JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
China imetangaza maambukizi mapya 13,146 ya #COVID19 ambayo yametajwa kuwa ni makubwa kuliko yaliyowahi kuripotiwa tangu Februari 2020

> Maelfu ya Watu wamewekwa karantini na hakuna kifo kilichorekodiwa hadi sasa

Soma https://jamii.app/Corona13146
JamiiForums inawatakia Waislamu wote pamoja na Watanzania kwa ujumla mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Mwenyezi Mungu akujalie Funga yenye Kheri na Baraka.

#RamadanKareem2022
DAR: Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar

> Tukio hilo limetokea leo Aprili 3, 2022

Soma - https://jamii.app/WafukiwaNaKifusi

#JamiiForums
πŸ‘1
#CAF: SIMBA YAIFUNGA GENDARMERIE 4-0, YAINGIA ROBO FAINALI

#Simba imeshinda mabao 4-0 dhidi ya Gendarmerie, Uwanja wa Mkapa. Imefikisha pointi 10 katika Kundi D


> Imefuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika

Soma > https://jamii.app/SimbaRoboFainali

#JFSports
ARUSHA: Michuano ya Golf ya Mount Kilimanjaro Klassic iliyokuwa ifanyike Aprili 7-10, 2022 imefutwa huku sababu zikiwa hazijawekwa wazi

> Washiriki wameahidiwa kulipwa Dollar 1,000 (takriban Tsh. 2,300,000) kama gharama ya usumbufu

Soma - https://jamii.app/GolfYafutwa

#JFSports
Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa ya Kuhifadhi #Quran yanatarajia kuanza Aprili 10, 2022 katika Viwanja vya Mkapa, Mnazi mmoja na Diamond Jubilee

Mashindano hayo hufanyika kila Mwaka na kushirikisha Watu kutoka ndani ya Nchi na nje

Soma - https://jamii.app/MashindanoQuran
#RamadanKareem
Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Haki za Binadamu (UN-OHCHR) limeripoti vifo vya raia 1,417 huku 2,038 wakijeruhiwa katika Mgogoro wa Urusi na Ukraine

> Aidha, 121 ya waliouawa ni Watoto

Soma https://jamii.app/RaiaMgogoro

#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
Mwaka 2019/20 CAG alionesha uwepo kwa viashiria vya #Rushwa, Udanganyifu na Ubadhirifu katika usimamizi wa matumizi ya kawaida

Matumizi ya Tsh. Bilioni 34.99 katika Mfuko wa Maendeleo ya #Utalii yalitumika pasipokuwa na nyaraka zilizoidhinishwa

#JamiiForums #Accountability #WAJIBU #JFUwajibikaji
SRI LANKA: Mawaziri wote 26 wamewasilisha barua zao za kujiuzulu usiku wa kuamkia leo kufuatia maandamano ya Raia kuipinga Serikali

> Inaelezwa kuwa, Serikali ilizima Mitandao ya Kijamii ili kuzuia maandamano hayo

Soma - https://jamii.app/SriLankaMinResigns
#Democracy
EWURA: BEI YA MAFUTA ITAENDELEA KUPANDA

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema bei ya Petroli imepanda kufikia dola 1,106 kwa tani 1 kwa Machi 2022 ikilinganishwa na Desemba 2021, tani 1 ya Petroli iliuzwa dola 717

Soma zaidi > https://jamii.app/MafutaKupandaBei
πŸ‘1
DAR: Watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa kukutwa wakikata baadhi ya vyuma vya ngazi ktk nguzo namba P9 kwenye Daraja la Tanzanite lililopo Salender

> Aidha, wengine 10 wamekutwa chini ya daraja hilo wakidai wanaokota vyuma chakavu

Soma - https://jamii.app/HujumaDarajaSalender
DODOMA: Kamati ya Uongozi ya Bunge imeridhia Bunge kuanza kurushwa 'live' kuanzia Aprili 5, 2022 baada ya maboresho ya Studio za Bunge

> Mwaka 2016, Waziri wa Habari, Nape Nnauye alisitisha matangazo ya 'Live' sababu ikiwa gharama

Soma - https://jamii.app/BungeLive
#JamiiForums
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameupa Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili miezi miwili ya kujitafakari kuhusu uwezo wao wa kusimamia ubora wa Huduma za Afya

> Hii ni kutokana na malalamiko kutoka kwa Wananchi kuhusu huduma

Soma - https://jamii.app/MuhimbiliLawama
UPDATE: Jeshi la Polisi linamshikilia Shaibu Kuselela (58), mkazi wa Kijiji cha Lipalwe, Tandahimba kwa tuhuma za kumuua mkewe, Amina Mtausi (40) kisha kumzika shambani

> Tukio hilo liliripotiwa kutokea tarehe 28 Februari 2022

Soma: https://jamii.app/MauajiYaMke
#JFMatukio
MBEYA: Riziki Henry (22) anashikiliwa kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mumewe Ayub Aron (33) na kumsababishia mauti

> Mauaji hayo yanaripotiwa kutokea alfajiri ya tarehe 02 Aprili 2022

Soma: https://jamii.app/AmuuaMumewe
#JFMatukio
BURUDANI: Kampuni ya #Netflix imeripotiwa kusitisha kuonesha filamu mpya ya Will Smith (53) ya β€˜Fast and Loose’ kutokana na kumpiga kibao Chris Rock, kwenye Tuzo za Oscar

Aidha, Kampuni ya #Sony nayo imesitisha muendelezo wa Filamu ya 'Bad Boys 4'

Soma - https://jamii.app/NetflixSonySmith
RWANDA: MAHAKAMA YA RUFAA YAIDHINISHA HUKUMU DHIDI YA SHUJAA WA 'HOTEL RWANDA'

Imeidhinisha kifungo cha miaka 25 badala ya maisha dhidi ya Paul Rusesabagina kama Rufaa ya Upande wa Mashtaka ilivyotaka, ikisema hilo ni kosa lake la kwanza

Soma: https://jamii.app/ShujaaJelaRwanda
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridhiano akisisitiza kujadili mambo yanayoendana na hali ya #Siasa, Uchumi na Mazingira ya Nchi

Asema "Msije mkaja na jambo mna hakika hili Rais hataweza kulitekeleza"

Soma https://jamii.app/SamiaMkutHaki
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar limesema sehemu ya mikakati yake ktk kuzuia biashara ya Wanawake kujiuza ni kuwakamata Wanaume ambao ni wateja

> Kamanda wa Polisi amesema lengo ni kupunguza matumizi ya nguvu kwa Wanawake wanaofanya biashara hiyo

Soma - https://jamii.app/BiasharaHaramu
RAIS SAMIA: Na kwa mipango na jinsi ninavyoiendesha Serikali, nina imani tutakapofika 2025 kama hatujafika, tutakuwa tunakaribia

> Tunatarajia Mwaka 2023 Uchumi utakua kwa 5% na 2024 Uchumi utakua kwa 6.8% kama tulipokuwa kabla

Soma - https://jamii.app/UchumiWaKati

#RaisSamia #Siasa