopuuza mafunzo ya usalama wa kidigitali

Soma - https://jamii.app/UlinziDigitali

#DigitalSecurity
CAG: Ukaguzi umebaini Taasisi 6 zilinunua vifaa na mali za kudumu za Tsh. Bilioni 1.43 ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli lakini hata hivyo hazitumiki

Kumekuwa na ongezeko la mali zilizonunuliwa ambazo hazitumiki ikilinganishwa na Mwaka 2019/20

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022
MAHUSIANO: UNYANYASAJI KIHISIA NI NINI?

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Unyanyasaji huu unahusisha udhalilishaji, kumshusha mtu thamani na kumkosoa mara kwa mara

Mtu anayekunyanyasa kihisia anaweza kutishia kukudhuru

Soma zaidi > https://jamii.app/DomesticAbuse

#DomesticViolence
MAREKANI: David Riston (49), Mkazi wa Maryland ameuawa kwa kung’atwa na nyoka wenye sumu kali aliokuwa akiwafuga nyumbani kwake kwa siri

> Polisi walimkuta amefariki baada ya majirani kutoa taarifa ya kutomuona mtaani

Soma - https://jamii.app/AuawaKwaNyoka

#JamiiForums
MITIHANI YA UALIMU KITAIFA KUSAHIHISHWA KIDIGITALI

Mfumo wa Kidigitali wa Usahihishaji Mitihani ya Kitaifa ya Ualimu ulioandaliwa na NECTA unaanza kutumika mwaka huu

> Waziri wa Elimu amekagua na kuridhishwa na mfumo huo

Soma https://jamii.app/MitihaniYaUalimu

#Technology
#CAGReport2022 imebainisha kuwa Balozi 6 katika mwaka wa fedha 2020/21 zilinunua bidhaa na huduma zenye thamani ya Tsh. bilioni 1.86 ambazo hazikuwa katika mipango ya manunuzi ya mwaka ya Balozi husika na hivyo kuisababishia Serikali hasara

Soma: https://jamii.app/CAGReport2022
DAR: Paroko wa Parokia ya Mt. Yohanne Paul II, Francis Kangwa amefariki na mwili wake kukutwa kwenye tanki la maji nyuma ya nyumba ya Mapadri wa Shirika la Missionaries of Africa iliyopo Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph-Posta Aprili 12, 2022

Soma: https://jamii.app/Parokoafariki
MANYARA: Simon Zakaria (58) anashikiliwa kwa tuhuma za ubakaji wa watoto watatu wenye miaka 12-13, Wilayani Hanang akiwemo binti yake

> Binti wa Mtuhumiwa mwenye miaka 12 ndiye aliyeripoti na kuwataja wenzake wawili

Soma - https://jamii.app/BabaAbakaMabinti
#CAGReport2022 imeonesha kuwa Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji limekuwa katika ukarabati kwa takriban miaka 10

> Inaelezwa sababu kuu ni Usimamizi Mbovu wa Mradi

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022

#JamiiForums #JFUwajibikaji
RONALDO AFIWA NA MTOTO WA KIUME

Cristiano #Ronaldo wa Man United ametangaza kufiwa na mtoto wake wa kiume

> Amesema wamebaki na mtoto wa kike, ikumbukwe mpenzi wake, Georgina Rodriguez alikuwa na ujauzito wa mapacha

Soma - https://jamii.app/RonaldoAfiwaMtoto

#JFSports
Licha ya vikwazo vya Nchi za Ulaya kutokana na uvamizi wa Kijeshi kwa Ukraine, Ndege za Emirates zinaendelea na safari za Urusi

Rais wa Emirates, Clarke amesema wenye uwezo wa kuzuia safari hizo ni Serikali ya UAE

Soma - https://jamii.app/NdegeZinaendaUrusi
NEW YORK: RAIS SAMIA ASHIRIKI UZINDUZI WA 'THE ROYAL TOUR'

Filamu hiyo inamshirikisha Rais Samia kama mhusika mkuu akiwa katika vivutio mbalimbali vya Utalii #Tanzania

Inalenga kuongeza Watalii na kuvutia Wawekezaji Nchini

Soma - https://jamii.app/UzinduziRoyalTour

#RoyalTourTanzania
URUSI: WATU 200,000 KUPOTEZA AJIRA KUTOKANA NA VIKWAZO

Kampuni kadhaa hususani za Magharibi zimetangaza kusimamisha shughuli au kuondoka #Russia baada ya Rais Vladimir Putin kutuma wanajeshi wake #Ukraine mnamo Mwezi Februari

Soma - https://jamii.app/KupotezaAjiraRussia

#RussiaUkraineCrisis
TETESI: HAALAND MBIONI KUJIUNGA NA MANCHESTER CITY

- Inadaiwa Manchester City imekubaliana na Wawakilishi wa Mshambuliaji Erling Haaland (21) kumsajili mchezaji huyo

- Inaelezwa kuwa Haaland atapewa mkataba wa miaka mitano na usajili unaweza kukamilika wiki ijayo

#JFSports
CAG: MAKUSANYO YA BILIONI 6.53 YALIFANYIKA NJE YA MFUMO WA GePG

Katika Mwaka wa Fedha ulioishia Juni 30, 2021 Taasisi 4 zilikusanya Bilioni 6.53 kama makusanyo yasiyotokana na Kodi nje ya Mfumo wa Kielektroniki wa kufanya Malipo kwa Serikali (GePG)

Soma - https://jamii.app/CAGReport2022
DRC: WANAJESHI WAUA WATU 15 KATIKA MATUKIO TOFAUTI

Wanajeshi wawili wanaosemekana walikuwa wamelewa katika matukio tofauti wamewashambulia raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa risasi na kusababisha vifo 15 wakiwemo watoto

Soma: https://jamii.app/mauajiKongo