JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HASUNGA: TATIZO LA AJIRA LITAKUWA BOMU KUBWA LISIPOWEKEWA MIKAKATI

Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga amesema, "Serikali imesema itatoa Ajira lakini hiyo itakuwa hatua moja. Vijana wanaomaliza ni takriban 90,000 - 100,000 kwa mwaka, kwahiyo haitoshi"

Soma > https://jamii.app/TatizoAjiraTZ
YANGA YAIFUNGA AZAM FC 2-1, YAFIKISHA POINTI 51

Yanga imepata mabao yake kupitia Djuma Shaban na Fiston Mayele. Bao la Azam FC limefungwa na Rodgers Kola

Yanga imefikisha Pointi 51 wakati Azam FC imebaki na Pointi 28

Soma - jamii.app/YangaAzamFC

#JamiiForums #JFSports
DAR: Wananchi wa Mkoa huo na maeneo ya Pwani wametahadharishwa juu ya kununua mafuta ya kwenye madumu kwani wauzaji wanachota baharini

Hiyo ni kutokana na mafuta mengi kumwagika baharini ukanda wa Pwani ikidaiwa yanatoka kwenye meli

Soma - https://jamii.app/MafutaBaharini

#JamiiForums
Marekani imesema inaamini Mali nyingi za Rais Vladimir Putin zimefichwa na Wanafamilia

Kauli hiyo inakuja kufuatia vikwazo vipya dhidi ya Watu wa karibu wa Putin wakiwemo Mabinti zake, Katerina Vladimirovna Tikhonova na Maria Vladimirovna Vorontsova

Soma - https://jamii.app/VikwazoWttPutin
Bodi ya Magavana wa Chuo cha #Academy imetangaza tarehe ya Kikao cha Maamuzi ya Shauri la #WillSmith kumshambulia #ChrisRock kwenye tuzo za #Oscar2022 kuwa ni Aprili 8, 2022

> Aidha, Will alijiuzulu kwa hiyari ktk Chuo hicho Aprili 1, 2022

Soma: https://jamii.app/WillSmith
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby ameishauri Serikali iruhusu uagizaji binafsi wa mafuta

> Asema, Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja unafanya kutokuwepo ushindani wa bei pale inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa na kunakuwa hakuna mbadala

Soma https://jamii.app/MafutaKuagiza
SERIKALI: KUNA ONGEZEKO LA WAGONJWA WA SARATANI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kwa takwimu Wananchi wanaokutwa na maradhi ya Saratani wamefikia 40,000 kila mwaka huku wengi wakiwa ktk hali mbaya kiafya

Soma - https://jamii.app/SarataniOngezeko

#CancerAwareness
ZELENSKY: MAFUTA YA URUSI KUTOWEKEWA VIKWAZO KUNAGHARIMU MAISHA YA WATU

Rais wa #Ukraine amesema Moscow imekuwa inapata Fedha nyingi kutokana na mauzo ya mafuta, hivyo haioni haja ya kuchukulia kwa uzito Mazungumzo ya Amani

Soma - https://jamii.app/OilRussia

#RussiaUkraineWar
KIGOMA: Baadhi ya Madereva wa Bajaji ktk Manispaa ya Kigoma Ujiji wameandamana na kufunga barabara kushinikiza kupandishwa kwa bei za usafiri kutoka Tsh. 500 hadi Tsh. 1,000 kwa wanaochangia usafiri

> Hii ni baada ya bei mpya za mafuta

Soma > https://jamii.app/KigomaNauli
SIKU YA AFYA DUNIANI: Maadhimisho ya mwaka 2022 yanabeba ujumbe "Dunia Yetu, Afya Yetu"

Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa zaidi ya vifo Milioni 13 Duniani kila mwaka hutokana na sababu za kimazingira zinazoweza kuepukika

Soma - https://jamii.app/SikuYaAfya2022

#WorldHealthDay
Bondia mstaafu, Floyd Mayweather atapanda ulingoni Mei 14, 2022 kupigana na Don Moore katika Pambano la Raundi 8 la Maonyesho, Dubai

Mara ya mwisho #Moore kupigana ni 2018 wakati #Mayweather ni 2017

Soma - https://jamii.app/BondiaFloyd

#JamiiForums
MDAU: NINI KINAKWAMISHA WATU KUKUA KIUCHUMI?

Anasema yeye amekuwa mtafutaji kwa takriban miaka 15 lakini maendeleo yake hayalingani na muda huo wa utafutaji

Anaeleza, baadhi ya watu watakwambia, "Acha pombe, Wanawake na starehe"

Je, vitu hivyo pekee ndiyo kikwazo cha kufikia Maendeleo?

Mjadala > https://jamii.app/UchumiMdau
KUMBUKIZI YA MIAKA 50 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMANI KARUME

Rais wa Tanzania; Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar; Dkt. Hussein Mwinyi na Viongozi mbalimbali wameadhimisha Siku hii kwa Dua na kuweka mashada kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume

Karume alizaliwa Agosti 04, 1905 na aliuawa kwa kupigwa risasi Aprili 07, 1972

#KarumeDay
SIMBA YAIFUNGA COASTAL UNION 2-1

Mabao ya Bernard #Morrison na Meddie #Kagere yameipa #Simba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union

Ni katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, leo Aprili 7, 2022

Soma - https://jamii.app/SimbaCoastal

#JamiiForums #JFSports
MKUU WA TRAFIKI: MARUFUKU TRAFIKI NA DEREVA KUZUNGUKA NYUMA YA GARI

Wilbrod Mutafungwa amesema hayo baada ya malalamiko ya rushwa dhidi ya Trafiki wanaosimamisha magari na Madereva au Makondakta kuwafuata na β€˜kumalizana’ nao nyuma ya gari

Soma - https://jamii.app/TuhumaZaRushwa
UN YAISIMAMISHA URUSI KATIKA BARAZA LAKE LA HAKI ZA BINADAMU

Uamuzi huo ni kutokana na uvamizi wake Nchini #Ukraine

Kati ya Wajumbe 193 wa Baraza hilo, 93 walipiga Kura kuunga mkono kusimamishwa Urusi, 24 walipinga na 58 hawakupiga Kura

Soma - https://jamii.app/RussiaSuspended

#JFLeo
#COVID19-TANZANIA: Serikali yasema kuanzia Machi 5, 2022 - Aprili 3, 2022 Visa vipya 116 vilithibitishwa kati ya watu 25,890 waliopimwa

> Dar imeendelea kuwa na idadi kubwa ya maambukizi

> Waliopata dozi kamili ya Chanjo kufikia Aprili 3 ni 3,318,374

Soma - https://jamii.app/VisaVipyaTZ

#UVIKO3
Jaribu mbinu hii ikiwa unapata changamoto ya kupata Usingizi

#JamiiForums #Afya
#MICHEZO: Inaelezwa Klabu ya #ManchesterUnited ipo kwenye hatua za mwisho kumtangaza Erik Ten Hag kuwa Kocha Mkuu akitokea Ajax

Ten Hag (52) atachukua nafasi ya Ralf Rangnick ambaye ni Kocha wa muda tangu Ole Gunnar Solskjaer alipotimuliwa 2021

Soma - https://jamii.app/ManUtdKocha
HASARA NDANI YA KENYA AIRWAYS: SERIKALI KUPUNGUZA WAFANYAKAZI, SAFARI

Shirika la Ndege la Kenya (KQ) litafanya mabadiliko ya kiutendaji kutokana na hasara iliyoletwa na #CoronaVirus

Shirika hilo limetajwa kujiendesha kwa hasara Miaka Miwili Mfululizo

Soma - https://jamii.app/HasaraKenyaAirways