JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFRIKA KUSINI: MFUNGWA KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUPANGA MAUAJI

Rosemary Ndlovu ambaye miezi mitano iliyopita alihukumiwa vifungo sita vya maisha kwa mauaji ya ndugu zake 6 atafikishwa Mahakamani kwa Mashtaka ya kupanga kuua watu wengine watatu

Soma - https://jamii.app/RosemaryMauaji3
MOTO SOKO LA KARUME: Kamanda wa Polisi Dar, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema Vibanda vya Machinga na Mama Lishe zaidi ya 30 vimeteketea kwa moto asubuhi ya leo Aprili 8, 2022

> Pia, baadhi ya vibanda vya Wauza Mabegi ktk soko hilo vimeungua

Soma - https://jamii.app/MotoKarume
Kuendelea kushuka kwa kasi ya utekelezaji wa Mapendekezo ya CAG katika Mashirika ya Umma na Serikali Kuu kunaondoa ufanisi wa uendeshaji wa Taasisi hizo

Kutotekelezwa Mapendekezo ya CAG kunapelekea upotevu wa Fedha za Umma

#JamiiForums #JFUwajibikaji #WAJIBU #Accountability
BUNGENI: Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga amesema Askari wa Maliasili wamekuwa na tabia ya kukamata watu na kuua akihoji, "Miongozo inaruhusu kumkamata Mtu na kumuua?"

Spika Tulia aagiza apeleke swali la msingi ili majibu yatolewe

Soma - https://jamii.app/MauajiRaia

#JFLeo
#SENSA2022: Rais Samia ametangaza Agosti 23, 2022 kuwa tarehe ya kuanza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

Amesema, "Kuna wanaoamini kuhesabiwa ni nuksi. Serikali isingependa kusikia kuna asilimia ya watu haikuhesabiwa. Hii si nzuri kuweka ktk Ripoti"

Soma - https://jamii.app/NemboTareheSensa
DODOMA: Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema anachojua Ndugai hayupo Bungeni na inawezekana atakuwa Jimboni kwake, lakini yeye hana barua rasmi ya kutokuwepo kwake katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea tangu kuanza Aprili 5, 2022

Soma - https://jamii.app/JobNdugai
BURKINA FASO: Roch Kabore, aliyekuwa anatumikia kifungo cha nyumbani tokea alipopinduliwa Nafasi ya Urais ktk Mapinduzi ya Kijeshi mwezi Januari, ameruhusiwa kurejea katika nyumba ya familia yake, kwa mujibu wa Serikali ya Mpito ya nchi hiyo

Soma > https://jamii.app/BurkinaFasoRais
#KENYA: MAHAKAMA YARUHUSU WANAUME KULEA WATOTO CHINI YA MIAKA 9

Mahakama imeruhusu Wanaume kupewa Malezi (Custody) ya Watoto walio chini ya Miaka tisa

Mahakama yasema wajibu wa Mzazi haufai kwenda kwa Wanawake tu Watoto wakiwa wadogo

Soma - https://jamii.app/Custody9KE
#HakiMtoto
TARURA yasitisha faini za kuanzia Machi 1, 2022 na kuendelea kwa Watumiaji wa Maegesho waliopitisha siku 14 bila kulipa ushuru

> Aidha, Watumiaji wa maegesho wataendelea kulipa ushuru ndani ya siku 14 tangu walipotumia maegesho kama kawaida

Soma: https://jamii.app/TaruraUshuruSitisha

#JFLeo
JAPAN YAPANGA KUPUNGUZA UAGIZAJI MAKAA YA MAWE TOKA URUSI

Ikiwa Nchi ya tatu kwa ukubwa wa uagizaji duniani, Japan imesema inapunguza uagizaji wa Mafuta na Makaa ya Mawe taratibu huku ikitafuta Wasambazaji Mbadala kufuatia vikwazo dhidi ya #Russia

Soma - https://jamii.app/JapanUrusi
CHOCOLATE YA KINDER JOY YADAIWA KUWA NA BAKTERIA WA SALMONELLA

Baadhi ya Mataifa ya Ulaya yameondoa Madukani Chocolate ya Kinder Joy kutokana na hofu za Kiafya kwa Watoto

#Salmonella husababisha kuhara, kupanda kwa Joto na maumivu ya Tumbo

Soma - https://jamii.app/KinderJoyBacteria

#Afya
MECHI SIMBA NA ORLANDO: Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeruhusu Mchezo wa Simba SC dhidi ya Orlando Pirates kuingiza mashabiki 60,000 kwenye Uwanja wa Mkapa mnamo Aprili 17, 2022

Itakuwa Mechi ya 1 #Tanzania kutumia Teknolojia ya VAR

Soma - https://jamii.app/SimbaVAR
#Sports
#KENYA: Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022, Mamlaka imetangaza orodha ya maneno ambayo sasa yatachukuliwa kama Matamshi ya Chuki

Baadhi ni Chunga Kura, Watajua Hawajui, Wakuja, Mende, Kama Noma Noma na Operation Linda Kura

Soma - https://jamii.app/HateSpeechWords

#KenyaElections2022
KIFO SPIKA WA UGANDA: BABA ASEMA MWANAYE ALIPEWA SUMU

Spika wa Bunge la #Uganda, Jacob Oulanyah alifariki Dunia Machi 20, 2022 akiwa Marekani akipatiwa Matibabu

Mzee Nathan Okori amesema Sumu iliathiri Afya ya Mwanaye ndio maana hakuweza kupona

Soma - https://jamii.app/UgandaSpikaSumu
PROF. KITILA MKUMBO: BAJETI IELEZE INAVYOSHUGHULIKIA MFUMUKO WA BEI

Mbunge wa Ubungo ameishauri Serikali ipunguze kodi ya Mafuta kuanzia Tsh. 300 hadi Tsh. 400 kwny Tsh. 792 inayotozwa, ili kupunguza mfumuko wa bei ambao unaongeza gharama za Maisha

Soma - https://jamii.app/KitilaMfumuko
Karanja Matindi, Raia wa #Kenya anayeishi Uingereza ameifungulia mashtaka Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwa kuagiza watumiaji wote wa laini za Simu kujisajili upya

Matindi anasema kujisajili upya kwa kufichua idadi ya namba za Simu, taarifa za mtumiaji na kutumia picha za wateja ni kinyume cha Sheria na inakiuka #Katiba

Soma - https://jamii.app/UsalamaWaSimu

#DigitalRights
MDAU: MPE MTOTO UFAHAMU WA KUTOSHA TANGU AKIWA MDOGO

Anasema Watoto wakianza kuongea huwa na maswali mengi, hivyo usimchoke. Ukiamka asubuhi akikuuliza unakwenda wapi mweleze kwa kiwango cha uelewa wake unakwenda Kazini na faida zake ni zipi

Akiharibu kitu usiwe mwepesi wa kumpiga kila wakati bali mweleze umuhimu wa kifaa hicho na shida mtakayopata kikiharibika.

Soma - https://jamii.app/UfahamuWatoto
#Malezi
MITANDAO SALAMA: Ili kufanya mtandao kuwa sehemu salama kwa kila mmoja:

- Ni vema kumtendea kila mtu unayeungana naye mtandaoni kwa hadhi na heshima

- Ni muhimu kutambua tofauti za kitamaduni na kuheshimu mitazamo tofauti

- Epuka kuwashambulia wengine kwa mambo binafsi

Soma > https://jamii.app/UsalamaMitandao1

#InternetSafety
WILL SMITH MARUFUKU KUHUDHURIA OSCARS KWA MIAKA 10

Amepigwa marufuku kuhudhuria au kujihusisha na shughuli za Academy kutokana na kumshambulia #ChrisRock usiku wa tuzo za #Oscars2022

> Marufuku haitahusisha kuwania au kushinda tuzo hizo

Soma - https://jamii.app/WillSmithOscar
Mijadala mbalimbali inayoendelea www.JamiiForums.com